Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Kama unaamini yuko kwa sababu tu unaweza ukaenda ukamkuta ila huna uhakika wa uwepo wake sidhani kama atakupenda kama yupo ikizingatiwa inasemwa anajua yote hata yale ambayo binadamu wanawaza sirini.
Nani amekuambia sina uhakika wa uwepo wake?
 
Sheria ya mantiki inasema everything that begins to exist has a cause, ulimwengu una mwanzo hivyo unahitaji chanzo. Mungu hana mwanzo, Yeye ni eternal, hivyo hahitaji chanzo.
Ni wakati gani ulimwengu haukuwepo?

Ulimwengu umekuwepo milele.

Ulimwengu haujawahi kutokuwepo.

The universe didn't begin to exist.

Ulimwengu umekuwepo, upo na utaendelea kuwepo.

Hauhitaji chanzo.

Huyo Mungu hayupo. Na wala huwezi kuthibitisha kwamba yupo.

Huyo Mungu ni imani zenu uchwara za maandiko yenu ya kiimani. Mliyo andikiwa na wajinga wa kale. Sasa mnaamini mkichwamkichwa tu!
 
Karibu upewe elimu.
Kabla ya space, time and matter.
Kwanza kabla hatujaenda mbali umekubali huyo Mungu hayupo?
Karibu upewe elimu wewe ambaye bado hujui hata maana ya neno kabla.

Kabla ni neno linaloelezea muda, kama time haikuwepo, hakuna kitu kinachoitwa kabla kwa maana ya kibinadamu. Mungu haitwi yupo kabla ya muda, bali yuko nje ya muda.

Rudi shule ukajifunze basic physics na philosophy kabla ya kuja kunipa elimu mimi.
 
Sijui.

Ila nakuona unakoelekea unavyotaka kutanguliza mkokoteni mbele badala ya Punda.
Angalau umeanza kuwa mnyenyekevu, keep it up.

Kwenye sayansi na falsafa, usipojua kitu huwezi kukataa jibu pekee lililopo lenye mantiki hadi upate jibu mbadala. Ukisema sheria za asili hazina chanzo, unavunja kanuni ya causality, unaijua kwanza hii sheria au naelewesha mtu asiye na uelewa?

Mimi namweka Mungu kama chanzo cha kwanza anayevuta kila kitu, sijui unaelewa?
 
Kusema atheist ni mgonjwa wa akili kwa sababu haamini hivyo ni kushambulia mtu badala ya kushughulikia hoja yake.

Kitanda tunajua kimetengenezwa kwa sababu tuna ushahidi wa moja kwa moja na wa kihistoria kwamba wanadamu hutengeneza vitanda.

Binadamu ni suala tofauti. Sayansi ya evolution haidai kwamba mwanadamu alitokea tu kwa bahati. Inaeleza mchakato wa mabadiliko ya viumbe kupitia urithi, variation, selection na muda mrefu.

Evolution yenyewe haijibu moja kwa moja swali la kwa nini kuna ulimwengu au chanzo cha kwanza cha uhai. Hapo ndipo hoja za kifalsafa kuhusu Mungu zinaingia.

Pia, kusema mwanadamu ni complex, kwa hiyo lazima awe ameumbwa na Mungu ni hoja yenye nguvu ya kifalsafa kwa baadhi ya watu, lakini si proof ya 99%. Hiyo asilimia inahitaji msingi wa kimahesabu unaoonyesha probabilities hizo zilitolewaje.
 
Karibu upewe elimu wewe ambaye bado hujui hata maana ya neno kabla.

Kabla ni neno linaloelezea muda, kama time haikuwepo, hakuna kitu kinachoitwa kabla kwa maana ya kibinadamu. Mungu haitwi yupo kabla ya muda, bali yuko nje ya muda.

Rudi shule ukajifunze basic physics na philosophy kabla ya kuja kunipa elimu mimi.
Huwezi kujibu hoja kwa kukimbilia neno, ambalo lipo sahihi.
Kabla ya space, time na maada.
Nini kilikuwepo?
Hili ndio msingi wa swali lako?
Inaonyesha wazi, huelewi hivi vitu.
Ndio maana umekimbia kabla ya kujibu.

Kama unaelewa, nawe ni mjuvi
Embu tuelezee kabla ya kuwepo
Time, space na maada ni kilikuwepo?

Darasa lipo wazi, tufute ujinga kwenye kichwa chako
 
Sheria ya mantiki inasema everything that begins to exist has a cause, ulimwengu una mwanzo hivyo unahitaji chanzo. Mungu hana mwanzo, Yeye ni eternal, hivyo hahitaji chanzo.
Hii ni sheria ya baadhi ya waamini mungu, sio sheria ya mantiki kwa ujumla inayokubaliwa na watu wote au kisayansi. Inaitwa "Kalam Cosmological Argument"
 
Huwezi kujibu hoja kwa kukimbilia neno, ambalo lipo sahihi.
Kabla ya space, time na maada.
Nini kilikuwepo?
Hili ndio msingi wa swali lako?
Inaonyesha wazi, huelewi hivi vitu.
Ndio maana umekimbia kabla ya kujibu.

