Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

Askofu: Wachaga acheni kuzikana majumbani

Mawazo mazuri sana japo naweza kusema amechelewa kuyatoa. uchaggani kashamba kamoja kana makaburi zaidi ya sita na kila moja linajengewa kama kanyumba kakuishi mtu.
 
Makaburi ni nyumba za ndugu waliotutangulia,na ndugu hukaa karibu daima.hili ni swala la utamaduni,watoto watapata vihamba mijini,kwenye plot zilizopimwa.kwa kizazi hiki wakiacha kuzika mgombani,wengi watakua hawapeleki miguu kule,maana shida/misiba huunganisha watu. . . .hasa watoto waliokulia mjini na hawajui ndugu zao. . . .hii kitu idumishwe cc: Mamndenyi
 
Last edited by a moderator:
Askofu kaona mbali, he is right

nyie kurupukeni wakati uchagani ujawai kuishi.....unapoenda kuomba kibali cha kuzika kijiji na kusema unataka kuzika ktk shamba lako lazima waje kupima ukubwa wa eneo la familia wakiridhika nalo unapewa go ahead ....kama mimi ninashamba la urithi heka 5 lipo machame kijijin unategemea nilifanye la maonyesho au niuze kwa vyasaka akuna kitu kama iyo arrifu ...bora niwe mbolea ya migomba watoto na jamaa wale kuliko kuchomwa na jua au kaburi langu kuwa kitanda cha makahaba
 
Uttaratibu mzuri wa kuzikana wala sio wa makaburi au kuchoma, ni bora ingetengwa kaburi moja kubwa kwa kila sehem husika, marehem wote wakawa wanapumzishwa humo pasipo kuangalia dini, kabila wala nini.

hahaha very fun
 
".................hatari ya kupunguza mashamba ya kahawa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi wa mkoa, lakini pia utaratibu wa sasa wa kuzikana majumbani, utaathiri vizazi vijavyo na kusababisha vikose maeneo ya ujenzi wa makazi".

point ya Askofu ni kuisha kwa ardhi ktk maeneo ya makazi na mashamba, He has a point tatizo ni kasumba yetu wabongo.
 
mwenzangu sijui wewe ni wa moshi ipi, moshi niliyopo mie sijaona uhaba unaousemea, hiyo blue kwanza wanaoamua kuzikia kwenye mashamba yao wanazika kiholela? ohh plz.

Nyamayao, mie Mkirua nipo Kirua Vunjo Moshi....sijui wewe uko wapi?? Huko KV tuna uhaba mkubwa wa ardhi..

..Nikupe mfano....babu alikuwa na Heka 8 akagawa zote kwa watoto wake 4 wa kiume (as usual) sasa baba yetu na viheka vyake 2 kazaa midume 7 naye amekata viwanja kwa kila mmoja unaweza kufanya hesabu na kuona tunakoelekea...huu ni mfano tu lakini unawakilisha uhalisia wa kinachoendelea huko....unadhani kwanini wachagga tunasifika kwa kuhamisha mipaka kwa minaajili ya kuongeza ukubwa wa shamba? Au unadhani kwanini tunathamini sana ardhi?...

Nakumbuka miaka fulani iliyopita akifa mtu mahali wanaobakia ni kucharangana mapanga kwa sana kisa vihamba....angalau baada ya kuhamia maeneo mengine km morogoro, tanga nk na kujiestablish wachagga wamekuwa wastaarabu na ukimuona nayegombania shamba la kijijini hadi kuumizana na ndg yake basi unajua huyuana ushamba fulani...

Hoja yangu ulipoweka blue ni kwamba nakubaliana na utamaduni wa kuzikana kwenye vijiji vyetu ila kijiji husika kitenge eneo maalum kwa ajili hiyo na sio kila mtu anazika kwenye shamba lake. Ni hapo tu na hii iwe kwa nchi nzima sio moshi tu. Mimi ni "muumini" wa mipango tena inayolenga vizazi vijavyo. Leo hii DSM tunalaumu walioipangilia kwa kuto kuona mbali hatimaye mji umekuwa kero na asilimia kubwa ya maeneo hayajapangiliwa lkn tunakuwa mstari wa mbele ku encourage watu kufanya mambo kienyeji. Hii sio sawa hata kidogo.

Mimi siyo mchaga. Lakini, naweza nikatumia uzoefu wa makabila mengine ambapo kuzika mtu kwenye eneo/shamba linalomilikiwa na familia, utumika kama njia ya kuepusha uvamizi wa eneo hilo kutoka kwa ndugu wengine ama watu wengine. Yaani utumika kama njia ya kuhakikisha umiliki endelevu wa eneo husika.

