Azam TV Max app na matatizo ya channeli ya UTV siku za mechi za simba CAF

Kioski

Member
Nov 24, 2017
91
101
Wakuu mimi ni mtumiaji mzuri wa azam tv max app kwenye simu yangu, kuna hii ya UTV chaneli kila ukifika muda wa mechi za simba unakuta imeondolewa HAIPO KABISA au ukiikuta na ukaifungua kwa ajili ya kungalia zako mpira unaambiwa CHANNEL IS NOT AVAILABLE IN YOUR AREA.

Ajabu ni kwamba baada ya mechi kuisha UTV unaikuta ipo imerudishwa na hata ukiifungua haileti matatizo yeyote.

Hili tatizo limekuwa sugu, sijui shida ni nini.
 
Nadhani ni copyrights, Azam wana ruhusa ya kurusha matangazo kupitia televisioni lakini sio digital media ukizingatia huvuka mipaka ya nchi walizoruhusiwa kwa kuweza kutazamwa popote.
 
Kweli,Azam hawaruhusiwi kurusha hizi game kupitia Azam max kutokana na copyright, download startimes app hizo game za caf zinaoneshwa tv 3,ila ni ya kulipia
 
Nadhani ni copyrights, Azam wana ruhusa ya kurusha matangazo kupitia televisioni lakini sio digital media ukizingatia huvuka mipaka ya nchi walizoruhusiwa kwa kuweza kutazamwa popote.
Changamoto iliyopo hawaweki wazi,.watu wanalalamika wenyewe wapo kimya kama hawaoni vile. Inakera sana.
 
Hapana mkuu mimi game ya juzi ya Simba vs RS Berkane nimeiangalia Live kupitia Azam max Utv

Sasa sijajua kama kuna vigezo vingine vya ziada
 
Wakuu mimi ni mtumiaji mzuri wa azam tv max app kwenye simu yangu, kuna hii ya UTV chaneli kila ukifika muda wa mechi za simba unakuta imeondolewa HAIPO KABISA au ukiikuta na ukaifungua kwa ajili ya kungalia zako mpira unaambiwa CHANNEL IS NOT AVAILABLE IN YOUR AREA.

Ajabu ni kwamba baada ya mechi kuisha UTV unaikuta ipo imerudishwa na hata ukiifungua haileti matatizo yeyote.

Hili tatizo limekuwa sugu, sijui shida ni nini.
Azam app inakula mb kiasi gani kwa mechi moja?
 
Back
Top Bottom