AU's dilemna and the Libyan crisis

AU's dilemna and the Libyan crisis

Wanafiki wakubwa hao. Walikuwa wapi siku zote? Bora wamezuiwa. Wakatatue mataizo yao ya kawaida kwanza kama njaa,ukimwi,tb,ujinga n.k

some people they sound strong and confident behind keyboard. tehetehe JF raha
 
Hivi wanaposema wanaenda ku-mediate huwa wanenda kufanya nini haswa? Maana wameenda Ivory Coast - tunajua walichovuna. Sasa ni mbinu hizo hizo wangezitumia kwa Quadaffi? Wangemshawishi ateuwe jamaa wa Benghazi kuwa mawaziri? AU is a bunch of incompetent 'leaders'! They better stay out.
 
Twende mbele turudi nyuma. Hivi Gadaffi alikuwa akiwashambulia waandamanaji au waasi? Libya kuna waasi walijitenga huko Benghazi na si waandamanaji. Waandamanaji gani wanakuwa na silaha na ndege za kivita? Juzi walenga shabaha wa Yemen wamewalenga waandamanaji na kuua makumi hatujasikia UN ikitoa Azimio!! Azimio la hao UN ni no fly zone lakini Marekani na mabeberu wenzake wanashambulia makazi ya Gadaffi na raia wasio na hatia, huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu!! Huko Somalia raia wasio na hatia wanauawa kila kukicha lakini Mabeberu wanaangalia tu kwa kuwa hakuna maslahi. Marekani na mabeberu wenzake wanataka ku justify ili waishambulie Iran si vinginevyo. Afrika tusipokuwa makini tutatawaliwa na hao wajua haki za binadamu ambazo nazo zinachagua, Libya na siyo yemen!!
Ni kweli. Lakini kila nchi ya watu wenye akili timamu inaangalia maslahi yake kwanza! Hebu tu tujiulize, kwa nini Arab League ilikomalia suala la no fly zone Libya na si Yemen?!
 
Kitendo cha Kanali Gadafi kuwashambulia raia wake kwa mizinga na ndege za kijeshi ni kitendo cha aibu na kinatakiwa kipingwe na wapenda demokrasia wote.

Baada ya kuona wenzake wa Tunisia na Misiri wakiondolewa madarakani kwa nguvu za wananchi Gadafi aliamua kutumia nguvu zote za kijeshi alizonazo kuwalazimisha wananchi wake wasipate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Kitendo hiki kingeruhusiwa kuendelea kingejenga precedence ya watawala wa kiafrika kutumia nguvu ya majeshi kuendelea kukaa madarakani, tumeshuhudia jinsi chaguzi nyingi Afrika zinavyovurugwa na majeshi kwa lengo la kuwalinda wanasiasa waliowapatia nafasi na wanaowarushia marupurupu yatokanayo na ukwapuaji wa rasilimali za nchi zao.

Kwa kuzuia mashambuliza ya anga na matumizi mengine ya ziada dhidi ya raia wa Libya napenda kuwapongeza viongozi wa USA, UK, Ufaransa na wengine wote wanaounga mkono nguvu za kijeshi kumzuia Gadafi kuwashambulia raia wake. Hii itasaidia sana ukuaji wa demokrasia Afrika kwani viongozi wengine ambao hawapendi kuona wakipingwa na wananchi wao kuogopa kushambuliwa pindi watakapotumia nguvu za kijeshi kuzuia wananchi hawa kutumia haki yao ya kidemokrasia kuwapinga (kuandamana).

Hapo kwenye red. Walibya hawana katiba.
 
baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Gaddafi amesema atafungua maghala kuwapa silaha wananchi kuilinda nchi yao. hivi hii ni kweli? wasiwasi wangu ni kuwa asije akawa anawapa silaha walewale ambao aliwashambulia na kuwaua ndugu zao wakati wa maandamano, nadhani mwisho wake utakuwa mbaya sana!
 
Good move,ukilingansha maisha ya tz na libya utashangaa kwwa nini wanaandamana huku wana kila kitu.Lakini watz tunatanguliza amani kuliko maisha bora. Ipo siku nasi tutasisimuka na kuijenga tanzania mpya.

