Askofu wa Katoliki Jimbo la Bukoba atetea uwepo wa kiti cha Rais Kanisani

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Wapendwa, nimeona mjadala juu ya kiti cha Rais na nikaonelea nitoe maelezo kidogo. Kanisa katika protocol zake inatambua na kuwaheshimu viongozi katika hadhi zao mbali mbali.

Hii protocol siyo ya sasa au jana ni ya miaka mingi. Rais ni kiongozi wa nchi hivyo hadhi yake ni hadhi ya nchi siyo yake binafsi.

Kwa sababu ya unyenyekevu wa viongozi wetu, kiti cha Rais kilikuwa kumebanwa kati ya mabenchi amezungukwa na masista na watu wengine. Kikawaida ingebidi sehemu moja ya kanisa benchi ziondolewe na kipangwe kiti chake rasmi na wapambe wake.

Hiyo ndiyo protocol halisi ya Mkuu wa Nchi anayekuja rasmi kwa dhifa ya kitaifa kama Rais wetu alivyokuja kwa kumbukumbu ya kitaifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hiyo si heshima kwake bali kwa nchi. Hewala si utumwa, tukikosa heshima kwa viongozi wetu tutakosa heshima hata nyumbani mwetu.

Tunatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Taifa kuungana nasi katika ibada ya kumwombea Baba wa Taifa. Ni jambo jema sana.

Hata kanisani tunaheshimu siyo mtu binafsi lakini nafasi yake anayoishika. Kwa mfano Kardinali akiwa yeye haongozi ibada hakai pembeni na maaskofu wengine bali anapewa kiti maalumu kwa heshima yake. Unashukuru wat wa Itifaki ya Ikulu waliotuazima viti walau tukatoa heshima hiyo ndogo kwa mgeni wetu maalumu wa siku hiyo.

Ndugu zangu nimeona nitoe maelezo hayo kwa sababu niliona hoja inakua bila kutazama protocol za kanisa na heshima zake. Vile vile hakuna katazo kiti Fulani kisiingie kanisani ndiyo sababu unaona hata viti vya plastic vinavyotumika sehemu nyingine vinawekwa kanisani watu wakiwa wengi.

Nachukua fursa hii kuwashukuru waamini wa Bukoba Kanisa Kuu na parokia Jirani kwa kuungana nasi kwa wingi kumwombea Baba wa taifa. Mungu awabariki.

Askofu Method Kilaini
 
Safiii Sana maana Bavichaaaa na Chadema walikuwa wamebeba Kama ajenda yao baada ya chama Chao kukosa muelekeo na dira na kuishia kupuuzwa na Watanzania.

Nimewaambia humu kuwa Rais wa nchi siyo Sawa na Rais wa Bendi ya Mziki, ulinzi na usalama wa Rais wa nchi Ni kipaombele na muhimu kuliko kitu kingine au mtu mwingine yeyote yule hapa nchini, usalama wa Rais ndio utulivu wa Taifa letu.
 
Safiii Sana maana Bavichaaaa na Chadema walikuwa wamebeba Kama ajenda yao baada ya chama Chao kukosa muelekeo na dira na kuishia kupuuzwa na watanzania, Nimewaambia humu kuwa Rais wa nchi siyo Sawa na Rais wa Bendi ya Mziki, ulinzi na usalama wa Rais wa nchi Ni kipaombele na muhimu kuliko kitu kingine au mtu mwingine yeyote yule hapa nchini, usalama wa Rais ndio utulivu wa Taifa letu
Aibu kwa wana Sacco's wa mtaa wa ufipa
 
Hata nami sikuona sababu ya kulalamikia hilo jambo, japo napingana na sababu alizotoa Askofu jimbo la Bukoba.

Naona angetembea na sababu za kiroho jibu lake lilikuwa jepesi sana, badala ya kuhangaika kutafuta sababu za ulimwengu mpaka akajichanganya.

Chanzo cha haya ni pale maoni yanapotolewa na mwanasiasa, kisha wafuasi wake/chama chake kuyabeba bila kujiuliza kama lililosemwa na kiongozi wao lina mantiki au hapana.

Kwanza, haya mambo ya kupigania vya ulimwengu huu yanatoka kwa mafundisho ya nani? sikumbuki wapi Yesu Kristu kwenye maandiko aliwahi kufundisha hilo jambo.

Zaidi, maandiko yanataka tuheshimu mamlaka zilizo juu yetu, sasa kama mamlaka imeamua kwenda na kiti chake kanisani, mnagoma ili iweje? kufanya hivyo sio kwenda kinyume na maandiko?

Kwa mtazamo wangu, Lema alikosea kwenye hili, nae kwa ushawishi wake, akawaponza wengi walioamua kuhukumu hili jambo bila kutumia fikra zao.
 
Hiyo ndiyo protocol halisi ya Mkuu wa Nchi anayekuja rasmi kwa dhifa ya kitaifa kama Rais wetu
stoner-snoop-dogg.gif
 
Labda tungemuuliza huyo Baba Askofu ni lini alimchagua huyo Kiongozi anayemsema? Nijuavyo mimi Viongozi wa watu huchaguliwa hata Papa mwenyewe hupigiwa kura!
Kwani 2020 hukupiga kura au kusoma hujui je hata picha hukuiona?
 
Kiti cha urais hakipashwi kuletwa kanisani!
Unatetea "utukufu" wa Rais /mwanadamu mbele ya utukufu wa Mungu! Hapa umepotoka kiasi kikubwa. mambo mengine jinyamazie! Umekengeuka!
 

Attachments

  • 1665830591123.jpeg
    1665830591123.jpeg
    244.1 KB · Views: 6
Back
Top Bottom