Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Kwani Rugemalila angetuchangia hapa JF Kama mchango wake kwa vijana wanaomiliki mtandao HUU mkubwa,huo mchango ungekataliwa??-Nawaza tu Kama Prof.Tibaijuka kwa sababu zozote zile aliomba msaada kwa Rugemalila,akapewa halafu aanze kumuuliza Rugemalila hizi hela unazonipa umetoa wapi? -To me hoja iwe kwa aliyetoa,lakini kuwashupalia waliopokea ni kutowatendea haki tu,maana Wao waliomba ,aliyewapa hakuwaambia source ni iptl au biashara ZAKE zingine.
 
Msomi tena Askofu hawezi kuchukuwa pesa ni mtu wa mungu, angekuwa Muislam ningekubali.

daaah....! nimekuelewa ila sijapenda, ni mchango wako ngoja niuheshimu kwani ndo waungwana tulivyo! tunaheshimu hata ikiuma! ahsante
 
Huu ulikua ni mkakati maalumu wa kuhakikisha mwaka 2015 rais ni mkatoliki
 
Majibu ya Rugemalira

ruge.jpg

Mmiliki kwa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni mwa waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa IPTL ukifafanua utata kuhusu mkataba wake na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa jumla kwa Pan African Energy​

Dar es Salaam. Maswali juu ya utaratibu uliotumika kutoa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye Akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutokana na mvutano baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL yameanza kupata majibu.

Wakati mmiliki kwa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira ameibuka na kukiri kuwa yeye ni miongoni mwa waliolipwa fedha hizo huku uongozi wa IPTL ukifafanua utata kuhusu mkataba wake na Tanesco na jinsi kampuni hiyo ilivyouzwa jumla kwa Pan African Energy.

Majibu ya Rugemalira

Katika ufafanuzi wake, Rugemalira alisema kati ya fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow, yeye akiwa mwanahisa wa IPTL alilipwa Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni), alizoziita ‘vijipesa vya ugoro' sawa na asilimia 30.

Alisema baada ya kuuza hisa zake kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP) aliruhusu pia asilimia 70 ya hisa za mbia mwenzake, Mechmar kutoka Malaysia ziuzwe pia kwa PAP.

Alisema kwenye akaunti hiyo kulikuwapo na Dola za Marekani 120 milioni, tofauti na kiwango kilichotajwa na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu aliyesema fedha hizo zilikuwa Dola 122 milioni.

Rugemalira alisema pia kuwa hatua ya kufikiwa kwa hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji John Utamwa Januari 17, mwaka 2014 saa 8: 30 usiku, ilitokana na Waziri wa Nishati kumuomba wamalize kesi zilizokuwa mahakamani.

"Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means' (jambo la muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo vijipesa vya ugoro," alisema Rugemalira.

Hatua ya kutoa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow na kugawiwa kwa VIP Engineering na PAP, imefikiwa huku mkopeshaji wa IPTL, Benki ya Standard Charted ya Hong Kong (SCB-HK), inayodai Dola za Marekani 145 milioni (Sh234.456 bilioni), ikiwa haijalipwa na wala haijajulikana italipwa kwa kutumia kanuni gani.

Itakumbukwa kuwa, baada ya benki za Malaysia zilizokuwa zimeikopesha IPTL kuyumba kiuchumi, deni la benki hizo lilinunuliwa na SCB-HK.

"Tumeridhia kuwa hizo asilimia 70 zichukuliwe na PAP na Standard Charted anadai kwamba yeye ndiye mkopeshaji na dhamana yake ni hiyo mitambo, kitu ambacho siyo kweli. Lakini kama ni kweli aende mahakamani kuthibitisha," alisema Rugemalira.

Hukumu iliyotolewa Februari 12, 2014 na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Washington DC, Marekani, ilitaka pande hizo mbili zikae na kukubaliana namna ya kukokotoa gharama ambazo shirika hilo la umeme linapaswa kuilipa benki hiyo.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari jana, Rugemalira alionekana kujikanganya juu ya kuitambua SCB-HK, kuna wakati alisema haitambui na hivyo haikuwa na fedha zilizokuwa Escrow na wakati mwingine alisema bado anaidai benki hiyo na kesi ipo mahakamani.