Una maana gani wanaandamana huku wana kila kitu? Japokuwa wabongo maskini tuna kila kitu. Uzembe wetu ndio unatufanya kuwa maskini. Walibya hawana kila kila kitu. Kwa mfano hawana freedom unayoitumia hapa JF kuandika unachoandika. Thats want they want. Kwako itaonekana kitu kidogo sana kulinganisha na utajiri. Lakini utakuja tambua when you loose your freedom and liberty. The way unavyoshangaa kwa nini wanaandamana huku wana kila kitu, ndivyo pia watu wanavyotushanga kwa nini tuko maskini wakati tuna kila kitu.
 
Sikutegemea kukuta waafrika wanaendelea kushangilia kinachotokea libya sasa hv bali walipswa kusikitika na kuonamisha vichwa chini wakilia, mnampongeza obamana sirkozy shame on you! Hamuoni ni jinsi gani wao kwa mashambulio ya siku moja tu wameua raia 64 na majeruhi zaid 100 sasa anaeua raia ni nani gaddafi au wamarekani? Af unadiriki kusema wazi kuwa raia hawamtaki gaddafi ni asilimia ngapi ya raia wote wasiomtaka gaddafi au ni kikundi cha watu wachache wenye uchu na madaraka wanaosapotiwa na wamagharibi ndo hawamtaki gaddafi, eti wanalinda raia, mbona palestina kila kukicha israeli anawauwa watu haendi huko kwalinda, miaka mingapi leo somalia watu wanakufa mbona haendi huko, mbona kongo watu wanakufa haendi huko, vp kuhusu bahrain ambako serikali inawaua waandamanaji na sio waasi na wala hausikii wakisemwa hata kwa maneno nini kupigwa na majeshi, acheni kuwa na fikra finyu huku mkijisifia kuwa wananchama wa jf kisima cha fikra pevu, MKIENDELEA kuwa na mawazo mgando kama hayo hamna haja hata ya kuwepo humu jf ni bora mkaangalie utaratibu mwingine lakini katika hili la libya western countries wana ajenda ya siri kubwa tu nyuma yao ambayo kwa kifupi ni strategic reason.
Pole mkuu naona 'umeinamisha kichwa na unalia kwa aibu'... Hivi hujui kama Congo kuna askari wa UN huko?! Somalia na Bahrain wameachiwa watu wa 'mashariki' wamalize mgogoro huo...au na wao hawawezi?!
 
endeleni kuwa worship hao mashetani wa magharibi bado wanatunyatia na sisi tutakuja kumia siku zina hesbau I HATE WESTERN .YAANI KWELI WA LIBYA WANAHITAJI MSAADA KIASI HICHO MHHHHHHHHHH UONGO MKUBWA NI MAFUTA YANAWAPELEKA IPO SIKU YAO .IMSIJIFANYE MNATATETEA DEMOCRACY ILA UKWELI UTABAKI KWA SASA WAZUNGU WAMEANDA KUPORA NA SI KUOKOA WALIBYA.
Kwa hiyo unashauri tuwa worship mashetani wa mashariki au???
 
TATIZO LA WAAFRIKA NI KUKOSA AKILI!
WAAFRIKA HAWANA MUDA WA KUJIULIZA KWANINI!? WAAFRIKA HAWAHITAJI KUJUA SABABU BALI KUAMBIWA TU...
MASKINI AFRIKA, MASKINI TANZANIA!!!

Wengi wetu hakuna anaejiuliza pindi tukiwafukuza WAZUNGU ama kudai MRAHABA UNAOSTAHILI NINI KITATOKEA!

WASWAHILI WANASEMA KILA MSHEREHEKEA MSIBA WA MAMA WA KAMBO, MSIBA HUMFIKA *****.
TAFAKARINI KWANZA NDIPO MUANDIKE UPUPU!
 
