Atakayeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini

Atakayeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini

Hahaha unamtisha nan?? Ccm walishajipanga siku nyingi kuiba kura na wameshafanikiwa! Na hata hivyo wameshajua kuwa wanaich wamewachoka wanabaki wanafiki mioyoni mwao. Kikwete ametumia mabavu ya kiti chake kwani alishaona chama chake kimemvunjikia mkononi mwake. Hata wewe pia ni mnafiki

Hivi mkishindwa tu, ni mmeibiwa kura?
 
Mijitu inabebana hospital na inalalamika kila siku leo inatuambia sisi wanaotulalamikia sina hela ya kumuona dr"Eti tutaisoma namba khaaaaaaaaaa !!!!!!!!!!!!!" kauli mbiu sasa HAPA KAZI TU.
 
Hata zile mil 6 za EL ni kura za mashetani wenzenu siyo za watanzania ila kwa vyovyote vile hata simba au yanga ikifungwa huwa inatafuta maneno ya kujifariji kwa hiyo siwashangai na siku zote mnaibiwa kura na ndiyo maana hakuna hata mbunge mmoja wa upinzani mjinga mkubwa.

Ww ni hasara kwa taifa
 
Mtu asiyekuwa na uhakika wa maisha kujidai oh mtaisoma namba ni fedheha tupu.
 
Huo ndio ukweli hata kama imetumika lugha ya ukakasi kwa mtoa post, ila itabaki kuwa hivyo,always watu wa chini ndio wanao feel pinch ya ugumu wa maisha,and the fact is baadhi ya vyama vimepata kura nyingi vijijini ambako kuna limited capacity ya ku analyze issues,miji mingi ambayo iko exposed to information trends za kura zinajionyesha.Na ni walewale wananchi wa kawaida ambao wanashabikia mambo kichwakichwa ndio wanaoumia bei ya mafuta ya taa ikipanda holela na ARVS feki zikisambazwa.Ikumbukwe kua ujamaa umebaki kua imani na tulipofikia kila mtu ataubeba mzigo wake,and this hold as far as we are in free market where Govt cant provide all services apart from public goods..and the Govt is just a referree to regulate issues.That is unapoimba wataisoma namba jiulize hali yako ikoje au mpaka leo hii you are struggling kupata chakula na mavazi!..Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe kwa kuwa action and reaction are equal but opposite.Keep on messing with ballot box and the time will tell with your mind full of hell hopes!
 
Ndio matatizo yale yale, huwezi kumsoma mtu ukamwelewa kabla ya kuandika. Mleta mada hajasema kumchagua Lowassa bali kazungumzia kuirudisha CCM madarakani. Wewe kwa akili yako unaweza kusema kumrudisha Lusinde Bungeni ni kuitakia kheri nchi? Au Kessy wa mizaha ni sahihi kwa ulimwengu wa sasa uliojaa challanges mbalimbali?
Ok fine, ungeweza kumkataa Lowassa na kumkubali Magufuli lakini kwa kumpa watu walewale wa ndioooo unadhani unamsaidia huyo Magufuli kuweza kutimiza azima yake ya yale aliyo ahidi? Ni kujidanganya kudhani kuwa Magufuli na ccm ileile anaweza kufanya lolote la maana zaidi ya kufanya mambo yawe magumu zaidi.
Mie nakubaliana na mtoa hoja kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ndio waisoma namba. Wataendelea kulala mzungu wa nne wakijifungua, watoto wao watakalia matofali shuleni, watoto wao waliojaliwa vipaji watashindwa kusoma elimu ya juu kutokana na umasikini wao na wale waliohitimu watabakia majumbani kwa kukosa ajira kwa vile hawajazaliwa katika familia zilizotukuka na kuishia KUISOMA NAMABA.
Mkuu usipate taabu kujibu,hata maandiko matakatifu yanasema 'wana macho ila hawaoni"..yawezekana hajaona the hidden fact kwenye post hio ya mtleta hoja..kinachotuvuruga akili ni U Vyama!
 
