Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,607
- 3,191
Rugemarila ni tapeli mkubwa wa kimataifa pamoja na prof. Malyamkono. Hawa ndiyo pia wanamiliki ile kampuni ya REPOA ambayo hutumika kutapeli taasisi za kimataifa kwa miradi hewa mbalimbali.
Huyu Rugemarila angekuwa China tungekuwa tulishamsahau siku nyingi. Alianzisha IPTL kwa mtaji wa TZS50,000 (elfu hamsini) halafu akapewa tenda ya mabilioni. Huyu ndiye Rugemarila ambaye utapeli wake mimi nauona ni zaidi ya Singasinga huyu wa PAP. Sitashangaa nikiambiwa hata huo uuzwaji na ununuaji wa IPTL, mpango mzima ulifanywa na Rugemarila.
Ndugu yangu, kama Rugemalira kweli aliwekeza tshs. 50, 000 IPTL na sasa amekuwa tajiri wa kutupwa, inabidi aingizwe kwenye rekodi za dunia za wajasiriamali waliofanikiwa. Ninavyofahamu mimi Rugemalira ni mfanyabiashara wa siku nyingi nani kati ya Watanzania wachache wenye hela lakini wasiotaka makuu. Huyu Bwana ndiye kampuni yake ya VIP Engineering ilileta ule mchele wa kitumbo, huyu bwana ndiye alikuwa anamiliki kampuni ya kwanza ya simu za mkononi na pia alikuwa anamiliki kampuni ya usambazaji wa oil iitwayo ELF Lubricants. Nimeandika hayo yote kuonyesha kwamba huyu bwana alikuwa na pesa hata kabla ya kuanzishwa kwa hiyo IPTL na ninashindwa kukubaliana na wewe kwamba share asilimia 30 alizokuwa anamiliki IPTL alizinunua kwa Tshd. 50, 000.00.
Naomba bandiko langu hili lisichukuliwe kama ninaunga mkono ufisadi lakini kwa kusema ukweli sioni ni kwa nini Rugemalira anatupiwa lawama wakati yeye ni mfanyabiashara aliyelipwa chake kwa maelekezo ya mahakama na serikali? Tuilaumu serikali ambayo iliagiza hawa watu walipwe hizo pesa.
Tiba