Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha Star TV kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.

"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."

"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabega na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi.

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo.

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda.

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku.

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka, hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli? Arudi ili nije kupata stress tena?

Ndoa..........mh!
 
Wewe umeoa gube gube. Huyo hata umuweke kwao miaka 10 hatoacha tabia yake.

Usitarajie mabadiliko yeyote toka nyumbani kwao maana huko ndipo penye chimbuko la tabia zake mbovu. Cha zaidi tarajia kuongezeka kwa tabia mbaya akirudi maana sasa yupo mafunzoni.
 
Wanawake wana mambo sana, kuna siku kwenye daladala mama mmoja akapiga simu alikuwa anaongea na house girl nadhani, akamuuliza baba kakupata sh ngapi ya matumizi....akaendelea basi sawa tumia elfu saba tu hyo elfu tatu weka pale tunapowekaga. Nilichoka na kuchoka mke anashirikiana na house girl kula ganchi kwa mumewe.
 
Wanawake wana mambo sana, kuna siku kwenye daladala mama mmoja akapiga simu alikuwa anaongea na house girl nadhani, akamuuliza baba kakupata sh ngapi ya matumizi....akaendelea basi sawa tumia elfu saba tu hyo elfu tatu weka pale tunapowekaga. Nilichoka na kuchoka mke anashirikiana na house girl kula ganchi kwa mumewe.
Mkuu hiyo yote ni umasikini wa kipato kwa wanawake wake wetu, chanzo chake kutoka kwenye familia yao huko, Yani ata mumewe awe na uchumi wa kati bado mke angemuibia tu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;........

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha StarTv kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.......
"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."
"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabegi na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi....

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo....

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda....

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku....

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka.....hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli?!!!!! Arudi ili nije kupata stress tena?!!!!!!!

Ndoa..........mh!
Bado mna utoto.Mmeoana mwaka mmoja tu ndiyo unaweweseka?Mkwe bado haujakua.
 
Back
Top Bottom