richaabra
JF-Expert Member
- Jul 12, 2016
- 1,454
- 3,469
Mimi ni muumini wa hili kanisa usharika wa Mbezi Louis, tokea nianze kusali nikiwa sunday school pale ni mwaka wa 18 sasa, katika vitu nlivyogundua ni kwamba haya makanisa hasa Kkkt yanaendeshwa kupitia sadaka za waumini yaani waumini wakisema wasitoe sadaka ndani ya miezi 3 tu hali ya viongozi ipo taabani
Usiposhiriki misa au kutoa Sadaka unaonekana mkosaji, ibada nzima ni michango tu kikapu kuanzia mwanzo hadi mwisho watu wanakamuliwa ni pesa kwenda mbele ila sijui kama wanajua hizo pesa zinapotokea ni wapi
Linapokuja swala la uchumi tunatakiwa tuwe kitu kimoja, kesho kama taifa tukiingia mikataba mibovu alafu kesho tukaja kuivunja nchi ikiingia kwenye madeni mazito haumii mtu mwingine tunaumia wote ndio haya matozo na kodi kubwa walizoweka huu ni mwanzo tu picha linakuja Viongozi wetu wa KKKT ikifika mahali mkaambiwa kuwa hatuna pesa sababu uchumi umeharibika muwe wasikivu maana ibada zenu ni kuomba pesa mwanzo mwisho, hajawajenga wachungaji na wainjilisti kujitegemea kiuchumi mmewajenga kuwakamua waumini kwenye kapu la sadaka.
Askofu Shoo unasema unabariki uwekezaji ni uwekezaji gani huo wa kijinga namna hii, unampa mtu Bandari kwa mkataba wa kudumu huo ni uwekezaji au uuzaji wa Bandari? Kesho akiingia kiongozi type ya Magufuli akauvunja mwishowe DP world wataenda mahakamani halafu tukidaiwa mabilioni ya pesa wanatuwekea Tozo na kodi kubwa tulipe wananchi, wananchi tukishapigika tukija makanisani mikono mitupu muwe waelewa maana kodi kubwa ni chanzo cha kufanya watu wafilisike.
Niwapongeze Roman kwa kuwa wakweli maana mmeona mbali, waumini wenu mnajua kabisa uchumi wao ukiyumba utaleta shida hadi kwenu ila uchumi ukinyooka hata kwa kanisa ni faida kubwa.
Na Mama ajue kuwa hatupingi maendeleo wala uwekezaji ila tunapinga uwekezaji wenye Dalili zote zinazoashiria uuzwaji wa mali zetu, Cha kwanza tunachotaka kujua ili Tumbariki mama kwenye Hili la Do world ni haya
1.Mkataba ni wa muda gani kwa nini kuna viashiria kuwa mkataba ni wa milele usalama uko wapi hapo, unawezaje kumpangishia mtu nyumba yako kwa mkataba wa kudumu?
2.Imekuwaje Ubinafsishe Bandari zote za Bara alafu za Zanzibar uziache Hivi Zanzibar hawapendi maendeleo? kama wanayapenda imekuwaje wao hawamo? Tukumbuke kuwa mikopo yote mikubwa Zanzibar mama hakuwasahau alihakikisha wanapata mgao wao, ila hii anayoiita Neema Zanziar hawapo maana yake ni nini?
3.Dp world kuna kipengele kuwa anapinga kuanzishwa au kuendelezwa kwa bandari mpya hadi yeye apewe taarifa na aamue yeye kubariki hilo?, Hivi fikiria kampuni ya bia ya TBL,TCC Zilipoingia ubia na wazungu wangeweka sheria kuwa hakuna kampuni yoyote ya bia itakayoruhusiwa kuanzishwa au kuzalisha bia, Ila ni TBL Pekee yao ndio mwenye hiyo kazi hebu fikiria hivi viwanda vyote pinzani vinavyoiingiza kodi kubwa serikali mfano wazee wa Serengeti Light think TBL angeweka kipengele leo Serikali ingepoteza mapato makubwa kiasi gani kwa kumlilia mtu mmoja
Endapo wazungu wa TANZANIA CIGARETTES COMPANY wangesema enzi hzo kuwa mkataba usomeke kuwa hakuna kampuni yoyote itakayoruhusiwa kufanya biashara ya kuuza sigara au kuzalisha zaidi yetu hivi think hivi viwanda pinzani visingekuwepo hali ingekuwa vipi na ni kwa nini Mkubali kusaini mkataba ambao unapinga uanzishwaji au uendelezwaji wa Bandari mpya hadi Dp ato idhini hapa ndipo shida yetu ila tukihoji mnasema tunaligawa Taifa jibuni hizi hoja.
2.a