Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

EMT hata mimi nakubaliana na baba Askofu, maana sioni mantiki ya mtu kumzikia ndugu nyumbani badala ya kwenye makabuli achilia mbali suala la matumizi mabaya ya ardhi. Ukweli ni kwamba sioni raha yeyote na wala sioni faida yeyote ile (ukiachia suala la kuenzi/kumbukumbu) ya kuweka kaburi ndani ya eneo la makazi ya kuishi maana kwa kufanya hivyo ni kuongeza simanzi kila unapofika nyumbani na pia kuwaumiza wenye mioyo laini kila wanapokuja kukutembelea na kukuta makuburi nyumbani.

Tunaweza kuwaenzi wapendwa wetu kwa kuwatengea eneo maalum na kuandaa siku maalum za kwenda kuyatembelea makaburi hayo na kuwafanyia sala na dua kulingana na imani na tamaduni za watu mbali mbali. Ukweli ni kuwa siungi mkono suala la kuwazikia watu majumbani na kuwafanya mliobaki muwe mnaishi na makaburi ndani ya makazi yenu.

Mkuu Suaa ni Kwamba, hilo Eneo Maalum litatoka wapi ?
Hizi Tamaduni nyingine tumezikuta, hatuna budi tuziache Jamani, Nadhani Eneo likiwa Low Density ki sheria linaruhusiwa kwa Maziko, wataalam wa sheria akina EMT wataliweka sawa hili.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Suaa ni Kwamba, hilo Eneo Maalum litatoka wapi ?Hizi Tamaduni nyingine tumezikuta, hatuna budi tuziache Jamani, Nadhani Eneo likiwa Low Density ki sheria linaruhusiwa kwa Maziko, wataalam wa sheria akina EMT wataliweka sawa hili.

Labda sheria za miji na makazi. I am not sure.
 
Absolutely mkuu, Yaani ulichokiandika ni kweli kabisa...
ipo miradi kwenye badhi ya vijiji hapa Tanzania watu wameanza kutumia mashamba yao ya vijijini kama dhamana za benki. Hii ni njia mojawapo itakayotutoa watanzania kwenye umaskini, ukulima wa hand to mouth angalau mkulima mmoja aweze kulisha watu kadha. Hii inawezekana kwa kutumia vifaa vya kisasa ambavyo ni ghali.

Tufikie mahali tuone kuwa kuuza mahindi Kenya ni fursa na tuichangamkie badala ya kusaka wanaofanya hivyo na kutaifisha magari yao! Sasa tunapoendelea kupamba rasilimali zetu chache tulizo nazo kwa makaburi na kuziondolea kabisa thamani hiyo, ukizingatia kahawa ndio imekwishaondoka kwakweli tunajimaliza wenyewe. Baba Askofu kaona mbali ambapo wengine wataona watakapokuwa wamechelewa.

Nafiki ardhi ni msingi mkubwa sana wa maendeleo kwa makabila mengi hapa nchini. Hata hivyo, kuna baadhi ya makabila kama kabila la kichaga ambalo ardhi ni mali kutokana na sababu mbalimbali. Kwa mfano, wachaga wanalima mazao ya kudumu kama ndizi na kahawa ambayo hukaa shambani kwa muda mrefu sana. Unawezakuta migomba na kahawa zilipandwa miaka ya zamani sana na mababu na hivyo baadhi ya watu wanapenda kuendeleza hiyo identity kwa sababu wanazoziua wao wenyewe.

Nilisoma huko nyuma kuwa wachaga wanapenda pia kuheshimu makaburi ya watu ambao siyo wachaga. Kwa mfano, miaka ya nyuma kulikuwa na Wakenya, kama sijakosea Wakamba, waliokuwa wanaishi maeneo ya Kilimanjaro na walitumia ardhi yao kuzikia ndugu na jamaa zao. Walipoandoka/hamia Kenya (Ukambani) Wachaga walichukua ardhi yao lakini waliacha makaburi ya Wakamba kama yalivyokuwa. Unaweza kukuta bonge la shamba halafu kuna sehemu zimezungushiwa mawe ukiuliza unaambiwa ni makaburi ya Wakamba waliokuwa wanaishi maeneo hayo. Sijui kama Wachaga wanafanya hivyo kwenye sehemu nyingine za nchi walipohamia.

Nafikiri system ya kihamba imewafanya wachaga waendelee kumiliki ardhi yao kwa kiasi kikubwa. Hii ni kwa sababu watoto wa kike wamekuwa hawapewi kipaumbele katika ugawaji wa vihamba. Kama wangekuwa wanapewa inawezekana uchagani kungekuwa na watu wa makabila mengine hasa wale walioa uchagani. Nadhani kwanza inabidi ubaguzi wa aina hii uondolewe. Hivyo, lingekuwa jambo la mbolea kama huyo Askofu angeongelea hili suala.

