Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mheshimiwa Mpaka kieleweke ni kweli kwamba kuna tatizo kubwa huko kwenye Uongozi wa Juu ATCL,Na Mimi kwa bahati mbaya nilikuwa mmoja wa watu waliokumbwa na Adhma ya kukosa Usafiri kwa karibu masaa 6 kutoka Dar kwenda Arusha,hali iliyonifanya nisafiri kwa Gari kwenda Arusha.
Na Habari za ndani nilizozipata kutoka kwa mmoja wa Wafanyakazi wa ATCL ni kwamba Mkuu kwenye Kitengo cha pesa ni Mzembe na hakuna anayeweza kumwambia Chochote kwa sababu ni Rafiki Mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu (David Mataka).Sakata la Kuahirishwa kuruka Ndege Nyingi Alhamis na Ijumaa ni matokeo ya Kukosa Mafuta,Kwani Kampuni ya BP imekataa kutoa tena Mafuta kwa sababu hawalipwi pesa zao kwa wakati,Kampuni hiyo ya BP inasemekana inawadai ATCL pesa nyingi kwa kukopwa Mafuta.
Uongozi wa Juu wa BP unadai kuwa Mkurugenzi wa ATCL anatumia Vibaya Urafiki wake na Viongozi wakuu serikalini kuliendesha Shirika hilo,kwani mwezi wa tano watu wa BP walipata note kutoka kwa katibu Mkuu Wizara ya Nishati na baadaye kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais,walipogoma kutoa mafuta kwenye ndege iliyokuwa inaipeleka Timu yetu ya Mpira Cape Verde.Hivi sasa hakuna mtu yeyote anayeongelea suala hili la Utata wa malipo ya Madeni kutoka ATCL,kila mtu yupo busy kwenye Maandalizi ya Harusi ya Mtoto wa Kike (Monalisa) wa Mkurugenzi Mataka.
Waungwana nafikiri sasa imefika wakati Tumpime Kiongozi kutokana na sehemu anayoongoza,ikiwa mtu anashindwa ku-deliver ni lazima aachie ngazi.Mataka aanze kuoyesha Mfano.Mapungufu yake yamekuwa mengi kuliko Mafanikio..
Uteuzi wa bwana Dave Mataka sidhani kama ulizingatia perfomance na ufisadi wake wa hapo awali. Ndio maana sio ajabu hata kabla ya ATC kuwa na birthday yake ya kwanza, tayari linaingizwa kwenye wodi ya walio mahututi.
- Kama sijasahau, huyu mkuu ndie yule yule aliyejenga PPF tower kwa $20,000,000 badala ya zilizokadiriwa awali $9,000,000. Sijui sisi waTZ ni wasahaulifu au hatujali.
- Baadaye nafikiri alifikishwa mahakamani ingawa sijui kesi yake iliishia wapi. Hivi ilikuwaje mtu wa aina hii akapewa tena shirika changa kama ATC bila uangalizi wa karibu?
- Hivi JK alikuwa hayajui haya au uswahiba wao ndio ulio bora kuliko ATC?
- Kwa nini hizi nafasi za kazi za ukurugenzi wa mashirika ya umma na idara zake, ikiwa ni pamoja na ATC, zisitangazwe hadharani, nyumbani na kimataifa, ili wenye zifa wakaapply na kufanya kazi kwa mikataba inayotegemea utendaji wao badala ya kusimika miungu watu wasiowajibika kwenye hizo nafasi?