Kwa mfano, baba anaamua kuzikwa kwenye eneo lake kuepusha watoto wake kuporwa eneo hilo na ndugu wa baba huyo, hususani kama watoto bado ni wadogo. Vivyo hivyo yaweza kuwa kuepusha mkewe kuporwa ardhi n.k.

Sasa, pengine hiyo ndiyo dhamira ya wachaga. Ukizingatia na uhaba mkubwa wa ardhi katika maeneo yao! Ila wachaga ndiyo wanafahamu sababu za kuamua kuzikwa huko.

Wala hujakosea hii ni sababu mojawapo kati ya nyingi.....
je, unaonaje tukahamia kwenye utaratibu wa kisheria maeneo yakapimwa na watu wakatumia hati kuyalinda badala ya kutumia makaburi?

Askofu anasahau wao walitoa kauli ya wachungaji wazikwe kanisani huu ndo ujinga ila nyumbani kila familia ina eneo lake la kuzikia shinda iko wapi kwani uko anakotaka wazikiwe ni hewani.
 
Interesting indeed. Kweli kwa sasa vihamba bado havijawa commercialised.

Wachaga wengi hawauzi vihamba vyao kwa watu ambao siyo wachaga.

Sidhani hata kama mchaga wa Kibosho anaweza kumwuzia mchaga wa Kirua sehemu ya kihamba chake.

Hii imechangia kwa wasio wachaga kushindwa kumiliki ardhi maeneo ya uchagani japokuwa wachaga wanamiliki ardhi mpaka Marekani.

Pia vihamba badala ya kumilikiwa customarily inabidi visajiliwe na kupewa vyeti?

Absolutely mkuu,
Yaani ulichokiandika ni kweli kabisa...
ipo miradi kwenye badhi ya vijiji hapa Tanzania watu wameanza kutumia
mashamba yao ya vijijini kama dhamana za benki. Hii ni njia mojawapo itakayotutoa
watanzania kwenye umaskini, ukulima wa hand to mouth angalau mkulima mmoja aweze kulisha
watu kadha. Hii inawezekana kwa kutumia vifaa vya kisasa ambavyo ni ghali.

Tufikie mahali tuone kuwa kuuza mahindi Kenya ni fursa na tuichangamkie badala ya kusaka wanaofanya hivyo na kutaifisha magari yao! Sasa tunapoendelea kupamba rasilimali zetu chache tulizo nazo kwa makaburi na kuziondolea kabisa thamani hiyo, ukizingatia kahawa ndio imekwishaondoka kwakweli tunajimaliza wenyewe.
Baba Askofu kaona mbali ambapo wengine wataona watakapokuwa wamechelewa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Moshi hakuna makaburini wala porini (kila mtu atazikwa kwake). Hata serekali inajua fika kumfidia mtu kiwanja chake kupisha mradi ni ndoto kwa moshi let alone kutenga eneo kubwa (mbona watu wa klm wangefurahi ofa kama hiyo). Maeneo mengi moshi vijijini yametangazwa kuwa manispaa na hairuhusiwi kufuga tena n.k ila hakuna miradi yoyote ya hospital wala shule ukiuliza nini na shida ni kwamba watu hawataki kuachia ardhi kupisha miradi bcoz ardhi ya urithi ni sacred huku na suala la ardhi ni gumu sana. Wachaga wengi wanawaza watazikwaje. na tajiri kuzikwa ktk public cemetery ni aibu kubwa huku.
 
Wala hujakosea hii ni sababu mojawapo kati ya nyingi.....
je, unaonaje tukahamia kwenye utaratibu wa kisheria maeneo yakapimwa na watu wakatumia hati kuyalinda badala ya kutumia makaburi?

Kweli. Hii nayo yaweza saidia sana. Sasa kuna mpango wa MKURABITA, ambapo wakazi wa vijijini wanamilikishwa ardhi kwa kupewa hatimiliki za kimila. Sasa, sifahamu kama mpango huo umeshafika huko.
 
nyie kurupukeni wakati uchagani ujawai kuishi.....unapoenda kuomba kibali cha kuzika kijiji na kusema unataka kuzika ktk shamba lako lazima waje kupima ukubwa wa eneo la familia wakiridhika nalo unapewa go ahead ....kama mimi ninashamba la urithi heka 5 lipo machame kijijin unategemea nilifanye la maonyesho au niuze kwa vyasaka akuna kitu kama iyo arrifu ...bora niwe mbolea ya migomba watoto na jamaa wale kuliko kuchomwa na jua au kaburi langu kuwa kitanda cha makahaba
halafu unataka miji yetu ipangwe kisasa
 
JAMANI watu wengne wanakosa lakusema' kiruu
 
Nyamayao, mie Mkirua nipo Kirua Vunjo Moshi....sijui wewe uko wapi?? Huko KV tuna uhaba mkubwa wa ardhi..