Rugemalira alisema kwamba alikuwa Mkurugenzi wa IPTL hadi Januari 24, mwaka huu alipong'atuka, ingawa pia alisema baada ya kung'atuka alikuwa bado anaiwakilisha IPTL kwenye vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kuuza hisa zake kwa PAP.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari, Rugemalira alitumia muda mrefu kuipigia debe PAP akisema ni kampuni bora inayoweza kuzalisha umeme kwa bei nafuu.

"Swali la kujiuliza sasa, IPTL ni nani, jibu lake ni PAP," alisema Rugemalira.

Pia kuhusu suala la Mkataba wa IPTL na Tanesco kuanza 1995 na kutarajiwa kufikia kikomo 2015, Rugemalira alisema siyo sahihi na kuwa mkataba huo ulianza 2002 na ulitarajiwa kukamilika 2022.

Akizungumzia suala hilo, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa bado hana taarifa rasmi.

"Kwa sasa siwezi kusema chochote, hizi taarifa ndiyo kwanza nazisoma, lakini kama itagundulika kuna vitu vimekiukwa, kuna vyombo husika vitakavyochukua hatua," alisema Utouh.

Ufilisi IPTL wabatilishwa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Philip Saliboko alisema ofisi yake ilikabidhiwa kazi ya ufilisi wa IPTL na Mahakama mwaka 2008 lakini mahakama hiyohiyo iliamuru Rita inyang'anywe ufilisi huo, Septemba 5, mwaka jana.

Saliboko alisema baada ya kunyang'anywa mamlaka ya ufilisi, IPTL ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Pan African Energy Ltd (PAT) iliyoelezwa kuinunua.

"Hata hivyo, ofisi yangu haikupewa ufilisi wa muda mrefu, ilipewa wa muda mfupi, kwa hiyo majukumu yangu hayakufikia yale ya kuuza au kufilisi mitambo, bali kuuangalia kama IPTL ipo salama hadi hatua nyingine zitakapotajwa," alisema.

Kauli ya IPTL

Mwanasheria wa IPTL, Joseph Mwakandege alisema PAT ilinunua hisa kutoka kwa VIP Engineering na Nechmar kwa uwiano wa asilimia 70 kwa 30 na baada ya kununuliwa hisa hizo, Mahakama iliamuru kuwa PAT iwe mbia wa jumla wa Kampuni ya IPTL.

Mwakandege alipohojiwa kuhusu mkanganyiko wa mkataba kati ya Serikali na IPTL, alisema makubaliano baina ya pande hizo yalikuwa ni yale ya Kujenga, Kuendesha na Kumiliki (BOO), hivyo mali za IPTL zinabaki kuwa zake hadi baada ya mkataba kumalizika 2015.

Alisema mkataba huo haukuwa na kipengele cha kuiachia Serikali mitambo yake ya kuzalisha umeme.

Kuhusu Akaunti ya Escrow, mwanasheria huyo alisema haikuwa akaunti ya Serikali, bali fedha zilizokuwamo zilikuwa mali ya IPTL baada ya kuwapo kwa mgogoro baina ya wadau – IPTL na Tanesco.

"Kwanza ifahamike kuwa Escrow ilianzishwa kwa ajili ya wadau. Baada ya VIP Engineering na Nechmar kuuza hisa, akaunti ilikabidhiwa kwa PAT," alisema.

Alisema baada ya mgogoro huo kutokea, kila mdau aligawiwa kiasi chake cha hisa na kuondoka, hivyo fedha zilizobaki ni za IPTL.

Alikanusha kuwa Akaunti ya Escrow ilikuwa na Dola za Marekani 270 milioni, bali Dola 105 milioni na wala si zaidi ya hapo.

"Nyinyi mnafikiri Escrow ni ya Serikali. Mnafikiri Serikali ni wajinga na mafisadi kiasi hicho?" alisema.

Chanzo:Mwananchi
 
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???

Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.

Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????

Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?

Ndo umeandika nn hapo. Si bora ungekaa kimya kuliko kufunua upumbavu wako
 
Kwani ishu ni fedha ya ESCROW Account au fedha ya Rugemalila? Kama kuna mtu alichota moja kwa moja fedha ya ESCROW anatakiwa atueleze, ila kama mtu alipewa na mtu aliyepewa na mtu aliyechota Escrow, hatuna haja ya kumuuliza. Vinginevyo hata mimi mlalahoi nitajikuta kwa namna fulani nimenufaika na kuchotwa kwa fedha hiyo na watu wengine!
 