Twende mbele turudi nyuma. Hivi Gadaffi alikuwa akiwashambulia waandamanaji au waasi? Libya kuna waasi walijitenga huko Benghazi na si waandamanaji. Waandamanaji gani wanakuwa na silaha na ndege za kivita? Juzi walenga shabaha wa Yemen wamewalenga waandamanaji na kuua makumi hatujasikia UN ikitoa Azimio!! Azimio la hao UN ni no fly zone lakini Marekani na mabeberu wenzake wanashambulia makazi ya Gadaffi na raia wasio na hatia, huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu!! Huko Somalia raia wasio na hatia wanauawa kila kukicha lakini Mabeberu wanaangalia tu kwa kuwa hakuna maslahi. Marekani na mabeberu wenzake wanataka ku justify ili waishambulie Iran si vinginevyo. Afrika tusipokuwa makini tutatawaliwa na hao wajua haki za binadamu ambazo nazo zinachagua, Libya na siyo yemen!!

Iko hivi, mwanzoni raia walihamasika na yaliyotokea Tunisia na Misri na wao wakaanzisha movement ya kumuondoa Gadafi kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiarabu hivi sasa Yemen, Bahrain, Saudi, n.k. Gadafi akaanza kutumia polisi kuwazuia waandamanaji kwa njia ya amani kama ilivyokuwa Misri jitihada ambayo ilishindwa kama ilivyoshindwa Misri. Gadafi akaenda mbali zaidi kwa kuanza kuwashambulia waandamanaji wa amani kwa risasi za moto badala ya mabomu ya machozi na risasi za mpira. Akaua waandamanaji kadhaa lakini bado akaendelea kuelemewa na dalili za wazi za kutokea ya Mubarak ikajidhirisha. Akaongeza kasi ya kutumia risasi za moto na akaenda mbali zaidi kwa kuwashambulia kwa mabomu mazito ardhini na kutoka angani kitu ambacho kiliwaudhi baadhi ya wanajeshi ambao walimuasi Gadafi na kuamua kuungana na waandamanaji na ndio wakaitwa waasi. Hata yemen sasa hivi kuna majeshi yameigeuka serikali kuu. Nadhani kwa historia hiyo fupi sidhani kama utawaona waasi kivipi lakini ujue kuwa ni watu wasiokubaliana na uamuzi wa Gadafi wa kuwashambulia raia kwa risasi na mabomu mazito
 
Viongozi wa Afrika bwana akili fupi sanaaaaaaaaaaaaaa! Wameng'ang'ania kujilinda dhidi ya raia wao wenyewe. Quadaffi katengeza jeshi la kujilinda yeye na familia yake dhidi ya watu wa Libya. Sasa njemba zinapiga za masafa marefu anaishia kulialia tu-hamna kitu. Halafu watu wanathubutu kusema Quadaffi kaifanyia Libya mambo mengi. Yepi hayo ikiwa hata kujilinda dhidi ya mashambulizi madogo tu hawezi.
 
Namshukuru Mungu kwaajili ya ufaransa, uingereza na marekani kwaajili ya kufanya huduma hii kubwa ya kitumishi, kumsambaratisha mtumishi wa mpinga kristo aliyekuwa anajiita mfalme wa wafalme...hana maana yoyote, na watamponda kama panya...go to hell gadafi/gaidi...pesa zake za kishetani ndo alizowajengea waislam wa Uganda/kampala na dodoma misikiti aliyoiita kwa jina lake..ni jini yule hana lolote, muuaji mkubwa, toka lini mtu anayejifanya kujenga mahekalu ya mungu anatumia mabomu ya ndege kushambulia raia wanaoandamana? wapi na wapi, do you think the world would every remain silent to witness another genocide just like they did in Rwanda? never ever, no more holocost, no more genocide....mtu yeyote yule hata kikwete akiwa anaua watu hovyohovyo, nchi zingine kwa sasa zitaingilia tu hata kama kuna watu ambao watalalamika namna gani..watakuja kuelewa badaaye,.....kwenda zako huko gadafi....
 
bravo sakozy, obama and cameron..bravoo bravoo....hongereni kwakweli kutuondolea dictator tena mchawi na shetani...cha ajabu zaidi, utakuta kuna watz ambao wanamsaidia gadafi, kama vile wanavyomsaidia na kumwombea osma bin laden tu...kwasababu wao ni magaidi,wauaji na waliojaa ukatili kama gadafi na osama...bravo mataifa ya magaribi...
 
