Sikutegemea kukuta waafrika wanaendelea kushangilia kinachotokea Libya sasa hivi bali walipaswa kusikitika na kuinamisha vichwa chini wakilia, mnampongeza Obama na sirkozy shame on you! Hamuoni ni jinsi gani wao kwa mashambulio ya siku moja tu wameua raia 64 na majeruhi zaid 100 sasa anaeua raia ni nani Gaddafi au wamarekani?
Af unadiriki kusema wazi kuwa raia hawamtaki Gaddafi ni asilimia ngapi ya raia wote wasiomtaka Gaddafi au ni kikundi cha watu wachache wenye uchu na madaraka wanaosapotiwa na wamagharibi ndo hawamtaki gaddafi, eti wanalinda raia, mbona Palestina kila kukicha Israeli anawauwa watu haendi huko kwalinda, miaka mingapi leo somalia watu wanakufa mbona haendi huko, mbona kongo watu wanakufa haendi huko, vp kuhusu bahrain ambako serikali inawaua waandamanaji na sio waasi na wala hausikii wakisemwa hata kwa maneno nini kupigwa na majeshi, acheni kuwa na fikra finyu huku mkijisifia kuwa wananchama wa jf kisima cha fikra pevu, MKIENDELEA kuwa na mawazo mgando kama hayo hamna haja hata ya kuwepo humu JF ni bora mkaangalie utaratibu mwingine lakini katika hili la libya western countries wana ajenda ya siri kubwa tu nyuma yao ambayo kwa kifupi ni strategic reason.