Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao, amekosoa utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambao wengi ni Wachaga, wa kuzikana nyumbani (vihamba) na kusema ni utaratibu wa hovyo. Akifafanua kauli hiyo juzi, Askofu huyo alielezea hofu ya kupotea kwa mashamba ya kahawa mkoani humo, kutokana na utamaduni uliosababisha ongezeko la makaburi kwenye mashamba hayo.

“Naomba Serikali mkoani, iweke utaratibu wa kudumu wa maeneo ya maziko badala ya watu kuzikwa ovyo majumbani… ardhi hii ni ndogo, lakini bado tunaimega kwa kuzika, hapo baadaye hatutakuwa na mashamba ya mibuni,” alisema.

Askofu huyo aliiomba Serikali kuelimisha wakazi hao, ili wabadili mfumo wa kugeuza makazi na mashamba yao sehemu ya kuzika ndugu zao, ili kutotumia vibaya ardhi ndogo iliyopo. Alisema hayo wakati wa harambee ya kuchangia Sh milioni 95 za ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Nanjara wilayani Rombo na kusisitiza umuhimu wa Serikali kuweka utaratibu wa maeneo ya kudumu ya maziko.

Kwa mujibu wa Askofu Shao, licha ya hatari ya kupunguza mashamba ya kahawa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa mkoa, lakini pia utaratibu wa sasa wa kuzikana majumbani, utaathiri vizazi vijavyo na kusababisha vikose maeneo ya ujenzi wa makazi.

Alisema kutokana na mkoa kubuni miradi mikubwa ukiwamo wa soko la biashara la kimataifa la Lokolova na mji wa kitalii wilayani Siha, ni matumaini ya Kanisa kuwa pia Serikali itaandaa utaratibu wa kila wilaya, kutenga maeneo ya maziko ya jumuiya. Dk Shao alisema iwapo mpango wa kila wilaya kutenga maeneo hayo utashindikana, Kanisa litakuwa tayari kununua ardhi kwa ajili ya waumini wake.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, alisema amelisikia na atalifikisha kwa Kamati ya Ushauri ya Mkoa ili ufumbuzi upatikane.

Source: Habarileo
 
kereeeuuwih! Mkirua na Nicas Mtei hebu kujeni pande hizi waume zangu!
sasa zile vihamba na boma zikae bila misalaba na yale mawe kweli itakuwa ni mgombani au dasalama?

EMT kwanza bora umesema mimi kila nikiwaza the fact kuwa nikifa nitazikwa mgombani inaniuma uue!yani kweli si ndo mwisho wa ndugu zangu k kuona kaburi langu!?watakfunga safari kweli all the way kutoka songea waje waone kaburi rombo!
chaaaaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
Kwani ukichota sukari kutoka kwenye gunia kwa kijiko kila.unapohitaji au uchukue kilo mbili kutoka same gunia halafu utumiie ikiisha ndo uchote tena kwenye gunia tofauti ya kuisha hiyo sukari kwa njia hizi mbili ni nini???!!

Kama hajaweka ratio ya arrable versus un arrable land ndani ya mkoa husika kuzingatia mazao yanayostawi humo then aliamua tu kusema ili ratiba itimie naye waziri eti nimelipokea ntalifanyia kazi!!!!!!!

Kama ni kuokoa ardhi basi angependekeza kuchoma maiti hii ndio haina mjadala maana ni jivu kumwaga mtoni kwisha habari!!!!!!!
 
Ukichukulia kwamba eneo la kaburi linachuliwa forever katika maana kwamba mahali lilipo hakuna mmea wala shughuli yeyote inaweza kuchukua nafasi. Nadhani haihitaji uwe mkali wa hesabu za Kalukulasi zile hesabu za majoka kujua nini kitawapata ndani ya miaka 30.
Kama kila kaburi linachukua nafasi ya mita 1.25 x 2.25=2.8125M^2 ni wazi kwamba wakizikwa wanafamilia 100 tu ni sawa na 2812.5squre meter kiamba cha ekari moja kitakuwa kiunga cha makaburi, ukizingatia kwamba kuna nafasi ya kutosha kati ya kaburi na kaburi. Kwa lugha nyingine Wachagga wataishi maeneo mengine ya Tanzania lakini eneo kuzunguka mlima Kilimanjaro litakuwa ni CEMETRY.
Pengine si mbaya kubadiri namna ya kuzika na kuacha kuchoma mwilli wa marehemu kisha kuhifadhi jivu kwenye mtungi.

Mimi kosa na Mungu kosa.
 
Ukichukulia kwamba eneo la kaburi linachuliwa forever atika maana kwamba mahali lilipo hakun mme wala shughuli yeyote inaweza kuchukua nafasi. Nadhani haihitaji uwe makali wa Kalukulasi zie hesabu za majoka.
Kma kila kaburi linachukua nafasi ya mita 1.25 x 2.25=2.8125 ni wazi kwamba wakizikwa wanafamilia 100 tu ni sawa ma 2812.5squre meter kiamba cha ekari moja kitakuwa kiunga cha makaburi, ukizingatia kwamba kuna nafasi ya kutosha kati ya kaburi na kaburi. Kwa lugha nyingine Wachagga wataishi maeneo mengine ya Tanzania lakini eneo kuzunguka mlima Kilimanjaro litakuwa ni CEMETRY.