JK kupeleka majeshi Comoro ilikuwa ni uvamizi?
huko hao wanajeshi walienda kunywa maji ya madafu au kiherehere cha kuingila mambo ya ndani ya nchi ingineeeeeeee.

KAMA Tz tuliingilia mambo ya nchi ingine basi hata America haijafanya cha ajabu
 
bravo sakozy, obama and cameron..bravoo bravoo....hongereni kwakweli kutuondolea dictator tena mchawi na shetani...cha ajabu zaidi, utakuta kuna watz ambao wanamsaidia gadafi, kama vile wanavyomsaidia na kumwombea osma bin laden tu...kwasababu wao ni magaidi,wauaji na waliojaa ukatili kama gadafi na osama...bravo mataifa ya magaribi...

Mi nadhani mkuu,umezungumza kiushabiki zaidi na chuki tu,jaribu kufikiri japo kidogo faida watakayoipata hao walibya ambao vita inapiganwa nchini mwao baada ya ghadhaf kushindwa...ni kweli kabisa kutoka moyoni unaona hizo siasa za nchi za nje za nchi za kimagharibi zinamanufaa yoyote katika nchi wazazodai wanasaidia kama si kulinda maslahi yao binafsi?Hili amesema Obama,Marekani ipo tayari kufanya lolote kulinda maslahi ya watu wake nchini Libya.....je hilo ndilo unaloshangilia kiongozi?
 
Aaah, Tanzania iliingilia kuzima uasi lakini Sarkozy na mabeberu wenzake wanaingilia kusaidia uasi!! Vitu viwili tofauti kaka. Japokuwa sikuunga mkono Tanzania kuingilia mambo ya ndani ya Comoro lkn kuna utofauti huo ambao inabidi uufahamu. Libya kuna uasi kama wa anjuan kwa hiyo nilitegemea Sarkozy na mibeberu mingine iingilie kuuzima lakini heee, wanataka kumuondoa Gadaffi!!
Mohammed Bacar aliingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 2001 kama huyo Gaddafi tu.. 2007 kwenye uchaguzi ambao haukutambuliwa na AU akajitangaza kuwa mshindi wa urais.

Hili swala tumelidiscuss hapa
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/11018-majeshi-yetu-comoro-who-is-responsible.html
 
Harakati za jamii ya kimataifa zinazoendela dhidi ya Libya zimekosolewa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Katika tahariri yake kuhusu mgogoro wa Libya, iliochapishwa kwenye magazeti nchini humo Rais Museveni amemkosoa na pia kumtetea Kanali Muamar Gaddafi.


Kiongozi huyo amepinga upinzani ambao unaungwa mkono na mataifa ya kigeni na ameyaita mataifa hayo kama yenye undumila kuwili unaothibitishwa na kuweka haraka marufuku ya ndege kupaa kwenye anga ya Libya.


Museveni ambaye ni mmoja walioteuliwa kwenye jopo la kutatua mzozo huo na Umoja wa Afrika amehoji kwa nini nchi hizo zina puuza hali mbaya kama vile ya Bahrain ama maeneo mengine yenye kuegemea upande wa magharibi.


Katika tahariri hiyo, anauliza ikiwa Benghazi pekee ndio kuna raia na Mogadishu hakuna au ni kwa sababu nchini Somalia ambapo wameomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati mzozo unaoendelea hakuna mafuta.


Aidha, Rais Museveni amemsifu Kanali Gadafi kama mmoja wa viongozi wa Kiarabu ambae hashabikii uislamu wa itikadi kali.


Kiongozi huyo pia amemsifu Gaddafi kama kiongozi wa Afrika ambaye ana mawazo yake binafsi asie shawishika na sera za kigeni.


Kwenye tahariri hiyo pia, Rais Museveni amekosoa sera za Gaddafi, na kutoa mifano kama alivyounga mkono utawala wa Iddi Amin alieongoza Uganda tangu mwaka wa 1971 hadi 1979.


Museveni ameongeza kuwa Gadaafi alikosa kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika, kwa mfano kwa kuwahusisha viongozi wa kijadi ama kitamaduni, kama vile wafalame na watemi katika masuala ya kisiasa.


