@gollocho, siyo kweli . Sauli ni matakwa ya Wa Israel wenyewe kutaka kionglozi wa namna hiyo na Mungu hakusita kuwapa.Cha mAANA ni kwa Askofu Mwenyewe kutoa kauli kuona hizo fedha zilikuwa kwa kazi gani?. Kama ni za Kanisa je kazi ya kanisa imefanyika au katumia kwa manufaa yake.?. Askofu Mkuu wa Jimbo la Bukoba anataarifa ya fedha hizo kwenye miradi ya kanisa? au ni biashara binafsi kati ya Rugemalira na Kilaini mwenyewe?.Nionavyo hizi fedha za IPTL na Rugermalira zinaweza kuwa aibu na fedheha kwa ndgu zangu NshomileKuanzia kwa Majaji Wetu Prof. Ruangisa, Mujulizi, Prof Tibaijuka na wenzake .Lets wait and see what will happen later before 26/11/2014?
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???
Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.
Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????
Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?
sisi pesa ya rugemalila inatuhusu nini jamani kama wamepeana kirafiki utajuaje kwani kilaini yupo kwenye nafasi gani ya utendaji kwamba akihongwa anaweza kusaidia jambo fulani,hapo ndipo utaamini kuwa pesa za rugemalila ni zake alitoa kama wewe unavyoweza kumpa mdogo wako lakini kama mtu anaushahidi wa kutosha kuwa rafu imechezeka mahakama ndiyo mahara pakuondoa utata.
sioni uhusiano wa moja kwamoja wa kumtia hatiani Kilaini kwamba nae ni sehemu ya mgao wa fedha ya IPTL. Labda mtoa mada ungetuambia ni kwa namna gani kilaini anainfluence kiutendaji ktk serikali ya Tz. vinginevyo, labda aliwahi kumkopesha au kuna biashara wanafanya usilete hoja ambazo hazijengi japo tunahitaji sana kuwajua wakwapuaji wa hii fedha ya umma.
Duh basi inatosha sasa! Ila inawezekana ilikuwa pesa ya issue nyingine kumbe ndio Mtumishi anaingizwa kwenye mtego bila kujijua
Baba Akofu siyo saizi yako, wafuate wachafu wala rushwa na walanguzi wa meno ya tembo
Kikwete ni chaguo la Mungu----Askofu Kilaini
Kama Papa angeona amefanya kosa wangemtoa kabisa altareni kama walivyomfanya padri karugendo, lakini kuhamishwa haina maana amefanya kosa. Hebu tuonyeshe hiyo barua ya Papa inayoelezea makosa ya Kilaini mpaka akahamishwa kutoka Dar.
Mkuu Mwikimbi, ili tuweze kumuhukumu huyu Askofu ni lazima tujiaminishe kwamba Yeye yuko kwenye nafasi za maamuzi ambazo hizo fedha ndiko zinakotoka ama yeye ndiye jicho la kuchunga hizo fedha.
Kwa mfano, Mama Ana Tibaijuka analalamikiwa kwamba alimegewa Sh. Billlion 1 na huyo Rugemalila hii inaweza kuingia alikini kidogo kwasababu Tibaijuka ni Waziri waSerikali, Hivyo hoja inaweza kujengwa kwamba alipewa fedha hizo ili kufifisha hoja ya Wizi huo endapo itaibuka kwenye Cabinet au Kwamba alihongwa pesa hizo ili atoe kiwanja au eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine walikubaliana na mtoaji wa pesa hizo. Hapa Tibaijuka atakuwa na kesi ya kujibu kwa namna yoyote ile.
Sasa tuje kwa Askofu Kilaini, unadhani alipewa fedha hizo ili kumziba mdomo au alipewa kwa matumizi gani.? Ili tuamini kwamba labda alihongwa, Je Kilaini yuko kwenye nafasi gani ya maamuzi ndani ya serikali kiasi tudhani mtoaji ametooa ili kumziba mdomo? Je unajuaje kwamba hizo fedha zimetolewa kama Shukrani tu kwa jambo lolote/Zaka/Fungu la kumi/Mchango wowote kwa Kanisa?
Tujitahidi kabla hatujarusha tuhuma tena kwa viongozi wa dini tuwe na angalau taarifa zisizokuwa na chembe ya shaka na maelezo ya kutoshereza.... Matola wala usipite jongea utoe la rohoni.
BACK TANGANYIKA
kwa hiyo ulitaka kwa kuwa ni askofu tusishike bango? Na wakat anapokea hizo pesa kanisa kuu la Bukoba walipewa taarifa? na je waumini au baraza la walei walishirikishwa?? Tatizo la Milungura kama hii inaharibu hadhi ya kanisa,hakuna aliye juu ya sheria,
Zaka hiyo