ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

Nasikia baada ya habari hii kutoka jana.. wanataka kuharakisha kuanzisha safari za Airbus DAR - Mwanza - Dar... sikilizeni leo au mapema wiki ijayo.. nawaambia mapema likitokea jambo mtu asisema "mwanakijiji alijuaje" kwa sababu mambo mengine huitaji manabii kuyasahihisha.

Hatuombei, lakini wasije wakatumwaga na haraka zao!
 
Ndege zimekua grounded sababu ya madeni kuzidi. Tupo tu tunang'aa macho airport. Hatujui hatima yetu. JF munafahamu hiyooo???? Wako wapi waandishi wa Tanzania?
 
Naambiwa ile Boeing yetu 737 imekuwa charter plane ya taifa stars.. maraipo Cape Verde na Alhamis hii inaenda Cameroon....
 
habari zilizotufikia wana JF ni kwamba hali ya hatari imetanda hapo airport
kila mtu akikimbia kwamba si mfanyakazi wa atcl..airtanzania imecancel flt zake zote kwasababu ya kukosa mafuta,,habari za uhakika zinasema kumbe toka juzi kampuni imekuwa ikifuta flt zake kwa kukosa hale ya mafuta ya kuwapa wanaotoa mafuta BP......HAKIKA NI SWALA LA KUSIKITISHA MAANA NIMEKUWA NIKIRUKA NA KAMPUNI HII TOKA NAANZA KAZI SASA INASIKITISHA KUONA WAKIWA KATIKA HALI MBAYA KISASI HIKI..JE NAJARIBU KUULIZA NANI ALAUMIWE..NA HABARI ZILIZOTUFIKIA INASEMA KWAMBA TATIZO LA PESA NI KUBWA SANA KUTOKANA NA MHESHIMIWA WA FINANCE ANAEJULIKANA KAMA ELIASAPHY KUAMUA KULIPA HELA KWA SEHEMU AMBAZO ANAJUA ANAPATA ULAJI YAANI 10PERC ....INASEMEKANA ATCL IMEKUWA IKIPEWA MSAADA NA MADENI MAKUBWA NA HAWA BP...NILIPOJARIBU KUWAULIZA WATU WA BP WAMESEMA HAKUNA NJIA YA KUSAIDIA TUMEWASAIDIA VYA KUTOSHA..SASA HII IMEKUWA NI TATIZO KWA KILA NCHI..NA TAARIFA MBAYA ZAIDI NI KWAMBA KILA MKURUGENZI ANAEPIGIWA APOKEI SIMU NA AKIPOKEA AKIJUA ANAULIZWA ANAJIBU MATUSI AMBAYO HAYATASAIDIA KATIKA KUREKEBISHA TATIZO
SISI KAMA ABIRIA TUNAOMBA WAZIRI UJE HAPA AIRPORT KUONA TUNAVYOTESEKA MAANA HATA CHAI WAMESHINDWA KUTUPA BADA YA KUKATALIWA KUTOKANA NA MADENI NA HII HOTEL YA HAPA....
TUNAOMBA MSAADA WENU KWA WALIOKARIBU WAJE KUTUSAIDIA TUPATE HATA MAJI...NA UKUWAULIZA ZIKO CANCEL HAKUNA ANAEKUBALI KUJIBU AKIDAI HANA LA KUJIBU
KILA SEHEMU NI UFISADI TU JAMANI HAYA MAMBO YATAISHA LINI ?????
TUKO HAPA TOKA SAA TISA USIKU HAKUNA ANAESEMA TUNAENDA MWANZA AU LA NA UKIUULIZA HAKUNA ANAJIBU
EE MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mbona ndege inaruka kila siku huku imejaa? Pesa wanapeleka wapi?

Nimefanya safari wiki iliyopita na nusura nikose nafasi kutokana na ndege kujaa.

Je, ni lini matumbo ya mafisadi yatajaa?

Kama habari hii ni ya kweli naomba nianze kujitoa taratibu kutoka kwenye kuchangia mafisadi.
 
Inasikitisha! Hiyo ndege ndo inatutangaza watanzania nje! A national flag bearer inakosa mafuta! Na ndo majuzi tu tumeambiwa kuna Airbus imekodishwa sasa italipwaje hiyo!
 