Kama unaelewa, nawe ni mjuvi
Embu tuelezee kabla ya kuwepo
Time, space na maada ni kilikuwepo?

Darasa lipo wazi, tufute ujinga kwenye kichwa chako
Hujui kusoma kwa ufahamu wewe, nimeshakujibu hili bado una rudia kuuliza kitu kile kile.

Unarudia neno kabla ya muda, wewe kichwa ngumu elewa kabla ni kipimo cha muda! Huwezi kuuliza nini kilikuwepo kabla ya muda kuanza, kwa sababu neno kabla halina maana kule ambako muda haupo.

Yani unaitafuta jana kabla ya muda haujaumbwa, make it make sense? Jifunze kusoma kwa ufahamu kwanza.
 
Hii ni sheria ya waamini mungu, sio ya mantiki. Inaitwa "Kalam Cosmological Argument"
Maskini umekimbilia Google kutafuta jina la hoja na wewe uonekane umevumbua jambo la msingi? Ngoja nikueleweshe, Kalam Cosmological Argument ni philosophical logic sio sheria ya dini na iliundwa kwa kutumia misingi ya hesabu na uhalisia.

Kama unaona haina mantiki, pingana na misingi yake, kwanza inadai kila kilicho na mwanzo kina chanzo, pili inadai ulimwengu una mwanzo.

Soma kwa ufahamu uone ni jinsi gani umelitumia hilo neno pasipo kuelewa hata maana yake na namna linavyofanya kazi.
 
Hujui kusoma kwa ufahamu wewe, nimeshakujibu hili bado una rudia kuuliza kitu kile kile.

Unarudia neno kabla ya muda, wewe kichwa ngumu elewa kabla ni kipimo cha muda! Huwezi kuuliza nini kilikuwepo kabla ya muda kuanza, kwa sababu neno kabla halina maana kule ambako muda haupo.

Yani unaitafuta jana kabla ya muda haujaumbwa, make it make sense? Jifunze kusoma kwa ufahamu kwanza.
Hakuna unacho elewa,
Endelea kuamini,
Kama umejibu quote,
Zipo hoja kama time is real or not.
 
Ni wakati gani ulimwengu haukuwepo?

Ulimwengu umekuwepo milele.

Ulimwengu haujawahi kutokuwepo.

The universe didn't begin to exist.

Ulimwengu umekuwepo, upo na utaendelea kuwepo.

Hauhitaji chanzo.

Huyo Mungu hayupo. Na wala huwezi kuthibitisha kwamba yupo.

Huyo Mungu ni imani zenu uchwara za maandiko yenu ya kiimani. Mliyo andikiwa na wajinga wa kale. Sasa mnaamini mkichwamkichwa tu!
Muda ni sehemu ya ulimwengu. Hakuna wakati ulimwengu haukuwepo kwa sababu muda ulianza pale ulimwengu ulipoanza. Kabla ya hapo kulikuwa na timelessness hali isiyo na muda. Na kilichosababisha muda uanze lazima kiwe kiko nje ya muda. Huyo ndio Mungu. Soma fizikia uache kukariri maneno ya vijiweni.
 
Hakuna unacho elewa,
Endelea kuamini,
Kama umejibu quote,
Zipo hoja kama time is real or not.
Ukifanya mjadala na mimi lazima uwe timamu na ujue kujenga hoja kwa mapana, lasivyo utaishia kuandika madudu tu kama haya uliyo yaandika hapa.

Acha kujifariji na haya madudu, hata kama muda ungekuwa ni illusion bado ulimwengu wa physics una causal timeline, hakuna mwanasayansi makini aliyewahi kusema ulimwengu hauna mwanzo kisa tu anajadili asili ya muda, ulicho kifanya wewe kinaitwa moving the goalposts unahamisha mada baada ya kushindwa kujibu hoja ya mwanzo.
 
Kwanza watu hawaumbwi.

Watu wanazaliwa kwa kuzaliana wenyewe kwa wenyewe.

Watu hawaumbwi na wala HATUKUUMBWA.

Biblia ni hekaya na hadithi za kutungwa na wajinga wa kale.

Biblia sio uthibitisho.

Biblia ni hekaya kama zilivyo hekaya za Abunuwasi.

Biblia imejaa hadithi zisizo na logical consistency.

Huyo Muumbaji kabla ya kuumba kitu chochote kile, alikuwa wapi?

Huko alikokuwa kulitoka wapi?

Na pia kuliumbwa na nani?
huenda upo sahih kila kitu kinapotokea kimesababishwa asili ya mwanadamu ni ipi kama hajaubwa?
 
Back
Top Bottom