SoC02 Azam Tv ni Funzo tosha kwa Wajasiliamali na Wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara

Stories of Change - 2022 Competition

Malle_Hanzi

Member
May 24, 2011
5
3
Na
Malle Hanzi
_______

Mwanzoni mwa miaka ya kuanzia 2010 kuja 2020, Tanzania ilibadili mfumo wa urushaji wa matangazo ya vituo vya Luninga kutoka Analojia kwenda Dijitali.

Sababu kuu ya kuhama kutoka Analojia na kwenda mfumo wa Dijitali ni upungufu wa masafa (frequency) uliotokea kuanzia mwaka 2000. Katika mfumo wa Analojia, Chaneli moja ya TV ilikuwa inarushwa katika frequency moja, wakati katika mfumo wa dijitali, frequency moja ina uwezo wa kurusha chaneli 15-18 au 20-25, ikitegemeana na teknolojia gani mrusha matangazo anatumia (DVB-T au DVB-T2). Hivyo Umoja wa warusha matangazo duniani na wanachama wake waliweka azimio la kuhamia mfumo wa Dijitali.

Fursa.
Kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa, fursa ya biashara iliyokuwa inaonekana mbele yao ni uuzaji wa visimbuzi/ving’amuzi. Ingawa kulikuwa makampuni ya Cable Televesion; lakini kwa takwimu zisizo rasmi soko la visimbuzi lilikuwa limetawaliwa na kampuni ya Dstv na kufuatiwa na Startimes.

King’amuzi cha DSTV kilianza mwaka 1995 kikimilikiwa na kampuni ya Multichoice ya Afrika ya Kusini kikihudumu nchi 9 barani. Startimes ilianza mwaka 1988 nchini China na kinahudumu nchi 7 barani Africa.

Tulishuhudia makampuni kadhaa yakianzisha visimbuzi vyao ambavyo vilitaka kushindana Startimes pamoja na Dstv. Visimbuzi hivyo ni Ting iliyoanza mwaka 2009, Zuku ikaanzishwa mwaka 2011, Continental, Digitek na Azam Tv zote zilianza mwaka 2013.

Mpaka mwezi March, 2021, kwa mujibu wa mtandao wa Swahili Times kupitia akaunti yao rasmi ya Twitter wanasema kuwa, takwimu za TCRA zinaonesha kwamba Tanzania ina ving’amuzi 3,065,311 ambavyo viko hai. Mchanganuo ving’amuzi uko hivi:-
Na.
Aina ya Kisimbuzi
Idadi ya Watumiaji
1
Startimes​
1,958,721​
2
Azam Tv​
771,065​
3
DSTV​
209,033​
4
Continental​
66,250​
5
Zuku​
39,087​
6
Digitek​
17,382​
7
Ting​
3,773​
Jumla
3,065,311

Chanzo:https://twitter.com/search?q=idadi ya ving'amuzi nchini tanzania&src=typed_query

Ukiangali jedwali hilo; utagundua licha ya Azam Tv kuanza baada ya DSTV lakini kwa sasa imewazidi wateja zaidi ya laki tano. Vilevile licha ya Azam Tv kuanza kwa wakati mmoja na vingamuzi vingine ila imeviacha mbali sana kwa idadi ya watumiaji. Maswali unayoweza kujiuliza ni haya​
  • Kwanini imeizidi DSTV watumiaji?​
  • Kwanini imevizidi ving’amuzi vingine ambavyo imeanza navyo?​
  • Ving’amuzi vingine vimefeli wapi?​
Kwa uelewa wangu; Ninaziona sababu mbalimbali ambazo zinaifanya Azam TV kuwa na mafanikio na kuwa hapo ilipo. Sababu hizi ndizo zinapaswa kuwa somo tosha kwa wajasiliamali na wafanyabiashara wengine; baadhi ya sababu ni: -

Uwekezaji na kuongeza thamani bidhaa. Wakati waanzishaji wa visimbuzi wakiwekeza kwenye mitambo na kujaza chaneli za ndani na nje katika visimbuzi vyao; Azam Tv wao walifanya zaidi ya hivyo. Wao waliwekeza kwenye michezo, wakitambua asilimia kubwa ya watanzania wanapenda michezo. Hivyo walianza kununua haki za matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya Tanzania. Hii iliwapatia wateja kwa sababu mechi moja ya ligi kuu inafanyika kwenye mkoa mmoja na Tanzania ina mikoa 26; hivyo iliwalazimu watu waliopo mkoa mechi inapochezwa na mikoa mingine kununua ving’amuzi ili kushuhudia mechi hizo.

