Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 418
- 974
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa unaandaa utaratibu mpya wa kuwapanga na kuwatambua wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo kwa kuzingatia ukubwa na aina ya biashara wanazofanya.
Alisema hatua hiyo inalenga kuondoa mkanganyiko uliopo katika eneo hilo, ambako wafanyabiashara wadogo na wakubwa wamekuwa wakifanya biashara katika maeneo yanayofanana, hali inayosababisha changamoto katika usimamizi wa shughuli za kibiashara.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari, Chalamila alisema Kariakoo ni miongoni mwa maeneo muhimu kwa shughuli za kiuchumi na mapato ya mkoa, hivyo linahitaji utaratibu maalumu wa kupanga wafanyabiashara na kutambua maeneo wanayopaswa kufanyia biashara.
“Kariakoo tunapatumia kama sehemu kubwa sana pia ya mapato ya mkoa wetu. Lakini kwa bahati mbaya sana Kariakoo hapo tumechanganya wafanyabiashara wadogo na wafanyabiashara wakubwa,” alisema.