Kuna wengine washaanza kuisoma namba huko Kagera... Wamesomeshwa namba kwa kunyang'anywa AMBULENCE..TV...
 
yani nimecheka hadi machozi. kusema ukweli hamna kuoneana huruma hospitali bila pesa hakuna matibabu tena madaktari wakaze kweli kweli. walimu na wenyewe wakaze kweli kweli. polisi wapige pesa kwenda mbele bandarini na TRA vivo hivyo. nina uhakika watu wa mjini wata survive ila huko bush tutegemee vifo tu

Wafe tuu mijitu mijinga sana
 
Bado hujatushawishi.kama huyo unayemtaka angekuwa na uchungu asingekuwa fisadi wa mali ya umma.
 
Labda nikuulize je kama lowassa jina lake lisingekatwa na ccm akapitishwa kuwania uraisi ungempigia Kura yako? Pelekeni unafiki huko.mnajifanya mna uchungu na nchi hii kumbe ni unafiki mtupu.nchi hii itakombolewa na wenye uzalendo wa kweli na uchungu bila kujali Chama .nahuyu si mwingine Bali ni john pombe Magufuli.
 
Nilishasema nataka bei ya mafuta iwe 4,000 kwa lita, sukari 3,000 kumwona daktari 15,000 n.k n.k. I don't care
 
Mbowe hawezi kuisoma namba. Ana biashara zake plus mshahara wa ubunge. Lowassa pia ana hela zake. Mbatia mhandisi pia mbunge. Tundu Lissu advocate. Ana hela zake. Kushangilia eti UKAWA watakoma ni ujinga. Atakayeisoma namba ni yule ambaye akija hospitali ukamwambia hela ya kumuona daktari ni 6000 anapanic anaanza kuwalaum madaktari.

Anaeisoma namba ni yule mwenye kipato cha chini, bima ya afya hana, hata hela ya kumshonea mwanae uniform hana. Anaeisoma namba ni yule ambaye hawez kuafford milo mitatu iliyo kamili kwa siku. Ni upuuzi kwa mtanzania wa manzese (asiyeweza kulipa ada ya shule ya 40k kwa mwaka) kusema Duni ataisoma namba wakati ana taaluma yake na pesa zake. Unaeisoma namba ni wewe ambaye tokea umemaliza chuo ni miaka mitatu huna kazi (halaf kwa upumbavu unashabikia hapa kazi tu). PUMBAVU SANA.

Unaeisoma namba ni wewe ambaye mtoto wako akiumwa mafua tu huwez kuafford dawa. Asilimia kubwa ya waliomchagua pombe ni ile 30% ya watanzania wanaoishi chini ya mstari wa umasikini (kipato cha siku kuwa chini ya dola za kimarekani 1.9.. sawa na sh 4000 hiv).

Hawa ndo wanaisoma namba, miaka 54 ya uhuru bado wanaishi gizani, bado hawawez kupata maji safi na salama...Halaf walivyo wapumbavu wanashabikia hapa kazi tu.. Kweli ni kazi..

Maana kushindia mlo mmoja kwa siku so mchezo, ni kazi kweli. Kumnywesha mwanao mwarobain kwa sabab huwez kumudu bei za madawa, so mchezo ni kazi haswa haswa.

Kama watanzania wenyewe ndo hawa ambao hawajitambui, WE HAVE A LONG WAY TO GO.

Umemaliza yote mkuu wangu tatizo manyani wa lumumba hawajitambui.
 
Kweli kabisa kaka mfano kwetu muleba kusin wameniangusha kweli kumrudisha yule mama fisadi tibaijuka na huko ni watu wenye shida kweli sasa nimeshawambia ndugu zangu sitaki simu za mizinga wafe wenyewe na ccm yao mimi huku dar sina shida kila mtu afe na shida zake.

Kweli kabisa mkuu ingekuwa dodoma tungesema elimu tatizo lakni kwa kagera ni ajabu sana waache waisome namba
 
Eti lumumba timu anakuja anamtaja lowasa wakati mwenye post hajataja mtu yeye anaongelea ccm,kweli nimeamini akili ndogo hawezi kutawala akili kubwa..
 
Tanzania hii ya ajabu sana
1.kuna baadhi ya hospital zake mfagizi ndo dr, ndo nurse, ndo mgawa dawa
2mifuko ya plastiki maarufu kama Rambo huvaliwa na wakunga wakati wa kuwahudumia wanaojifungua
3. ndio wazalishaji wa tanzanite lakini ni wauzaji namba 4
4.watu wake ni wepesi wa kusahau hata pale serikali inapo poka haki ya raia baada ya muda inasahau kabisaaaaaaa
 
Back
Top Bottom