Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha Star TV kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.

"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."

"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabega na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi.

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo.

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda.

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku.

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka, hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli? Arudi ili nije kupata stress tena?

Ndoa..........mh!
Pole sana mkuu. Inaudhi sana unapambana kwa ajili ya familia afu unakuta wife anakuletea maudhi ya kithenge.
 
n
kwa sababu unatumia nguvu kubwa kumtetea huyo mwanamke aliyekuwa anashirikiana na hg kula ganchi kwa mumewe, kama ulisoma comment yangu ya kwanza na kuilewa, concern yangu kwa hyo mama wa kwenye daladala sio kula ganchi au kubana hela, kilichonichosha ni yeye kushirikiana na hg kula ganchi ya hela ya matumizi.
WEKA PALE TUNAPOWEKAGA.
i kawaida sana mkuu....nakushanga umeichukulia in a negative way
 
Basi asililize hata radio tu. Aache ufala wa vitu vidogo vidogo, kazi ya mume ni kuhudumia familia na sio kugombania remort ya TV na watoto, mimi hata kuwasha TV siku hizi siwezi,
mwanaume wa kwanza kwenye huu uzi...kongole..wewe ni Mwanaume halisia..nashangaa kugombania tv na wife
 
Back
Top Bottom