Funzo: Mjasiliamali au mfanyabiashara yeyote anayeanza biashara ni lazima bidhaa yake aiongeze thamani, asiifanye tu ikawa ya kawaida kama bidhaa zingine zilizoko sokoni.

Utambulisho wa kipekee. Leo hii ukiizungumzia Azam Tv taswira ya kwanza unayoipata ni mahali pekee ambapo panaonesha Ligi kuu ya Tanzania na michezo mikubwa ya masumbwi ya nchi hii. Ukimuuliza mtanzania yeyote upekee au utambulisho wa Digitek, Continental, Zuku na Ting ni nini? Hatokuwa na jibu kwa sababu maudhui mengi yanayopatikana huko yanapatikana pia katika ving’amuzi vingine. Wiki chache zilizopita, mitandaoni alikuwa ana-trend bondia aitwaye “Mandonga” ambaye mwisho wa siku watanzania waliishia kumtazama katika kisimbuzi cha Azam Tv kwenye pambano lake. Kwa maana nyingine ili kushuhudia mapambano ya ndondi mengi yanayofanyika hapa nchini lazima uwe na kisimbuzi cha Azam.

Funzo: Kwa mfanyabiashara au mjasiliamali anayetaka kuanzisha biashara lazima ahakikishe biashara yake ina utambulisho wa kipekee ili kuweza kujitofautisha na bidhaa zingine.

Kujifunza na kuiga mazuri kutoka kwa washindani. Azam Tv wakati inaanza ilikuwa ikirusha matangazo yake kupitia Visimbuzi ambavyo vinatumia madishi pekee. Startimes ambao wametawala soko na ndiyo wenye wateja mara mbili na nusu ya Azam Tv; wamekuwa wakitumia antena na Dishi. Mwaka 2018, Azam TV waliamua kuingia kwenye ving’amuzi vinavyotumia Antena kwa kuwa huwa havihitaji fundi wa kuviunganisha.

Tazama: VIDEO: Azam yafanya maboresho ving’amuzi vyake - YouTube

Funzo: Ukiwa mfanyabiashara au mjasiliamali unapaswa kujifunza na kuchukua mazuri kutoka kwa washindani wako na kuyaboresha ili kuendelea kushindana sokoni.

Bei Shindani. Licha ya Azam Tv kuwa na utambulisho wa kipekee na bidhaa zao kuongezwa thamani; lakini bado wana bei ambazo ziko chini ukilinganisha na baadhi ya washindani wao. Kwa mfano; Kifurushi cha chini cha mwezi cha Azam ni Tshs. 8,000/= ambacho kina chaneli zaidi ya 80 wakati Zuku kifurushi cha chini ni Tshs. 9,990/= kikiwa na chaneli 42. Hivyo, Azam Tv wana vifurushi vya bei ya chini na pia wana chaneli nyingi

Funzo: Ukiwa kwenye biashara unatakiwa uwe na bei nafuu huku ukiwa na ubora/ujazo zaidi ya bidhaa shindani.

Matangazo. Azam Tv licha ya kuwa na vituo vyao vya redio na luninga lakini wameendelea kujitangaza kwenye radio na Tv zingine. Kwa mfano; niliwahi kusikia Tangazo la Azam TV kwenye kituo cha East Africa Radio ambao ni kampuni dada na wamiliki wa king’amuzi cha Digitek. Vilevile ukiingia katika intaneti utapata matangazo na habari za kutosha za Azam Tv. Hii ni tofauti na baadhi ya washindani wao kama Digitek na Continental ambao ukitafuta kwenye Google huwezi kuzipata tovuti zao rasmi. Mshinda mwingine ni Ting ambaye ukimtafuta mtandaoni utaipata wavuti yake lakini maelezo yeyote ya bidhaa zake.