Kwa hiyo likitengwa eneo maalum ardhi inakuwa wameileta kutoka sayari nyingine????!!!
Kwa hesabu zako ili ndoto itimie then inabidi wakazikwe Ungujaaaaaa au Rwanda
 
Wazo lake ni zuri ila kama anatenga eneo lingine bado itakua sio suluhisho.
Nafikiri tuungane na wahindi tuwe tunachoma moto tu ili kusave kile kihamba cha pale mamsera kisije kikajaa ni shida
nafikiri suala la kuzikana liangaliwe upya badala ya kuchimba mashimo migombani
 
Mila nyingi za wachaga kama kuzika mashambani mwao, kurudi kwao mara kwa mara hasa x-mass, kujali elimu na kufanya kazi kwa bidii ni baadhi tu ya sababu zinazowafanya wawe na maendeleo! Sasa huyu askofu ana lake jambo!
 
kereeeuuwih! Mkirua na Nicas Mtei hebu kujeni pande hizi waume zangu!
sasa zile vihamba na boma zikae bila misalaba na yale mawe kweli itakuwa ni mgombani au dasalama?

@emt kwanza bora umesema mimi kila nikiwaza the fact kuwa nikifa nitazikwa mgombani inaniuma uue!yani kweli si ndo mwisho wa ndugu zangu k kuona kaburi langu!?watakfunga safari kweli all the way kutoka songea waje waone kaburi rombo!
chaaaaaaaa!

Shem, to be objective hili wazo ni zuri na linaelekea kuchelewa... Nashauri maaskofu wengine akiwemo askofu wangu Isaack Amani wa RC waone hiliwazo kuwa la busara na kulifanyia kazi ipasavyo kwani sio kukosa mashamba tu bali hata thamani ya shamba likishakuwa na kaburi inashuka...huku tuendako tunatakiwa tutumie mashamba (vihamba ) kama collateral tuweze kupata mikopo nk...ukishaweka kaburi huwezi tena kulitumia kwa madhumuni hayo....so Naunga mkono hoja asilimia mia!

HUREEEEEEEEEH!
ntazikwa songeaaaaa!
🙂
 
akili za kushikuwa, angewaambia wawe wanachoma moto maiti ningemwelewa hata hivyo tanzania hatuba uhaba wa aridhi hata kidogo leo hii kunasehemu heka moja 50000 wakati kuna watu anaingia bar anateketeza na zaidi ndani ya siku moja..
 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk Martin Shao, amekosoa utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, ambao wengi ni Wachaga, wa kuzikana nyumbani (vihamba) na kusema ni utaratibu wa hovyo. Akifafanua kauli hiyo juzi, Askofu huyo alielezea hofu ya kupotea kwa mashamba ya kahawa mkoani humo, kutokana na utamaduni uliosababisha ongezeko la makaburi kwenye mashamba hayo.

"Naomba Serikali mkoani, iweke utaratibu wa kudumu wa maeneo ya maziko badala ya watu kuzikwa ovyo majumbani… ardhi hii ni ndogo, lakini bado tunaimega kwa kuzika, hapo baadaye hatutakuwa na mashamba ya mibuni," alisema.

Askofu huyo aliiomba Serikali kuelimisha wakazi hao, ili wabadili mfumo wa kugeuza makazi na mashamba yao sehemu ya kuzika ndugu zao, ili kutotumia vibaya ardhi ndogo iliyopo. Alisema hayo wakati wa harambee ya kuchangia Sh milioni 95 za ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Nanjara wilayani Rombo na kusisitiza umuhimu wa Serikali kuweka utaratibu wa maeneo ya kudumu ya maziko.

Kwa mujibu wa Askofu Shao, licha ya hatari ya kupunguza mashamba ya kahawa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa mkoa, lakini pia utaratibu wa sasa wa kuzikana majumbani, utaathiri vizazi vijavyo na kusababisha vikose maeneo ya ujenzi wa makazi.

Alisema kutokana na mkoa kubuni miradi mikubwa ukiwamo wa soko la biashara la kimataifa la Lokolova na mji wa kitalii wilayani Siha, ni matumaini ya Kanisa kuwa pia Serikali itaandaa utaratibu wa kila wilaya, kutenga maeneo ya maziko ya jumuiya. Dk Shao alisema iwapo mpango wa kila wilaya kutenga maeneo hayo utashindikana, Kanisa litakuwa tayari kununua ardhi kwa ajili ya waumini wake.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, alisema amelisikia na atalifikisha kwa Kamati ya Ushauri ya Mkoa ili ufumbuzi upatikane.

Source: Habarileo

Nikifa ningependa nikazikwe kwetu kibosho singa, kwenye shamba nililoachiwa na babu! nyuma ya boma la ng'ombe pale,
 
Kwa kuwa Askofu ni Mchaga acha awashauri wachaga wenzake...sisi wengine tuwe wasomaji tu!
 
EMT hata mimi nakubaliana na baba Askofu, maana sioni mantiki ya mtu kumzikia ndugu nyumbani badala ya kwenye makabuli achilia mbali suala la matumizi mabaya ya ardhi. Ukweli ni kwamba sioni raha yeyote na wala sioni faida yeyote ile (ukiachia suala la kuenzi/kumbukumbu) ya kuweka kaburi ndani ya eneo la makazi ya kuishi maana kwa kufanya hivyo ni kuongeza simanzi kila unapofika nyumbani na pia kuwaumiza wenye mioyo laini kila wanapokuja kukutembelea na kukuta makuburi nyumbani.

Tunaweza kuwaenzi wapendwa wetu kwa kuwatengea eneo maalum na kuandaa siku maalum za kwenda kuyatembelea makaburi hayo na kuwafanyia sala na dua kulingana na imani na tamaduni za watu mbali mbali. Ukweli ni kuwa siungi mkono suala la kuwazikia watu majumbani na kuwafanya mliobaki muwe mnaishi na makaburi ndani ya makazi yenu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Asante kwa ushauri suala la kuzikana halihusiani na rcc ya mkoa ni.letu binafsi wachagga
 
Back
Top Bottom