Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Baada ya kustaafu nifanye biashara gani?

Hichi ndio kinawakuta wastaafu wengi. Nguvu zimeisha, akili imechoka alafu uanze moja na biashara. Sector ambayo imejaa kila aina ya horror unayoifikiria. Kama ni biashara basi ilitakiwa ufanye wakati uko kazini ili hata ukistaafu ni kitendo cha kuendelea tu. Sababu mara nyingi kuanza biashara yoyote ile kupoteza kila kitu ni lazima ili kujifunza na wastaafu wengi huishia wakavu namna hiyo.

Nisikutishe bure mzee, kama una mwanao mkubwa anayejitambua na unayemuamini, mpe robo ya hizo pesa afanye biashara physical(kununua na kuuza) wewe uwe msimamizi au watakuchanganya wakuibie, pesa nyingine iweke kama backup. Alafu kuwa makini na kuomba ushauri mitandaoni, wengi wanaandika tu bila kufikiria na wala sio wafanya biashara, wengi matapeli, ushauri wa biashara omba wafanya biashara unaowajua. Pia kuwa makini na biashara za kuwekeza, mitaani na hasa mitandaoni, matapeli wamejaa kila kona.

Kuna daktari amestaafu kutoka muhimbili nilimkuta anauza mayai kwenye kiduka-genge. Hivyo usitegemee vikubwa sana.
Tatizo la hapa JF kila mtu ni mtaalam wa kila jambo. Na wakati mwingine wauliza maswali kama makoye sr (ingawa simuamini) wanauliza Padre jinsi ya kuishi na mwanamke ndani. Unategemea nini? Padre hajawahi na hatawahi kuoa, atakueleza nini kama si ndoto za alinacha
 
Mimi na mke wangu tulikua tunajadili hili jambo jana usiku ingawa hatujafika 45 yrs.
Nilimwambia kwamba pesa ya kustaafu sio ya kufanyia biashara, kwasababu hatuwezi kujifunza biashara uzeeni wakati over 35yrs tmekua kwenye ajira....
Then tukaja na mambo kadhaa yafuatayo...
1. Tuanze kuandaa shamba kwaajili ya kufanya kilimo na ufugaji tukingali bado tupo kwenye ajira.
2. Tukisha nunua sahamba mahala ambapo tutachagua basi tuanze ahughuli za kuliandaa shamba lile tukingali bado kwenye ajira.
3. Tuanze na kilimo kidogo kidogo ili tuanze kuzowea maisha ya shambani na changamoto zake.
4. Tuweke mifugo michache kwa kuanza kujifunza ufugaji na changamoto za mifugo.
5. Tujenge nyumba ndogo na tuchimbe kisima kwaajili ya kumuweka muangalizi wa shamba na familia yake.
Kumbuka leo ni tofauti na kesho katika Afrika
 
Kwahiyo 80 mio ni ndogo ? Kwa biashara unajua kuna watu wana import kwa 80mio ? Na wanazungusha hiyo hela ?

ama ananunua kwa supplier hapa Tz kwa 80 mio ? Hiyo hiyo kama hujaishi kwenye industry ya biashara ni ngumu kunielewa,
Unafanya biashara wewe..?
 
Jamii forum ni uwanja mpana sana Kuna watu wa Kila aina, ushauri wenu ni wa muhimu sana kwangu naendelea kusoma comments zenu, mwaka mzima nimekaa tu nyumbani sasa nataka niwe na cha kufanya asanteni sana
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Kuna memmber humu alitoa muongozo mzuri sana wa maisha kabla na baada ya kustaafu, ila ile thread siikumbuki ilikuwa na title gani? Labda waombe Admins waipost tena hapa, lakini katikamambo makubwa niliyojifunza ni kuwa makini na aina ya biashara unayoichagua na mazingira utakakoamua kuishi isiwe mjini, nenda nje ya mji ambako utapanua wigo wa kufanya shughuli zaidi za kufuga na kilimo
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Upo mkoa gani?
Unaweza kununua viwanja kwenye skwata huko. Sema majohe nk. Kiwanja ml 10 kisha unajenga chumba na sebule unapangisha. Ml 80 ukiisimamia vizuri hukosi vyumba 10. Kila chumba 150 kwa mwezi
Ni ushauri tu
 
Achana na biashara,sijui ufugaji,achana na kilimo,mazao....
Kwa 80m wekeza kwenye nyumba ya/za wapangaji na fremu(hii ni fixed asset),lenga pato/kusanyo la 1.5m kwa mwezi,nakuhakikishia huta kuja kunisahau

Jenga Rooms 20 (15 za makazi na 5 frame),uswazi room moja kila kitu inakula 3.2-3.5m
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80
 
Ukweli Sina uzoefu na biashara nilmudu kujenga nyumba ya kuishi na nyingine ya kupangisha ndo inanisaidia pamoja na pensheni ya Kila mwezi, asante Kwa ushauri
Sawa kwa kuwa huna uzoefu,achana na wazo la biashara.

Ukiwekeza UTT kwa riba ya around 15% kwa mwaka kwa hiyo mil80 kila mwezi utavuna around milioni 1 na pesa yako ipo palepale.

Sasa ukichukua hiyo mil1 jumlisha na pensheni yako ya kila mwezi unapata pesa fulani nzuri tu ya kukuwezesha kuishi tena kiboss tu hata hutatia huruma,usisumbue ubongo wako sasa hv baba yangu,kula jasho lako bila stress
 
Nimekuwa kazini Kwa zaidi ya miaka thelathini na sita, mwaka Jana nimestaafu nimelipwa mafao yangu nikazifix benk mwaka mmoja baadae nataka nizitoe nifanye biashara, naomba ushauri wenu ziko zaidi ya 80m
Binafsi nikifikia stage ya kuacha kazi nimepanga kuanza biashara ya Hardware na Kirikou kwaajili ya kubebea bidhaa za Wateje(Delivery)pia nitanunua mashine ya kufyatua tofali, option ya pili nitanunua heka kadhaa za shamba nitaanza ufugaji wa Kuku mchanganyiko na mbogamboga kibiashara
 
Back
Top Bottom