..Nikupe mfano....babu alikuwa na Heka 8 akagawa zote kwa watoto wake 4 wa kiume (as usual) sasa baba yetu na viheka vyake 2 kazaa midume 7 naye amekata viwanja kwa kila mmoja unaweza kufanya hesabu na kuona tunakoelekea...huu ni mfano tu lakini unawakilisha uhalisia wa kinachoendelea huko....unadhani kwanini wachagga tunasifika kwa kuhamisha mipaka kwa minaajili ya kuongeza ukubwa wa shamba? Au unadhani kwanini tunathamini sana ardhi?...

Nakumbuka miaka fulani iliyopita akifa mtu mahali wanaobakia ni kucharangana mapanga kwa sana kisa vihamba....angalau baada ya kuhamia maeneo mengine km morogoro, tanga nk na kujiestablish wachagga wamekuwa wastaarabu na ukimuona nayegombania shamba la kijijini hadi kuumizana na ndg yake basi unajua huyuana ushamba fulani...

Hoja yangu ulipoweka blue ni kwamba nakubaliana na utamaduni wa kuzikana kwenye vijiji vyetu ila kijiji husika kitenge eneo maalum kwa ajili hiyo na sio kila mtu anazika kwenye shamba lake. Ni hapo tu na hii iwe kwa nchi nzima sio moshi tu. Mimi ni "muumini" wa mipango tena inayolenga vizazi vijavyo. Leo hii DSM tunalaumu walioipangilia kwa kuto kuona mbali hatimaye mji umekuwa kero na asilimia kubwa ya maeneo hayajapangiliwa lkn tunakuwa mstari wa mbele ku encourage watu kufanya mambo kienyeji. Hii sio sawa hata kidogo.

mie mmarangu, hapo kwenye mfano wa baba huoni kwamba babu yeye aliacha kiasi kinachoeleweka ishu ikaja kwa baba? kwa nyie coz mna sehemu ndogo hata mie ningekushauri msizikie hiyo sehemu, kwetu sisi kuna eneo kubwa, kuna sehemu special imepangwa kwa maziko,hatuziki kiholela, mfano mjomba afiwe akazikie shambani kwake, hapana, atazikia kwenye eneo lililotengwa tangu awali, na ipo ya kutosha na ukizingatia wengine hatudhani kama tutazikiwa marangu,na bado kuna eneo la vihamba tulivyoridhishwa na wazazi wetu, nadhani eneo likijaa ndio watafikiria cha kufanya! kwasasa wacha tuendelee kuzikana marangu.
 
Hata mimi nashindwa kukuelewa kwani hili jambo liko wazi na sioni mahali pasipo eleweka.

Ndio maana nashindwa kukuelewa unapounga mkono hoja ya namna hii!!!!
Watu wanazikana kwenye eneo la familia ambalo wameamua kulitumia kwa sababu hizo wewe unaanzaje kusema hayo maneno au kuna mtu amezikwa kwa watu???!!!

Au makaburi ya jumla watazikwa wima kupunguza ukubwa wa kaburi???!!!!
 
kereeeuuwih! Mkirua na Nicas Mtei hebu kujeni pande hizi waume zangu!
sasa zile vihamba na boma zikae bila misalaba na yale mawe kweli itakuwa ni mgombani au dasalama?

Uuuuwiii dadangu barafu nyeupe (Snowhite) mimi kama mchaga wa kirua sitaweza kulikubali hilo aisee acha asili ichukue mkondo wake.Kwanini huyo asikofu ilo shamba analotaka wazikwe wafu asipande migomba na hiyo mibuni anayosema inapotea?Je bado zao la kahawa ni tegemeo kwa mkoa wa KLM tena au naye kaamua kuwa mwana si hasa!

@emt kwanza bora umesema mimi kila nikiwaza the fact kuwa nikifa nitazikwa mgombani inaniuma uue!yani kweli si ndo mwisho wa ndugu zangu k kuona kaburi langu!?watakfunga safari kweli all the way kutoka songea waje waone kaburi rombo!
chaaaaaaaa
 
acha tuwazike ndugu zetu mashambani kwetu, huo ni utaratibu tuliouamua na tukaupenda. kuna maeneo ya wazi mengi sana huko iringa na mbeya tutaenda kuwekeza na pesa tupeleke nyumbani.
ardhi ya kilimanjaro imeshajaa, sio makaburi ila kwa makazi ya watu, huwezi kuifanyia kilimo kwa sasa.
 
Hata mimi nashindwa kukuelewa kwani hili jambo liko wazi na sioni mahali pasipo eleweka.

Land as a property ina aspects za control,access,ownership and benefit na haya yote priority wanapewa wazawa na ndio mgogoro wa kote kwenye rasilimali.

Sasa yeye na wewe hizo aspects mnaziwekaje kwenye hoja yenu???!!!
 
Back
Top Bottom