Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Ninavyolijua vizuri kanisa katoliki, iwapo habari hii ni ya kweli, basi nasikitika kusema kwamba baada ya muda mtasikia Askofu Kilaini ame-resign. Kanisa Katoliki kamwe haliwezi kuendekeza upumbavu kama huo.
 
Asante sana kwa maelezo mazuri, lakini mada iliyopo mbele yetu ni kwa wameiba pesa ya UMMMMMMAAAAAAA.CAG kathibitisha hilo.Kila mtu atavuna alichopanda-by Deo Fili

Na aliyeruhusu pesa ya umma ziibiwe sio Rugemalira ni serikali yako uliyoichagua na kuiweka madarakani. Hiyo ndio ibebe lawama. Au basi wakae kitako wakubaliane kurudisha hizo hela kama walivyofanya wakati wa EPA.

Tiba
 
Lakini tuwe makini hizi ni tuhuma tu , hazijathibitishwa kwa hiyo tusimhukumu mtu bila ya kusikiliza upande wake
 
Askofu Kilaini ana akaunti hapo mkombozi benki? Pesa hizo ni zake? Ana miradi gani nje ya Kanisa? Ameliambiaje Kanisa katoliki. Maswali yako mengi sana kwenye uzi huu.
 
Duh basi inatosha sasa! Ila inawezekana ilikuwa pesa ya issue nyingine kumbe ndio Mtumishi anaingizwa kwenye mtego bila kujijua

Mkuu Elli nadhani sie hatuna matatizo na wanaopewa pesa za kifisadi ambao hawako katika utumishi wa umma. Shida iko kwa watendaji wa serikali. Mtendaji au kiongozi wa serikali ukipewa pesa lazima ihojiwe ni ya nini? Tena mashaka makubwa yanakuja inapokuwa pesa ya wizi kama hii ya IPTL.
 
Last edited by a moderator:
Hemu mwanzisha tuhuma aje na empirical evidence ya transaction isije ikawa ni hoja za majitaka kwa askofu.

Ruge kala, kilaini hajahusiswa so tuuma uchwara hazimlazimu kuja hapa kutoa maelezo.
 
Hizi hela zinaingiaje kwenye accounts za watu, maana mimi accounts zangu sikutagi ongezeko lolote lile la kinyemela zaidi ya makato.
 
Kijiji chakwao wana mladi was Maji ya bomba na phase two in

kuwekea kila nyumba umeme, yeye ni mfadhili binafsi wa miladi

hii, siyo fisadi kama baadhi mnavyo dhani.

Pia kuna shule ya kilaini primary hapo hawali ikiitwa KABANGAni while ya serikari.

kilaini kabomoa majengo yote na kujenga upya. Wenyeji wa uko wanajua sasa kusema ivo viela kafisidi utakuwa ukosefu wa hoja
 
Kusema kikwete chaguo la Mungu alikosea, yeye ni binadamu.

Kumtuhumu kuwa fisadi kwa viela vinavosemekana kupewa na

Rugemalila batili.

Kama RUGE alimpa kama ufadhili, kilaini binafsi hana kosa.

Hawezi kulinganishwa na wauza meno ya tembo, wachumia

BUNGE la katiba au walanguzi wa gesi ya mtwara, came on...
 
hivi ikiletewa zawadi na muumini utajuaje zawadi no za wizi au sio za wizi?
askofu alipewa sadaka akapokea, angejuaje Kama ni pesa za IPTL?
 
Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba mhashamu Askofu Kilaini. Yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

Kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.
Bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi.

ukiweka hapa valid benki stetimenti ndo utaaminika zaidi kuliko hayo maneno matupu
 
Kaleta hoja mufilisi, atwambie basi ata hao walopewa mabilioni

Kama angepewa mabilion ningetilia mashaka but 80m ni hela
ndogo mno, rejea mwainisho wangu wa miladi kilaini anayo fanya
 
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???

Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.

Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????

Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?

kwa hiyo ulitaka kwa kuwa ni askofu tusishike bango? Na wakat anapokea hizo pesa kanisa kuu la Bukoba walipewa taarifa? na je waumini au baraza la walei walishirikishwa?? Tatizo la Milungura kama hii inaharibu hadhi ya kanisa,
 
kwa hiyo ulitaka kwa kuwa ni askofu tusishike bango? Na wakat anapokea hizo pesa kanisa kuu la Bukoba walipewa taarifa? na je waumini au baraza la walei walishirikishwa?? Tatizo la Milungura kama hii inaharibu hadhi ya kanisa,




Baba Akofu siyo saizi yako, wafuate wachafu wala rushwa na walanguzi wa meno ya tembo
 
Mimi nadhani kwa mtu yeyote akipewa pesa na rafikiyake hauwezi kumuuliza kapata wapi ila inategemea nakiwango cha pesa kukihoji,mfano hauwezi kupewa amounts kama ile ya Tibaijuka ukaacha kuuliza.Hao viongozi wa Dini ndio waliotuambia Kikwete ni chaguo la Mungu sasa huenda Mungu anaanza kuwakosoa kwayale waliyotuambia
 
Back
Top Bottom