Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

kuchukua hizo pesa,hakumaanishi askofu ni fisadi,huenda alipewa kwa ajili ya miradi ya kanisa na yeye hakujua kama ni za kifisadi,msimuhukumu askofu
 
Hivi unajua maana ya kuwa kiongozi achilia mbali kiongozi wa dini/kiroho??!!!
Mkuu Ole ndo maana watu hawataki zawadi za viongozi ziwe mali ya serikali.Mambo hayawezi kuwa simpo ivo,huwezi kunilinganisha mimi na kiongozi ktk kupokea zawadi
 
Rugemarila ni tapeli mkubwa wa kimataifa pamoja na prof. Malyamkono. Hawa ndiyo pia wanamiliki ile kampuni ya REPOA ambayo hutumika kutapeli taasisi za kimataifa kwa miradi hewa mbalimbali.

Huyu Rugemarila angekuwa China tungekuwa tulishamsahau siku nyingi. Alianzisha IPTL kwa mtaji wa TZS50,000 (elfu hamsini) halafu akapewa tenda ya mabilioni. Huyu ndiye Rugemarila ambaye utapeli wake mimi nauona ni zaidi ya Singasinga huyu wa PAP. Sitashangaa nikiambiwa hata huo uuzwaji na ununuaji wa IPTL, mpango mzima ulifanywa na Rugemarila.

Njia sahihi kwake ni kujitokeza na kukiri au kukanusha. Ninachoona hapa mgawaji pesa alikuwa akitafuta influential persons na malengo yake hapa sijayajua. Huyu Rugemalira ni mtu wa namna gani? Wenye historia yake (cv) watuwekee hapa. Wabia / washiriki wake ni nani.....zahidi watafuta uraisi ili ni-conect dots kidogo... na nipate mwanga wa hapo baaadae juu ya nchi hii.
 
Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba MHashamu Askofu Kilaini. yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.

bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi

Kwa huyo usiwe na wasi wasi, atauambia alipewa kama sadaka, na anaweza kukufungulia maandiko matakatifu.
 
Askofu itabidi ajitokeze haraka sana kufafanua hiyo pesa alipewa ya nini, iko wapi na imefanya nini. Viongozi wa dini wawe makini katika kupokea misaada.

Uongozi wa Kanisa Katoliki pia ni muhimu sasa kukaa na kuchunguza kwa makini kwa nini pesa hii ya wizi ya Escrow uhamishaji wake wote umetumia bank ya Kanisa ya Mkombozi? Na pia waangalie kwa siku za mbeleni ni kwa namna gani bank hii haitatumika kupitishia pesa za wizi. Wasipofanya hivyo, bank hii itachafuka na kuonekana ni bank ya pesa za wizi na ufisadi.

Mimi kama mkatoliki nisingependa kuona taasisi ya kanisa kila mara ikitajwa kwenye vyombo vya habari jinsi mafisadi walivyoitumia benki ya mkombozi kukamilisha uhalifu wao.

kuchukua hizo pesa,hakumaanishi askofu ni fisadi,huenda alipewa kwa ajili ya miradi ya kanisa na yeye hakujua kama ni za kifisadi,msimuhukumu askofu
 
Msomi tena Askofu hawezi kuchukuwa pesa ni mtu wa mungu.
 
Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba MHashamu Askofu Kilaini. yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.

bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi

Milioni 80 mbona ni kitu Cha kawaida kwa sadaka au michango,,,!!!! Ingekuwa Kama amepewa bilioni kama alizopewa Tibaijuka hapa ningeguna pamoja na kujua kwa nini ape we hizo bilioni
 
.....iptl....pale issue ni kuwa je fedha hizo zilikatwa kodi?
 
Jamaa lilifanya kama walivokuwa wanafanyiwa Ngasuma na Papa Msofe wakiwa stejini.kuwapanya pesa
 
Kama hadi hao wanachukuwa basi hakuna kitakachotokea,

Mleta mada kwanza jibu maswali yangu alafu tuendelee. 1. Twambie hiyo pesa alipewa kwa sababu gani, ilikuwa ni sadaka, ilijuwa ni zawadi, ilikuwa ni pesa kwa ajili ya kazi ya Kanisa hila ilipitia kwa Kilaini? Je, Rugemalira alimwambia kuwa hiyo pesa ni sehemu ya pesa za IPTL, je Rugemalira hakuwa na pesa nyingine ya kumpa tofauti na hiyo ya IPTL? Je, ukiwa na rafiki mwenye uwezo wa kifedha akakwambi atakupa kiasi fulani cha pesa na tnajua kabisa kwamba pesa hiyo anayo utaikataa? Hapa wa kulaumiwa siyo Kilaini bali ni Rugemalira aliyetoa pesa hiyo. Halafu ndg mleta uzi unatudhibitishia vipi kuwa haya uliyaandika yana ukwali? Kama unao ushahidi (documents) tuwekee tuusome, vinginevyo utakuwa umeleta porojo za kutunga na kuwachafua watu. Halafu hakuna Bank inayoitwa Ukombozi kwa hapa Tanzania.
 
Mimi ni mkatoliki kabla hata sijazaliwa na bila shaka nitakufa nikiwa hivyo, ila Askofu Kilaini huwa naona ni mropokaji na mpotoshaji mkubwa, hasa alipotumia Altare ya Bwana (2005) kumpigia kampeni JK akisema ni chaguo la Mungu. Leo hii hawezi tena kukaa na kuthibitisha yale aliyokuwa anayaropoka.
 
Mama Tiba na Kila ini walipewa kwa ajili ya kampeni ya urais. Kumbuka aliwahi kutangaza Rais ni Chaguo la Mungu na hii iliwainfluence wapiga kura wengi kumchagua
 
Ndugu yangu huwezi kupokea hela ya mtu hivihivi hata kama atakuambia ni zawadi. Je kama kaziiba unafikiri wewe utasalimika? Haina tofauti na kununua gari la wizi! Hela ya kampuni ugawe kama njugu? Mkaguzi wa hesabu utamwambia kuwa ulipata ziada kubwa kiasi cha kuanza kugawa hela ya kampuni? Na kama una huruma sana kwa nini usiwagawie wale wenye shida kabisa ambao wamejaa hapa nchini?
 
Kikwete ni chaguo la Mungu----Askofu Kilaini

Chunguzeni kwa nini aliondolewa Dsm, Sio mwadilifu na mwenendo wake ulikuwa sio sawa. Ila kwanini fedha hizi zimekwenda sana kwa WAHAYA? Majaji wawili, Tibaijuka, Kilaini nk. Vipi 'mlima wa moto' hajalamba kweli?
 
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???

Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.

Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????

Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?

just someone out of the blue comes and gives you 80m,without even asking what for?anyway,it's dirty money,should not be in the church.kanisa katoliki ni kanisa imara sana na lina misingi yake tangu enzi,kama baba askofu hakujua basi hiyo m80 amrudishie mwenye nayo,kanisa haliwedhi kudhalilika kwa m80 wakati lina fedha ya kutosha.huo ulafi tuwaachie wanasiasa na hasa mama yenu aliyekiri kupokea mamilioni machafu
 
Back
Top Bottom