Hata hivyo, upungufu wa ardhi uchagani sidhani kama unasababishwa na wachaga kuzikia kwenye vihamba vyao. Zipo sababu mbalimbali zikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watu, uhamiaji, utamaduni wa kuhodhi ardhi kubwa, nk. Hivyo basi hata kama kungekuwa na sehemu maalumu ya kuzikia bado upungufu wa ardhi ungekuwepo. Hata hivyo ingekuwa useless kwa mchaga aliyeko Dar kwenda kuzikia makaburi ya Moshi badala ya kuzikia kwenye makaburi ya Kinondoni.

Nonetheless, urbanization inaongezeka ambapo ardhi itakuwa more commercial.
 
yani bora umewapa warning maana wamezidi kila deci
wanakwenda kuhesabiwa utafikiri wanaota manyoya
mapya jamani hhaaa! bora ya sie wanalumango


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao, amekosoa utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambao wengi ni Wachaga, wa kuzikana nyumbani (vihamba) na kusema ni utaratibu wa hovyo. Akifafanua kauli hiyo juzi, Askofu huyo alielezea hofu ya kupotea kwa mashamba ya kahawa mkoani humo, kutokana na utamaduni uliosababisha ongezeko la makaburi kwenye mashamba hayo.

“Naomba Serikali mkoani, iweke utaratibu wa kudumu wa maeneo ya maziko badala ya watu kuzikwa ovyo majumbani… ardhi hii ni ndogo, lakini bado tunaimega kwa kuzika, hapo baadaye hatutakuwa na mashamba ya mibuni,” alisema.

Askofu huyo aliiomba Serikali kuelimisha wakazi hao, ili wabadili mfumo wa kugeuza makazi na mashamba yao sehemu ya kuzika ndugu zao, ili kutotumia vibaya ardhi ndogo iliyopo. Alisema hayo wakati wa harambee ya kuchangia Sh milioni 95 za ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Nanjara wilayani Rombo na kusisitiza umuhimu wa Serikali kuweka utaratibu wa maeneo ya kudumu ya maziko.

Kwa mujibu wa Askofu Shao, licha ya hatari ya kupunguza mashamba ya kahawa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa mkoa, lakini pia utaratibu wa sasa wa kuzikana majumbani, utaathiri vizazi vijavyo na kusababisha vikose maeneo ya ujenzi wa makazi.

Alisema kutokana na mkoa kubuni miradi mikubwa ukiwamo wa soko la biashara la kimataifa la Lokolova na mji wa kitalii wilayani Siha, ni matumaini ya Kanisa kuwa pia Serikali itaandaa utaratibu wa kila wilaya, kutenga maeneo ya maziko ya jumuiya. Dk Shao alisema iwapo mpango wa kila wilaya kutenga maeneo hayo utashindikana, Kanisa litakuwa tayari kununua ardhi kwa ajili ya waumini wake.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, alisema amelisikia na atalifikisha kwa Kamati ya Ushauri ya Mkoa ili ufumbuzi upatikane.

Source: Habarileo
 
yani bora umewapa warning maana wamezidi kila deci wanakwenda kuhesabiwa utafikiri wanaota manyoya mapya jamani hhaaa! bora ya sie wanalumango

Wanasema mtu kwao, wewe kwenu wapi? Hata wasipoenda bado watalalamikiwa tuu kwa kukimbia vihamba vyao hasa pale panapokuwa na mchakato fulani hivi (kama utakuwa umenielewa). lol

kijasti.jpg
 
umenichekeshaje besti yaani hiyo picha uliyonitumia
mi huku niko hoi kabisa nyumbani kwetu ni kwenu kwani
wewe hujui bestito?
wanasema mtu kwao, wewe kwenu wapi? Hata wasipoenda bado watalalamikiwa tuu kwa kukimbia vihamba vyao hasa pale panapokuwa na mchakato fulani hivi (kama utakuwa umenielewa). Lol

kijasti.jpg
 
umenichekeshaje besti yaani hiyo picha uliyonitumia mi huku niko hoi kabisa nyumbani kwetu ni kwenu kwani wewe hujui bestito?

Jokingly, nasikia kwenu mwanaume akitaka kuoa haulizwi kama ana kabati la mbeo kama kule uchagani. Baada ya kudadisi sana nikakuta kuwa kwenu mna asili ya kutumia hicho kifaa hapo chini katika matumizi ya vyombo vya nyumbani.

Hiki ni sawa na kipozeo cha maji na ndiyo maana wanaume wengi wa kichaga wameacha kuoa uchagani na kuja huko kwenu. Achana kabisa na maji ya mtungi. Kunywa maji ya mtungi. lol.

kyela.jpg


On serious note, maggid alishawahi kuandika baada ya kumsikia mchungaji wa kanisa akiwatamkia waumini wake kuwa "Angalieni upepo, nguvu ya upepo. Duniani upepo unaweza kutingisha miti, ukavunja matawi na hata ukaangusha miti….!" Nae Sugu alishaenda mbali na kuliambia bunge letu tukufu kuwa huu si upepo bali ni kimbunga na kama kitashindwa kuangusha nyumba lazima kitandoka na paa. Sugu ana bahati sana aliyasema haya kipindi kile maana angeyasema sasa lazima angepigwa tuu. Si uliona walivyomfanyia jana? Maana tumechoka sasa!