Kwa Kweli Kwa Masikitiko Makubwa Napenda Kusema
Sitoshangaa Kuona Atcl Ikifilisika Kama Hali Inakuwa Ndio
Hii...hii Hsbsri Ni Kweli Nilifikiri Utani Niliposoma Na Ndio Maana Nkaamua Kuchunguza Kwanza Kabla Ya Kujibu.....ukweli Halisi Unauma Sana..kwanza Kwa Habari Za Uhakika Ile Ndege Ya Airbus
Imeanza Kuleta Matatizo Na Hata Majuzi Nilienda Nayo Mwanza
Nikaanza Kubishana Na Engineer Mmoja Akdai Ok Wakati Nadege Ina Vibrate...baada Ya Muda Alikuja Mzungu Na Kukiri Na Kusema Inapelekwa Matengenezoni Muda Si Mrefu ....ina Sikitisha Kununua Ndege Mbovu Kwa Pesa Za Wananchi Na Huku Wakuu Wakiwa Wanaiangalia Hii Hali Ni Ya Hatari Sana Na Kama Itaachwa Narudia Tena Sitoshangaa Kuona Kampuni Hii Ikikaribia Kufilisika Kama Si Kusahauliwa Katika Ulimwengu Wa Anga...nilijaribu Kufwatailia Hapo Nyuma Muda Mwingi Kuna Wakati Walikodisha Ndege Ya Wazungu Uko S.africa Na Wakatushusha ..kiliniuma Nikawaandikia Wana Jf Wakiwaona Wahusika Watuulizie Kulikoni..mpaka Hali Hii Inatokea Nilipofika Dar Nilimfwata Mhusika Akanjibu Hawana Cha Kusema Nilipoingia Kwa Undani Nikaambiwa Hii Ndege Wamesaini Mkataba Wa Miezi Mitano Kwa Hiyo Isiruke Iruke Wanaendelea Kulipa..na Hivi Tunavyoongea Wanalipa Doller 180,000 Kwa Ndege Wasioitumia...enyi Wananchi Tufanye Nini Na Hawa Watu
Leo Hii Nimepita Kuulizia Pale Ofisi Zao Za Mjin Nikakuta Watu Wengi Na Abiria Wakiwa Wanawasubiri Wahusika..nikapewa Namba Ya Kupga..akapokea Mtu Anaitwa Eliasaphiew Akisema Hana Cha Kusema Tusubiri Wako Mkutanoni..mpaka Sasa Apokei Tena Simu Yoyote Baada Ya Kujaribu Namba Tofauti......inaonekana Tatizo Si Pesa Hiizi Ndege Wanapata Abiria Kweli Tena Wengi Kwa Hiyo Tatizo Nafikiri Liko Kwenye Matumizi Kama Alivyoonyesha Mhusika Kwamba Wanalipa Sehemu Iyoonyesha Kuna Ulaji Tu......na Kwa Kweli Kwa Halii Hii Sijui Kama Iafika Hii Kampuni...nafikiri Muda Umefika Wananchi Waweze Kuamua Nini Cha Kufanya Haiwezekani Kikundi Cha Watu Wachache Wakaendelea Kuiua Kampuni....mama Kilango Kama Upo Nimesikia Jana Mambo Yako Embu Tutangazieni Haya Uko Bungeni Kabla Amjaja Kutuambia Kampuni Imefilisika......nafikiri Muda Umefika Kulazimisha Watu Wawe Comitted.........
Enyi Wafanyakazi Wa Atcl Hatujawaona Uku..iweje Mnapigiwa Makelele Wa Msada Wa Maisha Yenu Na Watu Wasiofanya Kazi Atcl..
Mtaamka Lini ....tusubiri Hatima Yashirika Hili
Wenu Awapendae
Predeshe Makoti
 
Mhh kama hali ndio hii kweli hatari,jana nilipata info moja toka kwa rafiki yangu alikuwa atcl sijui walimwachisha au alistaafu...kwamba katika zile ndege mbili zilizoletwa moja imeshindikana kabisa kiaaluma cha wanaita wamigraundi kama sijakosea...na hata hii ndege iliyobaki ndogo ina tatizo kubwa lakini inaendelea kuruka kwa sababu ya amri ya mkubwa mmoja...ikitokea swala la moto naskia hakuna kinachoweza kuonyesha kama kuna moto na nii sehemu gani kwa kweli nilishtuka maana sikuwa na aidia ya mambo ya ndege accounts na ndege taka mbili tofauti......ukija kwenye hii kubwa sijajua hasa tatizo ila nimeshangaa kuona ikitetemeka mara kwa mara....nafikiri kwa msaada wa maisha ya watanzania tunaomba wahusika wazikague vyema hizi ndege zetu zote kuanzia precission mpaka atc kuogpa majanga yatakayotupata........swali lingu bado nauliza hawa watu wakiwa wanakula hela za wananchi hawakujua ipo siku zitaisha na aibu ikawajia juu ya vizazi vyao au mpaka ashuke nabii kuwangazia umma hali ni mbaya ndipo viongozi wa nchi watakapoamka na kujua ni bora turekebishe mapema kabla ya kuuja kuharibika zaidi....tatizo kubwa ni kula bila kuangalia kilichobaki..hili liko mpaka bungeni na kama ukiweza kula na kuangali salio kila mara hata pale likiwa dogo unahangaika kulijazia hata kama kusahau mshahara likukua unaendelea kale kamchezo....kwa kweli kazi ipo kwenye hili shirika
loh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huyo Mataka hana uwezo wowote wa kuendesha shirika na alishashindwa siku za nyuma lakini JK hakutaka kusikiliza maoni ya wengi alipomteua tena. Sasa kuna kila dalili kwamba kampuni hiyo itaporomoka tena na labda sasa hivi ndiyo tutaizika kabisa
 