Funzo: Ukiwa mfanyabiashara au mjasiliamali; ni muhimu kuwekeza pia kwenye matangazo sehemu mbalimbali na mahali ulipopazoea.

Hitimisho
Ingawa inasemwa kuwa Azam Tv walitumia chaneli za ndani (Free To Air) ambazo hawakuwa na leseni ya kuzionesha kwa kulipia ili kujipatia wateja lakini kutokana na upekee wa maudhui na uongezaji thamani wa bidhaa yao, watanzania wangeendelea kuvinunua visimbuzi vyao. Kwa sasa Azam Tv ndiyo cha kisimbuzi chenye bei kubwa zaidi lakini bado wanaendelea kuongeza wateja kwa sababu nilizozitaja hapo. Kuna sababu nyingi ila hizi baadhi tu. Kwa mfanyabiashara au mjasiliamali anayetaka kuanza biashara ni muhimu kujifunza haya kutoka kwa Azam Tv.

_
Wakatabahu​
 
Ila king'amuzi cha Azam kinaenda kufeli kutokana na kutoa Contents zenye chembe za udiniudini na hizi kutolewa Kwa kitaalam. Fuatilia tamthiliya zitazowekwa channel two Sawa nne usiku siku za wiki . Tamthiliya hizi zote zitazowekwa hutukuza dini Fulani na kuonesha dini Fulani haifai.
 
Zuku tunajiunga hadi kwa buku 4
Kwq mwezi
 
Attachments

  • 5CA5273B-4916-4D66-A3ED-3F5BEADE7084.jpeg
    5CA5273B-4916-4D66-A3ED-3F5BEADE7084.jpeg
    29.8 KB · Views: 24
Ila king'amuzi cha Azam kinaenda kufeli kutokana na kutoa Contents zenye chembe za udiniudini na hizi kutolewa Kwa kitaalam. Fuatilia tamthiliya zitazowekwa channel two Sawa nne usiku siku za wiki . Tamthiliya hizi zote zitazowekwa hutukuza dini Fulani na kuonesha dini Fulani haifai.
Mtu huona kila anachokitafuta. We umeona hilo kwaku ndilo lililokichwani mwako.. Badirika mkuu huko tushatoka kitambo. Jifunze kuwa positive sio kila k2 we uone kasoro tu
 
Na
Malle Hanzi
_______

Mwanzoni mwa miaka ya kuanzia 2010 kuja 2020, Tanzania ilibadili mfumo wa urushaji wa matangazo ya vituo vya Luninga kutoka Analojia kwenda Dijitali.

Sababu kuu ya kuhama kutoka Analojia na kwenda mfumo wa Dijitali ni upungufu wa masafa (frequency) uliotokea kuanzia mwaka 2000. Katika mfumo wa Analojia, Chaneli moja ya TV ilikuwa inarushwa katika frequency moja, wakati katika mfumo wa dijitali, frequency moja ina uwezo wa kurusha chaneli 15-18 au 20-25, ikitegemeana na teknolojia gani mrusha matangazo anatumia (DVB-T au DVB-T2). Hivyo Umoja wa warusha matangazo duniani na wanachama wake waliweka azimio la kuhamia mfumo wa Dijitali.

Fursa.
Kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa, fursa ya biashara iliyokuwa inaonekana mbele yao ni uuzaji wa visimbuzi/ving’amuzi. Ingawa kulikuwa makampuni ya Cable Televesion; lakini kwa takwimu zisizo rasmi soko la visimbuzi lilikuwa limetawaliwa na kampuni ya Dstv na kufuatiwa na Startimes.

King’amuzi cha DSTV kilianza mwaka 1995 kikimilikiwa na kampuni ya Multichoice ya Afrika ya Kusini kikihudumu nchi 9 barani. Startimes ilianza mwaka 1988 nchini China na kinahudumu nchi 7 barani Africa.

