Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,698
4,693
Naangalia maoni ya wasomaji, na maneno ya rais, ufahamu ni tatizo. Kuna dalili za kushabikia maoni ya Askofu Shoo kama ahueni kufuatia Waraka wa Katoliki kumbe ni uzi ule ule! Katoliki hawakupinga Uwekezaji.

Tatizo ni Mkataba. Askofu Shoo anasema anaunga mkono Uwekezaji. Hajasema anaunga mkono Mkataba! Rais naye anaongeza hakuna wa kutugawa! Nani kawagawa? Sema juu ya MKataba! Kuna kundi linaonekana kujawa furaha ya matumaini ya kuungwa mkonoi na KKKT! Hawajiulizi uwekezaji nani kaukataa?

Nionavyo KKKT na Katoliki wako pamoja. Katoliki wameenda mbali zaidi na kuukosoa mkataba kwa maandishi. Ninayo hisia kwamba siku chache zijazo baada ya rais kuwapisha jukwaa lao, KKKT watakuja na msimamo halisi unaohusu Mkataba.
 
Naangalia maoni ya wasomaji, na maneno ya rais, ufahamu ni tatizo. Kuna dalili za kushabikia maoni ya Askofu Shoo kama ahueni kufuatia Waraka wa Katoliki kumbe ni uzi ule ule! Katoliki hawakupinga Uwekezaji....
Askofu Dk. Shoo kaongea kwa busara sana. Amesema waliishawahi kwenda Ikulu na mapendekezo yao wakiwemo TEC, BAKWATA na wao CCT.

Akasema anaamini walichoshauri kitashughulikiwa na wakiona imeenda tofauti basi wao watatoa Waraka. Hao TEC wamekurupuka!

Binafsi niwashauri TEC. Wawe makini sana na Baba Padre Dk. Kitima. Alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo SAUT wakati nasoma pale 2006 - 2009. Ni mtu wa kukurupuka na kuongea kabla ya kufikiri.

Hata wao Mababa Askofu wanalijua Hilo na wanajua pia ndio sababu ameshindwa kuupata Ubaba Askofu kutokana na hilo. Wawe makini asiwapotoshe!
 
Naangalia maoni ya wasomaji, na maneno ya rais, ufahamu ni tatizo. Kuna dalili za kushabikia maoni ya Askofu Shoo kama ahueni kufuatia Waraka wa Katoliki kumbe ni uzi ule ule! Katoliki hawakupinga Uwekezaji...
Askofu wa kanisa kama KKKT sitegemei akosane na TEC. Ajabu ni wasikilizaji kutotaka kuelewa kwamba huyu ni mtu ambaye ni seasoned. Anaongea kwa niaba ya mamilioni kanisani na hawezi kujisemea.

Anaposema sentensi mbele ya rais, ujue imepangwa vizuri! Anasema Mkataba vijana wetu hawa wa UVCCM wanasema anaunga mkono mama na DP world yake. Hakika naye asipokuwa makini anafarijika na kusema hakuna anayetugawa! Nani kasema tugawane maoni?
 
Askofu Dk. Shoo kaongea kwa busara sana. Amesema waliishawahi kwenda Ikulu na mapendekezo yao wakiwemo TEC, BAKWATA na wao CCT....
Swali dogo tu! Wanaposema wanakaribisha maoni, wakati CCM inaendelea na kampeni za kusema Mkataba uko sahihi, Spika anasema mkataba uko sawa tu!

Mahakama inasema una tatizo lakini uendelee tu! Je, kwa mtu makini unaweza kweli ukaelewa kwamba rais ana busara sana kuliko wote hawa ambao wako karibu naye kuliko hata viongozi wa dini na madhehebu?

Hizi nchi zetu ukiweka sana busara, unajikuta unadhalilishwa. Kumbuka mzee Warioba alivyodhalilishwa na tume yake ya Katiba utadhani amejipa kazi hiyo.

Mvungi akauwawa! Rais akiwepo na tena akiwa ameshawaunga mkono. wanapokonywa magari wakiwa Arusha. Nasikia wengine walirudi kwa mabasi!
 
Swali dogo tu! Wanaposema wanakaribisha maoni, wakati CCM inaendelea na kampeni za kusema Mkataba uko sahihi, Spika anasema mkataba uko sawa tu! Mahakama inasema una tatizo lakini uendelee tu...
Kwani ni lazima Kila mtu atoe maoni ya kukosoa? Wewe wa wapi? Kwani CCM au Spika kusema Mkataba ni mzuri sio maoni? Au wewe unafikiri maoni ni kupinga tu na kukosoa? Wa wapi weye?
 
Naangalia maoni ya wasomaji, na maneno ya rais, ufahamu ni tatizo. Kuna dalili za kushabikia maoni ya Askofu Shoo kama ahueni kufuatia Waraka wa Katoliki kumbe ni uzi ule ule! Katoliki hawakupinga Uwekezaji.

Tatizo ni Mkataba. Askofu Shoo anasema anaunga mkono Uwekezaji. Hajasema anaunga mkono Mkataba! Rais naye anaongeza hakuna wa kutugawa! Nani kawagawa? Sema juu ya MKataba! Kuna kundi linaonekana kujawa furaha ya matumaini ya kuungwa mkonoi na KKKT! Hawajiulizi uwekezaji nani kaukataa?

Nionavyo KKKT na Katoliki wako pamoja. Katoliki wameenda mbali zaidi na kuukosoa mkataba kwa maandishi. Ninayo hisia kwamba siku chache zijazo baada ya rais kuwapisha jukwaa lao, KKT watakuja na msimamo halisi unaohusu Mkataba.
Na Rais kasema Changamoto zitafanyiwa kazi
---
"Serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zote zinazojitokeza katika ushirikiano wetu chini ya sera ya PPP [Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi] ili kwa pamoja tuendelee kumhudumia huyu mwananchi. Hakuna jambo lisilokuwa na changamoto lakini zinapojitokeza tunazifanyia kazi kwa pamoja ziondoke" – Rais Samia Suluhu Hassan
 
Kwani ni lazima Kila mtu atoe maoni ya kukosoa? Wewe wa wapi? Kwani CCM au Spika kusema Mkataba ni mzuri sio maoni? Au wewe unafikiri maoni ni kupinga tu na kukosoa? Wa wapi weye?
Tatizo sasa umeanza kuandika kama kijana wa form 2! Hujui hata nafasi ya Spika na CCM kwenye maamuzi ya rais. Hujui hata historia ya maaamuzi mazito kama haya hapa nchini huendaje.
 
Askofu Dk. Shoo kaongea kwa busara sana. Amesema waliishawahi kwenda Ikulu na mapendekezo yao wakiwemo TEC, BAKWATA na wao CCT. Akasema anaamini walichoshauri kitashughulikiwa na wakiona imeenda tofauti basi wao watatoa Waraka. Hao TEC wamekurupuka!

Binafsi niwashauri TEC. Wawe makini sana na Baba Padre Dk. Kitima. Alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo SAUT wakati nasoma pale 2006 - 2009. Ni mtu wa kukurupuka na kuongea kabla ya kufikiri. Hata wao Mababa Askofu wanalijua Hilo na wanajua pia ndio sababu ameshindwa kuupata Ubaba Askofu kutokana na hilo. Wawe makini asiwapotoshe!
Mpaka leo haikija shughulikiwa ,ujue hamna kitu hapo saa100 anafikiriaje kurudisha hela za watu alizohongwa
 
Back
Top Bottom