Itabidi nidai fedha zangu maana hapa nilipo nina ticketi mbili za ATC! Ni aibu kwa taifa kukosa ndege flag bearer yenye uhakika. Yaani hata precision wanawazidi sasa maana wanaboeing na wana mpango wa kuagiza nyingine.
 
mmh kile kiwaziri kinacho husika si kiliwachimba mkwala wafanyakazi wa ATC si mnakumbuka wakati wanapokea ndege used ile wakatudanganya mpya sijui inaruka yenyewe ile.Hiki kiwaziri nacho kina kula pale kijitokeze sasa kujibu tuhuma.
Nae tumkomalie ajiuzuru.
 
Nawaletea taarifa hii ambayo ingeliweza kulisaidia sana shirika letu la ndege kama ingefanyiwa kazi.

Jana ATCL wameshindwa kupata mafuta ya kurusha ndege zao na hivyo kushindwa kusafirisha abiria wao kwenda maeneo mbalimbali nchini.


Isome hapo chini .
 

Attachments

vii) Kukiviza kitengo cha ufundi cha ATCL kiasi cha kukifanya kishindwe kabisa kuzifanyia matengenezo ndege za ATCL kama ilivyokuwa awali.
 
Mod,naomba ipelekwe kwenye jukwaa la siasa kwani nimekosea kuipost hapa kwenye matangazo ile hali hili sio tangazo
 
Mheshimiwa Mpaka kieleweke ni kweli kwamba kuna tatizo kubwa huko kwenye Uongozi wa Juu ATCL,Na Mimi kwa bahati mbaya nilikuwa mmoja wa watu waliokumbwa na Adhma ya kukosa Usafiri kwa karibu masaa 6 kutoka Dar kwenda Arusha,hali iliyonifanya nisafiri kwa Gari kwenda Arusha.

Na Habari za ndani nilizozipata kutoka kwa mmoja wa Wafanyakazi wa ATCL ni kwamba Mkuu kwenye Kitengo cha pesa ni Mzembe na hakuna anayeweza kumwambia Chochote kwa sababu ni Rafiki Mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu (David Mataka).Sakata la Kuahirishwa kuruka Ndege Nyingi Alhamis na Ijumaa ni matokeo ya Kukosa Mafuta,Kwani Kampuni ya BP imekataa kutoa tena Mafuta kwa sababu hawalipwi pesa zao kwa wakati,Kampuni hiyo ya BP inasemekana inawadai ATCL pesa nyingi kwa kukopwa Mafuta.

Uongozi wa Juu wa BP unadai kuwa Mkurugenzi wa ATCL anatumia Vibaya Urafiki wake na Viongozi wakuu serikalini kuliendesha Shirika hilo,kwani mwezi wa tano watu wa BP walipata note kutoka kwa katibu Mkuu Wizara ya Nishati na baadaye kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais,walipogoma kutoa mafuta kwenye ndege iliyokuwa inaipeleka Timu yetu ya Mpira Cape Verde.Hivi sasa hakuna mtu yeyote anayeongelea suala hili la Utata wa malipo ya Madeni kutoka ATCL,kila mtu yupo busy kwenye Maandalizi ya Harusi ya Mtoto wa Kike (Monalisa) wa Mkurugenzi Mataka.

Waungwana nafikiri sasa imefika wakati Tumpime Kiongozi kutokana na sehemu anayoongoza,ikiwa mtu anashindwa ku-deliver ni lazima aachie ngazi.Mataka aanze kuoyesha Mfano.Mapungufu yake yamekuwa mengi kuliko Mafanikio..
 
Inasikitisha, Infadhaisha, Inachefua, Inadumaza, Inadidimiza, Inakandamiza, Inatia Aibu, Isahihishwe!!!!
 
Nilipata habari hizi za matatizo ya ATC kwa wiki nzima na nimeamua siligusi tena suala hili kwa sababu ni ujinga, upuuzi, na kejeli kwa watu wote wanaolitakia mema shirika hilo. Tumepiga kelele kuanzia Novemba mwaka jana juu ya matatizo makubwa ndani ya shirika hilo, tumeonesha na ushahidi kuwa lina ufujaji mkubwa wa fedha, lisilona kipaumbele na linaloendeshwa kishkaji..

Sasa wamenunua hilo li Air Bus ambalo limezidi kurundika madeni kibao... watumie maji sasa kulirusha.. grrrrrrrrrrrrrrrr
 
Waheshimiwa Lile Ni Shirika Letu, Na Wamekosea. We Have Tu Help It Stand And Give Ushauri Nini Wafanye Ili Liendelee Aidi....!
 
Back
Top Bottom