Tulishuhudia makampuni kadhaa yakianzisha visimbuzi vyao ambavyo vilitaka kushindana Startimes pamoja na Dstv. Visimbuzi hivyo ni Ting iliyoanza mwaka 2009, Zuku ikaanzishwa mwaka 2011, Continental, Digitek na Azam Tv zote zilianza mwaka 2013.

Mpaka mwezi March, 2021, kwa mujibu wa mtandao wa Swahili Times kupitia akaunti yao rasmi ya Twitter wanasema kuwa, takwimu za TCRA zinaonesha kwamba Tanzania ina ving’amuzi 3,065,311 ambavyo viko hai. Mchanganuo ving’amuzi uko hivi:-
Na.
Aina ya Kisimbuzi
Idadi ya Watumiaji
1
Startimes​
1,958,721​
2
Azam Tv​
771,065​
3
DSTV​
209,033​
4
Continental​
66,250​
5
Zuku​
39,087​
6
Digitek​
17,382​
7
Ting​
3,773​
Jumla
3,065,311

Chanzo:https://twitter.com/search?q=idadi ya ving'amuzi nchini tanzania&src=typed_query

Ukiangali jedwali hilo; utagundua licha ya Azam Tv kuanza baada ya DSTV lakini kwa sasa imewazidi wateja zaidi ya laki tano. Vilevile licha ya Azam Tv kuanza kwa wakati mmoja na vingamuzi vingine ila imeviacha mbali sana kwa idadi ya watumiaji. Maswali unayoweza kujiuliza ni haya​
  • Kwanini imeizidi DSTV watumiaji?​
  • Kwanini imevizidi ving’amuzi vingine ambavyo imeanza navyo?​
  • Ving’amuzi vingine vimefeli wapi?​
Kwa uelewa wangu; Ninaziona sababu mbalimbali ambazo zinaifanya Azam TV kuwa na mafanikio na kuwa hapo ilipo. Sababu hizi ndizo zinapaswa kuwa somo tosha kwa wajasiliamali na wafanyabiashara wengine; baadhi ya sababu ni: -

Uwekezaji na kuongeza thamani bidhaa. Wakati waanzishaji wa visimbuzi wakiwekeza kwenye mitambo na kujaza chaneli za ndani na nje katika visimbuzi vyao; Azam Tv wao walifanya zaidi ya hivyo. Wao waliwekeza kwenye michezo, wakitambua asilimia kubwa ya watanzania wanapenda michezo. Hivyo walianza kununua haki za matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya Tanzania. Hii iliwapatia wateja kwa sababu mechi moja ya ligi kuu inafanyika kwenye mkoa mmoja na Tanzania ina mikoa 26; hivyo iliwalazimu watu waliopo mkoa mechi inapochezwa na mikoa mingine kununua ving’amuzi ili kushuhudia mechi hizo.

Funzo: Mjasiliamali au mfanyabiashara yeyote anayeanza biashara ni lazima bidhaa yake aiongeze thamani, asiifanye tu ikawa ya kawaida kama bidhaa zingine zilizoko sokoni.

Utambulisho wa kipekee. Leo hii ukiizungumzia Azam Tv taswira ya kwanza unayoipata ni mahali pekee ambapo panaonesha Ligi kuu ya Tanzania na michezo mikubwa ya masumbwi ya nchi hii. Ukimuuliza mtanzania yeyote upekee au utambulisho wa Digitek, Continental, Zuku na Ting ni nini? Hatokuwa na jibu kwa sababu maudhui mengi yanayopatikana huko yanapatikana pia katika ving’amuzi vingine. Wiki chache zilizopita, mitandaoni alikuwa ana-trend bondia aitwaye “Mandonga” ambaye mwisho wa siku watanzania waliishia kumtazama katika kisimbuzi cha Azam Tv kwenye pambano lake. Kwa maana nyingine ili kushuhudia mapambano ya ndondi mengi yanayofanyika hapa nchini lazima uwe na kisimbuzi cha Azam.