Njia sahihi kwake ni kujitokeza na kukiri au kukanusha. Ninachoona hapa mgawaji pesa alikuwa akitafuta influential persons na malengo yake hapa sijayajua. Huyu Rugemalira ni mtu wa namna gani?Wenye historia yake (cv) watuwekee hapa. Wabia / washiriki wake ni nani.....zahidi watafuta uraisi ili ni-conect dots kidogo... na nipate mwanga wa hapo baaadae juu ya nchi hii.

Huu mtandao inaonekana ni mkubwa kuliko tunavyofirikiri.
 
Tatizo ni nyinyi waumini kujifanya mnajua sana kuliko wachungaji, mapadri na maaskofu, hivi wewe unajua maana ya chaguo la mungu, au unakurupuka tu kwa kuwa Kikwete ni kiongozi mmbaya? Hebu rudi kwenye biblia kasome kitabu cha 1 Samweli 8 na 9 utajua kuwa hata mfalme wa kwanza wa Israel,Saul, alikuwa chaguo la Mungu lakini hakuwa kiongozi mzuri kwani baadae alimuasi Mungu. Kwa hiyo kuboronga kwa Kikwete hakumfanyi yeye kutokuwa chaguo la Mungu.

Mm si muumini ninaekurupuka, Askofu Kilaini anatumika na wanasiasa kwa malengo yao binafsi, si busara kulitumia kanisa kwa maslahi yako binafsi. Hili suala lilifika mpaka kwa Papa na ndio sababu ya Kilaini akarudishwa kijijini kwake kutoka jimbo kuu la Dar-es Salaam
 
Kanisa la St Peters pia wamelipwa fedha hizo ,alitoa kama mchango wake katika harambee.....Lakini mimi sidhani kama kulipwa hela na Ruugemarila ni shida....Je kama mlikua mnadaiana? Tuache cheap politics
 
Siwezi kukupinga juu ya hayo mengine uliyoandika kwa sababu sina uhakika.

Lakini kwenye ile kesi ya mwanzo kati ya TANESCO na IPTL, taarifa za BRELA ilionesha kuwa IPTL ilianza kwa mtaji wa TZS 50,000 tu (paid up share capital). Na baada ya hapo ikaweza kupata mkataba wa kuiuzia TANESCO umeme, mkataba wa mabilioni ya pesa. Huu ulikuwa ni mtaji wa kuanzishia kampuni lakini siyo uwekezaji katika mradi wa ufuaji umeme. Kulikuwa na dhana kuwa si jambo la kawaida kwa kampuni iliyokuwa na mataji mdogo kiasi hicho, kampuni ambayo ilikuwa hajawahi kufanya biashara yoyote hapa Duniani, kuaminiwa na kupewa tenda kubwa kiasi kile. Pia wakati wa uwekezaji katika mradi wa ufuaji umeme ilithibitika kuwa uwekezaji ulikuwa ni mdogo sana tofauti na Rugemarila alivyokuwa akidai.

Mafanikio ya biashara hayaangalii faida pekee yake bali na uhalali wa biashara yenyewe. Inawezekana Rugemarila amefanikiwa kupata faida kubwa lakini faida yenyewe inapatikana kwa mbinu chafu ambazo haziangukii kwenye misingi bora ya biashara, ni kama huu wizi alioufanya kwenye ESCROW, na kujipatia U$75 million. Ni dhahiri kampuni yake itaonekana kuwa na hela nyingi lakini je, tuite haya ni mafanikio katika biashara au mafanikio katika wizi kwa kupitia mwavuli wa biashara?

