Nimeibiwa takribani laki 5 na Binti wa duka langu jipya ndani ya miezi miwili. Nichukue uamuzi gani?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

JUMLA NIMEBONDWA 477,000/=

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu ni mwendo wa dakika 20 tu kutembea hivyo hagahramiki usafiri.

Kumfukuza naweza ila ni haiwezi rudisha hasara, nae alambe joto la jiwa kurejeshe hasara kwa namna moja ama nyingine.(kwa wale mnaodhani kwamba kumla mwanamke ni adhabu mjitafakari upya, ni nonsense ego ya wanaume wenye akili fupi kudhani kwamba mwanamke utamuumiz kwa kitu alichoumbwa kukimudu)

Ushauri nilioupata na naenelea kupokea

Hadi sasa nimeshauriwa na wanajamii forums rikiboy, Auz, Nshomile wa Muleba na Glenn wameshauri kwamba arejeshe deni na si kuondoka sawa na kumsamehe, Binti atabaki kwa makubaliano kwamba simwambii mama yake ila ntakuwa namkata mshahara elf 50 kila mwezi, nikisema nimfukuze nilete mwingine ntaanza upya kuibiwa, bora shetani unaemjua kuliko malaika usiemfahamu, binti ni muoga amekiri na kutubu bila majibishano hii ni advanyage kuliko angekuwa jeuri, nimeona nimsamehe na kumpa nafasi ya pili huku nikiongeza umakini zaidi ila kwa upande mwengine nae atatumia nguvu kubwa kujaribu kurudisha imani yangu kwake.

na hii ndio mbinu inayotumika hata na wahindi japo lengo ni moja kurejesha pesa ila mbinu yao ni ya tofauti wanakupeleka polisi utakaa huko hadi ndugu zako warejeshe hasara uliyosababisha. ushauri 1 ushauri 2 ushauri 3 ushauri 4 ushauri 5
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha,

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Nimfanye nini huyu binti iwe funzo kwake kwamba vya watu si vya kugusa gusa ?
Nipm namba yake,nikimkula nakulipa.Usisahau picha yake
 
Ni duka langu jipya nililofungua mwezi wa tatu, kwakuwa mimi ni muajiriwa niliona nitafute binti awe anakaa hapo, mimi tunawasiaana nae ila napitiaga baadhi za siku jioni na weekend.

Binti ana miaka 23, mama yangu mdogo ndie alienisaidia kumpata maana ni majirani, ni binti ambae sikudhania kabisa atanifanyia hivi maana mara kibao nikieda dukani namkuta anasoma vitabu vya dini yake na anavaa kwa staha, niliwahi kumuona boyfriend wake siku moja ni kijana wa 25 hivi, kwa uvaaji wake sikuona kama wanaenda na huyu binti na nahisi anahusika kumfundisha huyu binti mbinu za kunitwanga.

huwaga nikienda dukani pesa ya mauzo huwa naiweka kwenye draw chumba cha nyuma, sasa sijui niseme ni kumwamini sana binti au uvivu wangu, nikawa naweka kwenye draw tu, na kuna mara chache sana nilikuwa nachukua elf tano tano hizi, sasa baada ya wiki 2 hivi naenda kuchukua pesa niende kuiweka benki, nikabaki nashangaa ni kama elf 50 hivi haipo, dahh!! nikaona labda ni zile pesa ndogo ndogo nachukua hazipo ila nikichekecha kichwa nakumbuka nilishazifanyia hesabu, niliona wazi hapa nimepigwa ila sikutaka kuwa na haraka nikasema kama nahisi ni binti basi niwe na ushahidi usio na shaka.

nikachukua uamuzi wa kuhesabu mzigo mzima wa dukani, juzi hapo nimeshinda dukani nacheki balance ya kila kitu kilichotoka ili kujua vingapi vimebaki, sasa ipo hivi mimi nina madaftari manne la kwanza ni la bidha zinayoingia au kurudishwa na zile zinazotoka iwe ni kwa cash, mkopo, matumizi binafsi au kutupwa zikiharibika, hili daftari kila bidhaa ina kurasa zake ili kujua balance yake ya stock. la pili ni daftari la pesa iliyoingia iwe ni mauzo ya cash au marejesho ya bidhaa zilizouzwa kwa mkopo, la tatu ni la madeni pamoja na marejesho yake, la nne ni bidhaa zilizochukuliwa kwa matumizi binafsi ama zilizoharibika.

Sasa nilishazoea nilikuwa natumia hilo daftari la kwanza la mizigo inayotoka na kuingia kuhitimisha balance, hapa nikifika dukani nilikuwa nategemea daftari hili zaidi bila kufanya reference ya madaftari mengine, binti kumbe akanisoma akaanza kamchezo baadhi ya bidhaa anaandika zimetoka na kweli zina balance ila haandiki kwenye madaftari ya cash, madeni au lile la matumizi binafsi. mimi nikawa naonaga mambo yapo sawa tu nikitizama daftari la kwanza.

Sasa juzi hio baada ya kuona nina kashoti kwenye hela nilizotunza nikahisi nachapwa, sikutaka kumpa tuhuma kirahisirahisi, nilitaka niwe na ushahidi usio na shaka, nilifika dukani mapema sana jioni saa 10 nikaanza kuangalia kila kilichotoka napiga tiki kama kipo kwenye madaftari yale matatu, nikiona bidhaa imetoka ila haipo kwenye madaftari mengine sipigi tiki, hapa bidhaa ambazo hazikuwa na tiki zilikuwa na thamani ya 147,000.

Kuna watu huwa wanakopa na hawa mara nyingi tunajuana, sasa kuna deni moja mteja alileta downpayment ya elf 80 akasema atamalizia laki siku zijazo, ni deni la mda kidogo, nikampigia simu akaniambia alishalipa, nae binti hapo akaanza kiswahili eti alisahau kuandika, nikaona huyu bado nnae wacha nifanye ukaguzi wa ziada.

Nilizoea kuhesabu mzigo kwa macho, Siku hio nilifungua kila box naangalia ndani, nikaona kwamba kuna box mbili za kati zimeweka maplastiki tu ila zina uzito unaofanana na bidhaa zake, sikusema kitu ila hali ya binti huku chini usoni ilikuwa ni tete,

Sikuamini kabisa nilichokiona kwa huyu binti maana sikuwahi kumdhania kabisa, alibaki tu kainama analia sana, nikamwambia aende kutafakari huko nyumbani, akawa ananisisitiza sana kuniomba nisimwambie mama mdogo maana atasema kwa mama yake.

Jumla ya hasara niliyopata,

Mizigo ambayo imetoka ila haimo kwenye rekodi ya mauzo - 147,000.
Madeni yaliyorejeshwa ila hayajarekodiwa - 100,000.
Maboksi yaliyojazwa plastiki bidhaa hazipo - 180,000
Pesa niliyoweka kwenye bahasha na kukuta imepungua - 50,0000

JUMLA NIMEBONDWA 477,0000

Mshahara wa binti ni laki 1 kila mwezi. kila siku ana allowance ya elfu 3. anaishi karibu na duka ni mwendo wa dakika 20 kwa kutembea.

Ishu inakuja kwamba Huyu binti kama nilivyosema ni mtoto wa jirani wa mama mdogo, sitaki kukurupuka niwavunjie ujirani wao.

Nadeal nae vipi huyu dogo ?
Kama yuko tayari, usimwambie Mama yake kama alivyoomba, aendelee kufanya kazi kwa ufuatiliaji wa karibu, mlipe nusu mshahara mpaka deni lilipwe.
 
Back
Top Bottom