Funzo: Kwa mfanyabiashara au mjasiliamali anayetaka kuanzisha biashara lazima ahakikishe biashara yake ina utambulisho wa kipekee ili kuweza kujitofautisha na bidhaa zingine.

Kujifunza na kuiga mazuri kutoka kwa washindani. Azam Tv wakati inaanza ilikuwa ikirusha matangazo yake kupitia Visimbuzi ambavyo vinatumia madishi pekee. Startimes ambao wametawala soko na ndiyo wenye wateja mara mbili na nusu ya Azam Tv; wamekuwa wakitumia antena na Dishi. Mwaka 2018, Azam TV waliamua kuingia kwenye ving’amuzi vinavyotumia Antena kwa kuwa huwa havihitaji fundi wa kuviunganisha.

Tazama: VIDEO: Azam yafanya maboresho ving’amuzi vyake - YouTube

Funzo: Ukiwa mfanyabiashara au mjasiliamali unapaswa kujifunza na kuchukua mazuri kutoka kwa washindani wako na kuyaboresha ili kuendelea kushindana sokoni.

Bei Shindani. Licha ya Azam Tv kuwa na utambulisho wa kipekee na bidhaa zao kuongezwa thamani; lakini bado wana bei ambazo ziko chini ukilinganisha na baadhi ya washindani wao. Kwa mfano; Kifurushi cha chini cha mwezi cha Azam ni Tshs. 8,000/= ambacho kina chaneli zaidi ya 80 wakati Zuku kifurushi cha chini ni Tshs. 9,990/= kikiwa na chaneli 42. Hivyo, Azam Tv wana vifurushi vya bei ya chini na pia wana chaneli nyingi

Funzo: Ukiwa kwenye biashara unatakiwa uwe na bei nafuu huku ukiwa na ubora/ujazo zaidi ya bidhaa shindani.

Matangazo. Azam Tv licha ya kuwa na vituo vyao vya redio na luninga lakini wameendelea kujitangaza kwenye radio na Tv zingine. Kwa mfano; niliwahi kusikia Tangazo la Azam TV kwenye kituo cha East Africa Radio ambao ni kampuni dada na wamiliki wa king’amuzi cha Digitek. Vilevile ukiingia katika intaneti utapata matangazo na habari za kutosha za Azam Tv. Hii ni tofauti na baadhi ya washindani wao kama Digitek na Continental ambao ukitafuta kwenye Google huwezi kuzipata tovuti zao rasmi. Mshinda mwingine ni Ting ambaye ukimtafuta mtandaoni utaipata wavuti yake lakini maelezo yeyote ya bidhaa zake.

Funzo: Ukiwa mfanyabiashara au mjasiliamali; ni muhimu kuwekeza pia kwenye matangazo sehemu mbalimbali na mahali ulipopazoea.

Hitimisho
Ingawa inasemwa kuwa Azam Tv walitumia chaneli za ndani (Free To Air) ambazo hawakuwa na leseni ya kuzionesha kwa kulipia ili kujipatia wateja lakini kutokana na upekee wa maudhui na uongezaji thamani wa bidhaa yao, watanzania wangeendelea kuvinunua visimbuzi vyao. Kwa sasa Azam Tv ndiyo cha kisimbuzi chenye bei kubwa zaidi lakini bado wanaendelea kuongeza wateja kwa sababu nilizozitaja hapo. Kuna sababu nyingi ila hizi baadhi tu. Kwa mfanyabiashara au mjasiliamali anayetaka kuanza biashara ni muhimu kujifunza haya kutoka kwa Azam Tv.

_
Wakatabahu​
Mkuu. Umenyoosha Sana . Nimepata shule ambayo sikuwahi kuifaham hasa kwenye historia ya soko la VISIMBUZI TZ. Umeongea kwa details Sana mkuu. Nimeshawishika ku view profile lako kuona nyuzi zako za nyuma mzee... Uzi wa kufungia mwezi kabisa huu
 
Back
Top Bottom