Ndugu yangu, kama Rugemalira kweli aliwekeza tshs. 50, 000 IPTL na sasa amekuwa tajiri wa kutupwa, inabidi aingizwe kwenye rekodi za dunia za wajasiriamali waliofanikiwa. Ninavyofahamu mimi Rugemalira ni mfanyabiashara wa siku nyingi nani kati ya Watanzania wachache wenye hela lakini wasiotaka makuu. Huyu Bwana ndiye kampuni yake ya VIP Engineering ilileta ule mchele wa kitumbo, huyu bwana ndiye alikuwa anamiliki kampuni ya kwanza ya simu za mkononi na pia alikuwa anamiliki kampuni ya usambazaji wa oil iitwayo ELF Lubricants. Nimeandika hayo yote kuonyesha kwamba huyu bwana alikuwa na pesa hata kabla ya kuanzishwa kwa hiyo IPTL na ninashindwa kukubaliana na wewe kwamba share asilimia 30 alizokuwa anamiliki IPTL alizinunua kwa Tshd. 50, 000.00.

Naomba bandiko langu hili lisichukuliwe kama ninaunga mkono ufisadi lakini kwa kusema ukweli sioni ni kwa nini Rugemalira anatupiwa lawama wakati yeye ni mfanyabiashara aliyelipwa chake kwa maelekezo ya mahakama na serikali? Tuilaumu serikali ambayo iliagiza hawa watu walipwe hizo pesa.

Tiba
 
Mm si muumini ninaekurupuka, Askofu Kilaini anatumika na wanasiasa kwa malengo yao binafsi, si busara kulitumia kanisa kwa maslahi yako binafsi. Hili suala lilifika mpaka kwa Papa na ndio sababu ya Kilaini akarudishwa kijijini kwake kutoka jimbo kuu la Dar-es Salaam

Kama Papa angeona amefanya kosa wangemtoa kabisa altareni kama walivyomfanya padri karugendo, lakini kuhamishwa haina maana amefanya kosa. Hebu tuonyeshe hiyo barua ya Papa inayoelezea makosa ya Kilaini mpaka akahamishwa kutoka Dar.
 
Acha WİVU WA KİKE...mama ako alitolewa b.i.kr.a na haus boi..huu si uzushi na kama ni uongo aje hapa kukanusha,hii si chuki maana hata mimi ni houseboi

jamani mama zetu wamekosa nn? unaweza kuwa na wazo zuri lkn jinsi ulivyolileta inaweza pelekea ukapuuzwa! wamama ni watu muhimu sana 2waheshimu,mama yangu ni mama yako na mama yako ni mama yangu wote wana sifa sawa {wame2fanya tuwe hapa sasa}.mchango wako umenifanya mpaka nitoke nje ya mada! polen wakinamama mungu atawasimamia!
 
Kwanza ijulikanr kabise rugemalila alilipwa pesa zake halali.ila yeye pia a limit a had garish a serikali kuhusu uchotwaji Wa hizo pesa akiitaka serikali iangalie kwa makini ilo suala kua kuna wajanja wamepanga kukwapua izo hizo.yeye kama mbia alikua na haki ya kuuza visa zake na alifanua hivyo kisheria na kihalali.report akija ndo mtashaangaa kwa io alowapa hela watakua safe sana.fedha chafu ni ile aliyolipwa sighs nae akamlipa rugemalila.kwa ilo rugemalila hapa nae ni mhanga Wa izo fedha chafu kama alivyopewa na alivyowapa wengine tutaujua ukweli wote soon.
 
Huyu rugemarila bila shaka ni mhaya huyu.. Maana naona anagawa hela kwa wahaya wenzake

anyway huyu atakuwa rostam namba mbili... Maana rostam alimsapoti JMK
 
Zakajamani alikuwana billion 80 gawakwakumi nimillion 80 kwawale waopitia aata .....
 
Kama Papa angeona amefanya kosa wangemtoa kabisa altareni kama walivyomfanya padri karugendo, lakini kuhamishwa haina maana amefanya kosa. Hebu tuonyeshe hiyo barua ya Papa inayoelezea makosa ya Kilaini mpaka akahamishwa kutoka Dar.

Kwa hili kosa baba askofu hana pa kutokea TEC haitamvumilia kuchafua kanisa.Je pesa zimeingia kwenye account ya kanisa?? kama ni binafsi lazima abebe ka-msalaba kake. Kama amezipitishia kanisani basi ni kashfa kwa kanisa.Naanza kuogopa zaidi hii IPTL saga.
 
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???

Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.

Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????

Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?

That is APPEAL TO PITY. Jenga hoja acha kutafuta huruma. Sasa unalialia nini...kama kuku jike a.n.a.p.andwa na jogoo....
 
Back
Top Bottom