Azam Media wakataa shutuma dhidi ya rushwa ya kurusha vipindi vya tamthilia kutoka kwa wazalishaji binafsi

mangiTz

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,548
2,618
Habari wana jamvi, kumekuwa na taarifa za chini kwa chini baada ya kuibuka sakata la wasimamizi wa televisheni kule Dstv sasa imehamia Azam nao wamejibu mapigo.

Note; ukimshtumu mtu au kampuni hakikisha hiyo kesi una ushahidi nayo la sivyo inakugeukia, kesi kama hizi ikikugeukia utalipwa faini moja mbaya ambayo itakugharimu.

Pia soma:

FB_IMG_1701418480695.jpg

Video iliyosambaa mitandao ya kijamii Deogratius Shija akimtuhumu Wasiwasi Mwabulambo kwa kupokea rushwa

Snapinsta.app_406483569_18400860217006868_5539114931511091120_n_1080.jpg
TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigizaji na mtengeneza filamu, Deogratius Shija, akiwatuhunu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yetu kwa vitendo vya rushwa.

Kampuni yetu inamuarifu Shija na umma kwa ujumla kuwa, haivumilii vitendo vya rushwa, udanganyifu na mbinu zozote chafu katika kusaili maudhui kwa ajili ya kuonyeshwa katika chaneli zetu, kadhalika hatupendezwi na tabia ya watengeneza maudhui kutunga shutuma dhidi ya watendaji wetu kwa sababu tu kazi zao hazikupitia kwenye chujio la kupima ubora.

Kwasababu hizo, tunatoa muda wa wiki mbili kwa Deogratias Shija, kuwasilisha ushahidi au vielelezo kuhusu tuhuma alizozitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji au kwenye mamlaka za kisheria, TAKUKURU, Film Board, au Jeshi la Polisi, ili kuwezesha hatua stahiki zichukuliwe kwa watuhumiwa wote wanaodaiwa kuihujumu kampuni kwa vitendo vyote kinyume na taratibu za kazi.

Kampuni yetu ina utaratibu maalum wa ndani, ulio wazi na shirikishi katika manunuzi ya filamu na maudhui mengine kutoka kwa wazalishaji binafsi.

Azam Media Ltd inatumia fursa hii kuwaomba wadau wa filamu nchini kufuata njia sahihi zinazokubalika kisheria ikiwemo kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Filamu, Polisi au TAKUKURU pale wanapokuwa na ushahidi wa madai yao badala ya kutumia njia ambazo zinaweza kuleta taharuki na taswira mbaya kwa jamii ndani na nje ya Tanzania.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma

1.12.2023.
 
Habari wana jamvi , kumekuwa na taarifa za chini kwa chini baada ya kuibuka sakata la wasimamizi wa televisheni kule Dstv sasa imehamia Azam nao wamejibu mapigo

Note; ukimshtumu mtu au kampuni hakikisha hiyo kesi una ushahidi nayo la sivyo inakugeukia, kesi kama hizi ikikugeukia utalipwa faini moja mbaya ambayo itakugharimu.

Pia soma

Video iliyosambaa mitandao ya kijamii Deogratius Shija akimtuhumu Wasiwasi Mwabulambo kwa kupokea rushwa

yeye pia anakesi, alishiriki kutoa rushwa. kinacho muuma ni kazi yake bado ikawa rejected
 
Note; ukimshtumu mtu au kampuni hakikisha hiyo kesi una ushahidi nayo la sivyo inakugeukia, kesi kama hizi ikikugeukia utalipwa faini moja mbaya ambayo itakugharimu.
Barua gani haina saini haina muhuri hata wa kielectronic tutaamini vipi km ni kweli barua ya Azam sio kwamba kuna mjuba kakaa tu kaiandaa huko uchochoroni yaan Idara haina hata Mkuu wa Idara husika ambae anaiwakilisha Idara husika akatia saini akagonga muhuri au Mimi ndio nipo nyuma ya muda?
 
Upo nyuma ya muda, nenda kwenye official account ya Azzam Facebook utaikuta.
 
Back
Top Bottom