Sasa basi baada ya kumsikiliza huyo mchungaji wa kanisa Maggid alitafakari na mwisho kuamua kuandika kuwa "...nyumba ya kijijini haijakamilika bila kuwa na mtungi. ... Hakuna tu siri ya mtungi, kuna falsafa ya mtungi pia. Ninapoingia kwenye nyumba kijijini huangalia kwanza ulipo mtungi. Kwenye mtungi yawezekana ndimo yalimo maji ya kunywa.

Na ukiinamia mtungi wa maji, usiaangalie sana, chota maji yako, kunywa. Lakini, mtungi pia hutumika kuhifadhia vyakula; iwe unga au maharage. Mara nyingi mtungi huwekwa kwenye kona ya chumba. Na mtungi ukikaa sana, basi, siku ukiinuliwa, hutaacha alama.

Na unafanyaje basi mtungi wa maji unapoonyesha kuwa na nyufa, kuwa maji yameanza kuvuja? Kuna mawili; la kwanza si la busara sana. Ni jawabu la muda mfupi, la pili ni la busara zaidi, ni suluhisho la muda mrefu. .... mtungi wenye nyufa unaweza kuzibwa kwa kusaga vipande vya mtungi wa zamani, kisha ukachanganya na nta. Baada ya hapo utasiliba kwenye nyufa za mtungi. Hiyo ni njia ya kwanza, ni suluhisho la muda mfupi.

Maana, tabu inakuja, siku mtungi utakapohitajika kuchemshia ‘komba'-..... Basi, kwenye moto mkali wa kuni nyufa zile, pamoja na kusilibwa na nta, hazitahimili nguvu ya moto. Mtungi utamegeka vipande vipande. ' Komba', ama togwa la pombe litamwagika.

Naam, dawa ya mtungi wenye nyufa si kusiliba kwa nta, ni kufinyanga mtungi mpya, basi. Na jamii yetu imekuwa ni kama ya ‘Super-glo', ile gundi inayoaminiwa inaweza kusiliba, ama kuunga chochote kile. Kila jambo tunakimbilia kuitafuta ' Super-glo'. Kama nta, Super-glo nayo haihimili kwa muda mrefu joto la moto, au hata la jua.

Wanadamu tuwe na ujasiri wa kuyatambua matatizo yetu kama yalivyo. Tusiwe wepesi wa kukimbilia ' kusiliba' kwa nta ua super-glo. Mengine ni ya kuyafanyia mabadiliko ya jumla."

Neno La Leo kutoka kwa Maggid Mjengwa : Maisha Yetu Na Falsafa Ya Mtungi.. | FULL SHANGWE BLOG

Suluhisho alilotoa Askofu linaweza kuwa ni "super-glo" maana kuna makabila mengine hawaziki kwenye "vihamba" lakini kuna uhaba wa ardhi. Pia hiyo ardhi haijaweza kutumika kiabiashara kwa manufaa ya wakazi wa pale zaidi ya "viasaka" aka wageni kuja kuchimba madini pale na kuacha mashimo tuu, huku wakiawambia wakazi wahame maeneo yao haraka kwa sababu madini hayo ya dhahabu yana madhara makubwa sana kwa binadamu kama kupata kansa ya ngozi na wendawazimu.

Well, naona usije ukakatika "stimu" hivi hivi na kuishia kuvunja kile na chungu na kukiziba kwa "super-glo"

 
Last edited by a moderator:
Mwambieni aje kufanya kazi azania front sikuzote anangangania hukokijijini kuna nini na kwa nini tusiende uko siku za mwisho kama yeye akiwa hai ataki kuja mjini??
 
jamani EMT umeamua kuniandikia waraka mrefu kiasi hicho mpaka kusoma nashindwa!
haa!!! kwanini wanifanyia hivyo mtoto wa mwanamke mwenzio?
 
Last edited by a moderator:

yaani migomba ibaki bila misalaba?
mi nizikwe migombani tu
wanangu wasije pata tabu ya kuhamisha kaburi khaaaa!!
 
Askofu naona anafanya kampeni ya kutufanya tuuze mashamba yetu, maana vihamba vinafanya maeneo kutouzwa ovyo.
Ushauri wake ni mzuri, lkn utakua mzuri zaidi akianzia na vihamba vya pale kwao halafu na sisi tutaiga mfano
 
Wazee wa kichaga waliwaza mbali mno. Wakijua wakiruhusu watu wafanye wanayotaka moshi hadi migombani ardhi itaisha.
Hapo isihusishwe na chochote mana wachaga kuzikana kwao hakuna gharama zinazotoka serikalini.
 
Back
Top Bottom