Daima mtu anayefaidika na ushindani ni mteja na siyo ninyi wafanyabiashara

Blacklight

Member
Jun 5, 2023
7
8
Kwenye Dunia hii ya mabeberu watu wanaoongoza kutengeneza hela ni wafanyabiashara, wakifuatiwa na watu wenye vipaji, kisha watu wenye taaluma zenye demand kubwa na kuendelea.

Huenda this fact imewafanya watu wengi waamini biashara ni mlango wa nyuma wa benki, yaani njia ya kupata hela nyingi, wengine wakiamini ni njia nzuri ya kuepuka utumwa wa kuajiriwa, kupata muda zaidi wa kufanya mambo mengine.

Regardless ya sababu ipi inayokufanya kuingia katika biashara, wote tutakubaliana kwamba wafanyabiashara wengi hutumia muda mwingi kwenye biashara zao, huwa na stress na fatigue kuliko mtu aliyeajiriwa. Kubwa zaidi kwa mujibu wa utafiti uliofanyika USA wafanyabiashara wengi hupata kipato pungufu ya 35% ya mtu aliyeajiriwa.

Kubwa la kubwa zaidi, biashara nyingi hufa ndani ya kipindi kifupi na chache husurvive baada ya miaka mitano, pigia mstari husurvive na siyo hufanikiwa.

Ni kama vile najaribu nashawishi watu wasifanye biashara, nope but najaribu kuemploy realistic thinking.

Sasa nini huwa shida? Twende pamoja;

1. CONFIMATORY BIAS
Hii ni hali ya kuover-estimate nafasi yako ya kufanikiwa. Wengi tunapofungua duka tunavuta taswira na kuona biashara zetu zinaenda kuwa Azam ya kesho or maybe Google, inaanza kucreate a lot of money, millions of money.

It's good thing ku-think bigger and l encourage that lakini swali ambalo inabidi ujiulize, huo ndio uhalisia? Shida ya confirmatory bias ni kuwa too optimist na kusahau kufanya homework yako vizuri na kuuweka ukweli kando.

2. UCHAGUZI MBAYA WA WAZO LA BIASHARA
Kabla hujaamua kuyavulia nguo maji, fahamu kwenye kila kitu unachokifanya una options even if unahisi hauna. Epuka kuwa na wazo moja tu la biashara, kuwa na mawazo kadhaa mezani kisha tathimini wazo moja moja halafu uchague the best one. Hapo sasa utahitaji exposure na experience, not bad huwezi jua kila kitu but usimsahau mwalimu wako wa geography form 4, toka ukafanye research.

Daima tambua wazo lenye risk kubwa huwa na expected return kubwa. S hata wewe unaona betting (utani kidogo wakubwa) na zenye risk ndogo kama maduka ya Mangi huwa na expected return ndogo pia, kazi ni kwako kwenye kuchagua.

3. KUAMINI USHINDANI UNAFAIDA KWAKO
Daima mtu anayefaidika na ushindani ni mteja na siyo ninyi wafanyabiashara Competition inachofanya ni hiki; utaona jirani yako anauza bidhaa A kwa 200 wakati wewe unauza 250 so automatically utakuwa na mzunguko mdogo, competition itakulazimu ushushe bei Ili uongeze mzunguko, wakati huohuo umepunguza profit margin yako, sanasana utamchukia mpinzani wako na hapo ndio mwanzo wa kurogana.

Unaweza usinielewe sababu competition ni ideology tuliyokaririshwa tangu utotoni lakini ukweli ni kwamba makampuni mengi makubwa yaliyofanikiwa yanajaribu kupunguza ushindani kwa kununua patent right na vizuizi vingiii vya kuingia kwenye soko lao. Si unaona Microsoft, Coca-Cola na Pepsi, Google, Azam TV na Ligi Kuu yetu halafu we unaamini kwenye ushindani 😅!

Kama unahitaji competition ili utoe high standards services utakuwa hauna tofauti na mashirika ya umma. Fanya ujenge Soko lako mwenyewe ambalo hakuna mpinzani atakugusa hata afanye nini.

