ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

""Lets use fonts wisely.""
haswa:::::::::::::::::::::::::::::: mkuu hii itaruka jK atakapokuwa serious na mali za umma
 
Ile ndege "mpya" iliyokodiwa na ATC kutoka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia aina ya Airbus 320 bado haijaanza safari zake, na kwa karibu miezi saba sasa imeishaligharibu shirika hilo zaidi ya shilingi Bilioni 2 za malipo ya kukodi na matengenezo mbalimbali ya kuifanya ndege hiyo ipendeze.
Habari za kuaminika toka ndani ya shirika hilo kongwe la ndege nchini zinasema kuwa hadi hivi sasa ndege hiyo ambayo ilipokewa kwa mbwembwe wiki chache zilizopita bado haijaanza safari zake na hata itakapoanza itaanza kwa deni kubwa ambalo itachukua muda mrefu sana kuweza kuona faida. Kwa mwezi huu tu unaoisha shirika hilo litalipa karibu shilingi milioni 700 kama malipo mbalimbali yanayohusiana na ndege hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya ATCL wameanza kuonesha wasiwasi endapo habari za jinsi ndege hii inavyoshughulikiwa zitajulikana na vyombo vya habari. Hata hivyo hofu hizo zimechelewa kwani hadi hivi sasa inajulikana wazi kuwa mkataba mzima na jinsi ndege hii ilivyopatikana, kuingizwa na kusimamiwa na uongozi wa juu wa ATCL ni aibu kubwa kwa taifa.

Licha ya mkataba huo wa Wallis ambao unakodisha ndege hiyo kwa karibu dola milioni 30, shirika la ATCL liliingia mikataba mingine na kampuni ya Aeroman ya El Salvador ambayo ilipewa jukumu la kuitengeneza ndege hiyo ambayo ilikuwa na mapungufu mengi ambayo unaweza kuyaona kwenye eneo la "Pics and Documents" hapo juu. Mkataba huo ambao na wenyewe si chini ya shilingi milioni 400 nao unaliongezea deni shirika hilo.

Pamoja na kampuni ya Aeroman, ATCL imeingia mkataba mwingine na shirika la ndege la Mauritius ili kuwapatia mafunzo na mafundi wa kuisimamia ndege hiyo. Kinachoshangaza watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia suala hili ni jinsi gani shirika ambalo halina wataalamu na marubani wenye uzoefu wa kurusha ndege aina ya Airbus ambayo ni mojawapo ya ndege za kisasa na zinazotumika zaidi duniani hasa kutokana na kutumia kiasi kidogo cha mafuta kulinganisha na Boeing iliweza kuingia mkataba wa kuipata ndege hiyo bila kuandaa raslimali watu.

Habari mpya zinasema kuwa baada ya taarifa za ndege hii kucheleweshwa kuruka kutoka mapema leo kuna dalili kuwa safari za ndege hiyo zinaweza kuanza saa yoyote kuanzia sasa na si mwezi mmoja baadaye kama ilivyokuwa inatarajiwa.

KLH News inatoa wito wa serikali kufuatia ukodishaji wa ndege hiyo na kuangalia mapungufu yote yaliyotokea kabla (Mungu aepushie mbali) jambo baya halijatokea na ndipo watu wajifanye wanajali na wanataka kufuatilia.

Kabla ya kukodishwa na ATCL ndege hiyo ilikuwa inamilikiwa na shirika la ndege la Jamaica ambao walipoiachia ilikuwa na kila aina ya ubovu wa ndani ambao haulingani na umri wake. Hata hivyo haijulikani ni kwanini ilipoingia nchini ndege hiyo ilisemwa kuwa imekodishwa toka kampuni ya Wallis Trading ya Ufaransa wakati mkataba uliosainiwa ambao KLH imeuona unaonesha wazi kuwa kampuni hiyo ni ya Liberia (hata kama kampuni yake mama ni ya Ufaransa).
 
hapo lazima kuna mkono wa mtu na kuna harufu kubwa ya rushwa ndani yake..mm naona hapo tuhesabu tu shirika hili limesha aga dunia....wamekodi kwa bei ghali sana sasa watawezaje kulipa na shirika kupata faida kama siyo kuliua shirika nn..Mashirika mengi ya umma yamekufa kwa design hii hii hapo ss wadanganyika tuhesabu muda si mrefu shirika linakufa.Yaani wanaenda kukodi ndege Liberia kwa wachovu wenzetu kweli ndege itakuwa nzima kweli mmmh! watendaji wote na bodi nzima wawajibike kwa hilo.
 
Ningeseme kuwa Bwana David Mataka afanyiwe uchunguzi kwani huyu bwana sio mfanyi biashara mzoefu ila ni mtu anayejua kushawishi sana watu. Pia ni menda sifa........
 
MMh nchi yetu imejaa watu wanafiki na watu ambao wakipewa kitu kidogo wanatulia Jamani hii ni aibu na pia ni ujinga hela nyingi kupotea hivihivi plz Tanzania tusimame tuwaondoe watu kama hawa wanaichezea hii nchi hakuna mwingine atakeweza kutusaidia.....
hatupendi vita lakini kwa jinsi tunavyoenda iko siku watu watapigana
 
sioni sababu ya kuendelea kuwa na shirika ambalo linatumia tu pesa ya walala hoi na halina faida yoyote kwao.
tukiomba hesabu ya matumizi na mapato ya atcl sidhani kama wataweza kutuwekea hadharani kwa ilivyojaa wino mwekundu wa hasara!
 
