BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Ameongeza kuwa Tume hiyo inapaswa kuwa na muundo wa Kijaji ikiwa na Watendaji ambao ni Majaji kama Tume iliyoundwa kuchunguza Majaji wanaochunguza Ukiukwaji wa Maadili ili iweze kutoa maamuzi yanayokubalika na kuheshimika.
Aidha, amependekeza Wajumbe wa Kamati ya Usaili inapaswa kuanzishwa kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania na wasitokane na uteuzi wa Rais huku akitolea mfano wa Kenya ambako Wajumbe Kamati hiyo Huteuliwa na Tume ya Utumishi ya Bunge, Chama cha Sheria, Baraza la Viongozi wa Dini na baadaye Rais hupewa majina kwaajili ya kutangaza Uteuzi wao.
==========
"Hata Wajumbe wa Kamati hiyo wote kwa sehemu kubwa ni wateule wa Rais na hivyo uhuru wao ni wa kutia maanani, ni vyema kabisa kuwa Kamati hii iwe ya Majaji kama ile iliyoundwa kuchunguza mambo yanayohusu Majaji wanapochunguzwa dhidi ya ukiukwaji wa maadili ili iweze ikatoa maamuzi yanayoheshimika na kukubalika" -Askofu Ruwai'chi
"Kifungu cha 5(2) kinasema kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe watashika nafasi zao baada ya kuapishwa na Rais, kwa mujibu wa kifungu cha 8(1) muda wa Utumishi wa Wajumbe umetajwa kuwa ni miaka Mitano (5) sawa na Ibara ya 74, Kifungu cha Nne (4) cha Katiba inavyosema, aidha kifungu hicho cha 8(2) kinatoa sababu ya ukomo wa Utumishi wa Mjumbe kuwa ni pamoja na kumalizika kwa muda wa miaka Mitano (5) tangu alipoteuliwa, ikiwa amefariki, ikiwa amejiuzuru au kujitokeza jambo lolote ambapo tangu alipoteuliwa ikiwa asingekuwa Mjumbe asingeweza kuteuliwa au ameondolewa na Rais kutokana na sababu mbalimbali kama uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi au kwa sababu nyingine yoyote au pia kwa sababu ya tabia mbaya, kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa Mjumbe, kigezo cha kutokea kwa jambo lolote ambapo kama asingekuwa Mjumbe asingeweza kuteuliwa ni Kigeni na hakipo kwenye Katiba, mandhari Katiba imetoa vigezo, sababu zinzoweza kusababisha mtu kuondolewa basi hizo ndizo kigezo halali na cha kuzingatia" -Askofu Ruwai'chi
"Kamati ya Usaili inaundwa na Kifungu cha 9(1) na kujumuishwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Mjumbe mwingine mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa kuzingatia Jinsia, isitoshe kusema kuwa hiki ni kitu kipya na kama tulivyosema hiki ni kitu ambacho hakimo katika Katiba, ili Kamati hii iweze kuwa na nguvu na iaminike ni lazima ianzishwe na Katiba na vile vile Wajumbe wake wawe ni tofauti na hawa ambao wanaonekana ni wateule wa Rais" -Askofu Ruwai'chi
"Kwa pale Nchini Kenya kwa mfano Wajumbe wa Kamati ya usaili wanateuliwa na Vyombo vya Kisheria ikiwemo Tume ya Utumishi wa Bunge, Chama cha Sheria cha Kenya, Baraza la pamoja la Viongozi wa Dini na Rais yeye hupelekewa majina ili atangaze uteuzi na sio kuwateua" -Askofu Ruwai'chi
"Kifungu cha 10(1) kinaonyesha kuwa Mwenyekiti na Makamu wake wataeuliwa na Rais moja kwa moja na wao hawahusiki na mchakato wa usaili, hili ni sawa kwani Katiba haidai hivyo lakini kosa la sheria ni kule kuwafanya Mwenyekiti na Makamu wake wasiwe Wajumbe wakati tayari Katiba inawaita ni Wajumbe, hivyo vyote ambavyo vinapendekezwa na Sheria juu ya Kamati ya usaili ni Batili" -Askofu Ruwai'chi