Tahriri yake imekamilika kwa kuutaka umoja wa Mataifa kudurusu azimio lake la marufuku ya ndege kupaa kwenye anga ya Libya.


http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2011/03/110322_uganda_libya.shtml
 
Museveni mwenyewe anajua fika kuwa dunia inaendeshwa mithli ya samaki baharini; "samaki nkubwa anamla mdogo." Mambo ndivyo yalivyo hata nchini mwake.
 

Monday, 21 March 2011 22:45
By Mkinga Mkinga,
The Citizen Reporter


While there has been worldwide condemnation of the Western powers' invasion of Libya invasion, the leader of the embattled North African nation Col. Muammar Gaddafi has written to President Jakaya Kikwete and other African leaders, according to the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Bernard Membe.

"I have the envelope here though I am also not aware what its contents are… I am taking it to the President right away," said Mr Membe when contacted by The Citizen yesterday.


Apparently not in position to reveal more information, the minister said Tanzanian officials had been in constant contact with the Libyan government and the African Union Commission over the current situation in Libya."I have been meeting with the Libyan envoy in the country and, of course, I have received a letter from President Muammar Gaddafi addressed to President Jakaya Kikwete," said Mr Membe.


A mix of Western coalition aircraft and navies led by the United States launched air strikes on Libya on Saturday to enforce UN Security Council Resolution 1973 on protection of civilians from violence by forces supporting the Libyan leader.


Members of the coalition included the Britain, France, Canada, Italy and Belgium.Mr Membe said the AU Peace and Security Council is due to meet Friday this week to discuss the Libyan conflict, but he did not say the council would convene at what level.


He said Uganda is expected to table a motion calling for an emergency AU summit to further discuss the developments in Libya.Representatives of the UN Security Council would be invited to the meeting, he said, "because the no-fly zone resolution, which has prompted intervention by the Western powers was passed by the UN."


"Our concern is that many African countries were not properly represented during the meeting which passed the resolution," the minister pointed out.Meanwhile, Ugandan President Yoweri Museveni has condemned the attacks on Libya saying they were rushed.


"The Western countries, which are most active in these rush actions, should look at that route. It may be one way of extricating all of us from possible nasty complications. What if the Libyans loyal to Gaddafi decide to fight on?


"Using tanks and planes that are easily targeted by Mr Sarkozy's planes is not the only way of fighting. Who will be responsible for such a protracted war? It is high time we did more careful thinking," President Museveni said in a statement whose copy was made available to The Citizen.


President Museveni said the African members of the Security Council voted for this Resolution of the Security Council, noting that it was contrary to what the AU Peace and Security Council had decided in Addis Ababa recently.


"Regarding the Libyan opposition, I would feel embarrassed to be backed by Western war planes because quislings of foreign interests have never helped Africa," he added. Meanwhile, a renowned political scientist and lecturer at Saint Augustine University of Tanzania (SAUT), Prof Mwesiga Baregu has described the UN resolution as "very strange".


"Instead of seeking peace, it has gone for invasion which now is costing innocent Libyans lives," the academic added.

In the opinion of Prof Issa Shivji, an expert on Pan-African Studies, it was unbecoming for foreigners to intervene as the Libyan uprising was by the people of Libya against their autocratic system headed by Gaddafi.

"They do not want to replace Gaddafi with an American or European stooge," he said, noting that as usual, "imperialist powers headed by the US want to fish in troubled waters and under the guise of protecting the citizens of Libya, they have now decided to invade Libya."


"All history has shown that these powers have their own interests. In the case of Libya, oil is paramount. They will bombard the country, turn it into another war zone, militarise the Mediterranean and hijack people's revolution," he said.


Prof Shivji added: "We ought to learn from what they have recently done in Afghanistan, Iraq, Haiti and in the Balkans and what they are doing in Pakistan. It is surprising that the African Union is so silent on the invasion of the continent."


Speaking to this paper yesterday, Mr Faraja Kristomus, an assistant lecturer in the Department of Foreign Languages and Linguistics at the University of Dar es Salaam, said he was also against the attacks of the allied forces against Mr Gaddafi.
Not sure if has been posted.
 
Back
Top Bottom