Hivi hadi warudishe fedha zote walizototumia kuwekeza na kuanza kuingiza faida si itakuwa kasheshe.. halafu wataweza kweli katika ushindani wa bei...?
 
hamna kitu! shirika hili litaendeshwa kwa hasara kwa atleast miaka saba wa sabiini ijayo!

mwanakijiji hebu tuombee hesabu za mapato na matumizi ya atcl tafadhali
 
ATCL yaani ni kichefu chefu!!

Lakini ni viongozi wa serikali ndio wanaowalea hawa, kwani mmesahau Nyang'anyi na kashfa ya mahujaji! Serikali Kuu ilipata hasara ya bilioni 5!! lakini hakuna yeyote aliyechukuliwa hatua!! sasa mnatarajia nini?

MKJJ unazungumzia hasara ya bilioni 2, wakati waliweza kusamehe bilioni 5!!
 
hamna kitu! shirika hili litaendeshwa kwa hasara kwa atleast miaka saba wa sabiini ijayo!

mwanakijiji hebu tuombee hesabu za mapato na matumizi ya atcl tafadhali

utakimbia..!! please don't ask me that again... kama ni kulia nishalia sana.. Mattaka should've been gone a year ago!!
 
Ile ndege "mpya" iliyokodiwa na ATC kutoka kampuni ya Wallis Trading ya Liberia aina ya Airbus 320 bado haijaanza safari zake, ilikuwa na mapungufu mengi ambayo unaweza kuyaona kwenye eneo la "Pics and Documents" hapo juu. ).

Mkuu mbona hatuzioni hizo picture?
 
kuna wakati nilikuwa nikifikiria kukimbia tanzania nikaona ngoja niangalie shule ya mwisho ni wapi nimepata kadigirii na kusema ngoja nijiajiri baadae nkaona mwisho utakuwa ni kuajiriwa na kuona shirika nililoplipenda zaidi kufanya kazi litakuwa atcl baada ya kubiinafsishwa lakini nilipoitwa kwenye interview nakuambiwa nimepita kwa kweli ilinichukua miezi si chini ya minne kabla ya kukimbia pale accounts,,sikupenda hivyo ila niliapa kulitumikia nchi yangu na wazazi wangu kwa moyo wote na kusema kama nitaiba nitawaibia wazazi lakini si watanzania...si kwasababu zipi walakini ni baada ya kuangalia matumiizi yanayofanyika pale hakuna alieumbwa kwa moyo wa ubinadamu akafanya mambo yale...napenda kuwaokeza tu nilikuta peni za sh 350 mtaani unakuta risiti ya sh 2000 kwa kila moja na kwa mwezi peni 500 kila department 100!!!!jamni sisi ni binadamu tujiangalie na haya mambo tusifikirie kesho kampuni itakufa no prblm kumbuka watoto unaowasomesha wanatarajia kufanya kampuni kama hizi eeh mungun tusaidie.....bado nafikiri kwa nini nisiende kubeba mabox kama watu wanzaidimkuiba mpaka sasa kwa style hiizi......maziwa madogo yanauzwa 5000/= kwenye risit unakuta sh 10000..sasa hivyo vingine zaidi nisiwakatishe tamaa mlioko uko udsm ...somen mjee kuona yaliopo msije kukkimbia nchi mkatuachia vichanga vyetu...ila nasema narudia tena kusema hakika kama kuna mtu atathubutu kuyafwatilia haya mashirika ya umma nakuweka hadharani matumizi yake nahisi udsm ingekuwa NHC kila mmoja angesema hapa ndio nshafika ...enyi wakurugenxi amwogopi mungu jamani hata kidogo?????embu angalieni ubinadamu nawakaribisha wenye kupenda nchi yetu tutoe maoni kuweza kumsaidia huyu ndugu yetu ZITOO ama zito haya mambo unayajua na kama unayajua mbona umekaa kimya ???????unataka kuja kusikia zimeanguka ndio mkimbilie kupeana kwenye tume ...embu tuliangalie hili....
 
kuna kipindi kaka yangu mmoja alienikunvinsi kwenda pale yeye alikuwa acc nilipoingia nilimuuliza kitu cha kwanza niliuliza huku ndani kuna ambae anaenda kanisani au msikitini jibu lilikuwa rahisi kula chako uondoke....hakika sikujuta maana nilishaanza kujiajiri na kusema tena niliapa kuiiba kwa wazazi na familia yangu lakini si watanzania....,,kibaya sikuna cha kula mle ndani zaidi ya kupitisha risiti amabzo mwisho walioenda kununua ndio wanafaidika....,,nashukuru kuona na yule kaka yangu amekimbia kabisa tena nje ya nchi na akutaka kabisa kusikia hayo...nasikitika kuna ushauri alioutoa mpaka sasa hakuna aliekubali kuufwatilia n ndio unaoliumiza hiili shirika..mwisho nawaasa wenzangu hapo acc....tusikubali kufile uozo tujaribu
kuangalia haya
 
Nasikia baada ya habari hii kutoka jana.. wanataka kuharakisha kuanzisha safari za Airbus DAR - Mwanza - Dar... sikilizeni leo au mapema wiki ijayo.. nawaambia mapema likitokea jambo mtu asisema "mwanakijiji alijuaje" kwa sababu mambo mengine huitaji manabii kuyasahihisha.
 
Back
Top Bottom