Baada ya kumzuga mara tatu bila mafanikio, Rafiki wa kazini bado analazimisha nimfundishe kuchoma kaya, Nichukue uamuzi gani?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni kama rafiki japo naweza kumuita bro, ana miaka 40 na kitu ?

Binafsi hii ndio starehe yangu japo kwa sasa huwa ni stiki mbili ama tatu kwa wiki.

Sasa huyu bro sijui ni kipi kilichomshawishi atake kujaribu haya mambo umri ukiwa umeshaenda mithiri ya jua la saa kumi na moja.

Mara ya kwanza nilidhani utani nikapuuzia tu, mara ya pili akanikumbusha nikaona this is serious lakini bado nikamzuga, Mara ya tatu hii naona ni kama amemaindi kwamba nachofanya hakiko sawa.

Sasa nimefikiria sana hii ishu ni vipi maana kwanza kabisa huyu ni mtu mwenye familia yake ambae hata ofisini ni wle mfano wa kuigwa katika mambo ya family, maadili, n.k.

Napata wakati mgumu sana, upande wa kwanza sitaki kabisa kumfundisha, Binafsi tayari nina uzoefu hata sina uraibu nayo ila kwa huyu mwenzangu nahofia ataanza kustua mara kwa mara maana mwanzoni ukiwa mgeni utatamani tena na tena kustua, kilevi hadi ukizoee inabidi upate uzoefu.

Upande wa pili naona heri nusu shari kuliko shari kamili maana nisipomfundisha anaweza kwenda mutaani, mitaani huko watu wanaigana tu na hawana elimu ya hiki kilevi ndio maana wengi akili huwaruka, kwa upande wangu kabla sijaanza haya mambo nilijielimisha vya kutosha kwa kufunzia kwa wenzetu jinsi ya kutumia kwa njia sahihi, nachoogopa huyu mwenzangu akijifunzia mtaani bila elimu inaweza kumdhuru kwa namna hizi:
  • Mitaani huwa zimepuliziwa dawa za kuzibusti ama mambo mengine, Hii hufanya wengi kushuka uwezo wa kufikiri.
  • mzigo wa mitaani mingi hata wakulima hawajui wanacholima, mzigo unaukuta una mambegu kama yote na ukizivuta nguvu za kiume zinapungua, mzigo haujakomaa umevunwa haraka kwa tamaa ya pesa ama hofu ya kukamatwa, mzigo umeshaharibika hauna unyevu kabisa, haya ni mambo ambayo yapo kinyume kabisa na kilevi hiki na wengi hutumia bila elimu matokeo yake waweza kuanza ona mambo yasiyokuwepo.
 
Back
Top Bottom