4. KUJIFANYA UNAJUA SANA KULIKO WATEJA
Wafanyabiashara wengi wanaangalia biashara zao kutokea ndani kwenda nje badala ya nje kuja ndani. Wanaamini bidhaa zao na huduma zao ni bomba kiasi wanapuuzia mitazamo ya wateja na kujaribu kuwashawishi wateja waone kama unavyodhani wewe.

Ukichunguza business plan nyingi za biashara nyingi zilizofanikiwa zilivyosasa na namna zilivyokuwa kipindi zinaanza ni tofauti, be flexible.

Haijalishi una business idea nzuri kiasi gani au bidhaa nzuri kiasi gani, hiyo idea au bidhaa kiuhalisia siyo nzuri mpaka wateja waseme hivyo.

5. KUSHINDWA KUWATAMBUA, KUWAFIKIA NA KUWATUNZA WATEJA MUHIMU
Kwenye kila biashara kuna potential customers ambao hao kila mfanyabiashara akiwaona anajua leo mauzo yatakuwa juu na wasipokuja mauzo yanakuwa chini, kama hujajua hilo chunguza utagundua.

Infact kabla hujaanzisha biashara inabidi ujiulize ninalenga soko gani haswa na ujue namna ya kulifikia. Ukishawajua potential customers wako usikubali kuwapoteza, utajuta maana kuwarudisha ni kazi. Daima kumbuka kanuni ya robo huchangia robo tatu, yaani robo tatu ya mauzo yako huchangiwa na robo tu ya wateja wako ambao hao ndio tunawaita potential customers

Sababu zipo nyingi sana zaidi ya 20 na by the grace of God nitazidi kuwaeleza ndugu zangu siku baada ya siku, tuombeane uzima, Mungu awabariki.
 
Kwenye biashara kuna kitu kinaitwa " "price fixing". Hii ni criminal offence kwenye nchi za wenzetu lakini huku watu wanaifanya. Yaani wale big importers wa aina fulani ya bidhaa wanakaa chini na kukubaliana kuiuza kwa bei fulani.
 
Uzi konki sana na umejaa madini advanced knowledge of business management.
Japo uzi umekosa wachangiaji nadhani ni kwa sababu ya watu kutoelewa concept iliyozungumzwa imewaacha gizani au ni ile kasumba tu ya watu kupenda kuchangia nyuzi za vichekesho,kusifia makalio na kula tunda kimasihara.
 
We fugaaaa gurueeee pelekaaa Gazaaa over.......
Utanishukuru badayeeeee
 
Uzi mzuri Sana
Tena umenikuta nipo napambana hapa kuokoa kibiashara changu

Tatizo moja kubwa sana ambalo naona startups nyingi tunalo ni kukosa skills za biashara
Wengi tunaingia kwenye biashara hatujui A Wala B tunaingia tu Sasa tukiona tunazama wachache hutafuta skills na wengi biashara hufa
Biashara sio ya Kila mtu
 
Biashara niyakila mtu sema, **** mambo 2 inabidi uyajue au uyafanyie tafiti

1. Experience
2. Idea

Ukiwa na mtaji invest kwenye experience ya biashara uliyonayo na sii idea ya biashara uliyonayo. Sijui kama unanielewa
 
Uzi poa, though sijajua hii ya waajiriwa huwazidi wafanyabiashara kipato pingufu ya 35% source ni ipi na waliofanya utafiti walikuwa serious kweli 😁
 
Utafiti umefanyika USA...kwahiyo inawahusu wamarekani...huku ni tofauti
Hapo sawa, lakini duuuuh mbona marekani have got a lot of businessmen and they are very successful how come waajiriwa wawazidi kipato, anyway research can reveal what we can't see with our naked eyes!!!
 
Kwa huko kwao inawezekana mkuu, maana haki za wafanyakazi zinazingatiwa.

Huku kwetu mtu kaajiliwa na mshahara wake ni buku 3, kuna kutoboa hapo.
 
Biashara, unazalisha kitu bomba unahisi wateja watakufuata weeeeeeh!

Unaanza tena kuwasalandia kuwatafuta duuuh! Bado nnatafuta sumaku ya wateja wanitafute. Sijui ntaipataga!??
 
Back
Top Bottom