Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

muu umetoa darsa murua sana, Tatizo ni hawa wanafunzi wako, uwezekano wa kuelewa hoja ni mdogo ndo maana sisi wengine huamua kuwa blast tu.

Ni imani ataelewa tu.Maana hili swala liko wazi kabisa
 
Wacha kutumia lugha ya kuudhi kwa viongozi wa kidini maana haisaidii chochote

Nini cha kuudhi hapo? Kumbuka viongozi wa dini si Mungu, bado ni binadamu tu. Sasa kazi kwenu anaowaabudu na kuwafanya miungu watu
 
Kuanzia sasa wale waliofika kwa Gwajima kupata ushauri wa kiroho, you know the name of the game. Hakuna aliye salama. Sitarajii mapadre wakatoliki wajitokeze hadharani kumwaga maungamo ya waumini wao hadharani kwa sababu ya political interest.

kwani ya Dr Mihogo yalikuwa maungamo!
 
magamba kaeni chini mfanye uteuzi...kuwatumia usalama wa ccm kumlinda na kumlisha maneno dr slaa ili akawatukane wakristo kutawatokea puani mwaka huu. wapuuzy wakubwa!
 
sijui nimuamini nani

kende ndugu yangu...hawa wanasiasa wanamengi sana tusiyoyajua kiasi cha kuwaamini...mi nakushauri piga kura yako ya mabadiriko ifikapo hiyo 25/10 mambo ya kuwaamini achana nayo...hawasomeki!
 
Last edited by a moderator:
Hili ndio tatizo la watanzania wengi, tunapenda kukurupuka bila kufanya utafiti. Kama ulisikiliza hotuba ya Dr. Slaa alimnukuu huyo Gwajima kuwaa ndiye aliyesema na kuwa Maaskofu 30 wakatoliki wamehongwa maana wale wa Kilutheri walishakubali kumuunga Lowasa mkono. Dr. Slaa alisema kama ni kweli maaskofu wamehongwa?!!!!

Hata mimi namshangaa Gwajima kama kiongozi wa dini kutoa siri za waumini wake na kuendelea kusema kuwa Dr. Slaa amewatukana maaskofu akisahau jinsi alivyomtukana Kadinali Pengo. Kweli manabii wa uwongo hawataisha!
ahahahaha, pole mkuu, ndo Gwajima huyo, haangaliagi nyani usoni, anatwanga kotekote. Gwajima ukimletea za kuleta anakupa zotezote.
mshumbuzi kam-delila dr slaa wetu.
 
We are talking about the Moral responsibilities of Religious leaders, and especially those who listens to the confessions of their flocks. Also do not forget that it is the role of religious leaders to intervene and try and resolve any problems between couples and families, thus is it morally correct to talk of these confessions and problems in public and at press conference paid for with his followers contributions. Viongozi wa dini wanapaswa kuwa na uvumilivu wa ziada.

Jee unaunga mkono Gwajima kurekodi mazungumzo ya watu anaotatua matatizo yao, Jee anawafahamisha kama anawarekodi??
yeye dakitari slaa kama kiongozi mkubwa wa kisiasa, tena aliyekuwa na wafuasi na wapenzi nchi nzima, tena padiri mstafuu na baba wa familia ya wake kadhaa, ilikuwa sahihi kwake kusema uongo kuwa kahama chadema sababu ya lowassa? ilikuwa sahihi kwake kudanganya kuwa mashekhe na maaskofu wamehongwa? ilikuwa sahihi kwake kumwita askofu Gwajima mshenga?

acha dakitari apewe za uso, kajitakia huyo kwa kudelilwamo na delila.

ukawa tulidhamiria kufanya sisa za kistaarabu lakini siasa za majitaka mmeziasisi ninyi ssm sasa acha mvune mlichopanda.

na bado, dakitari ameambiwa afungue tena mdomo wake ndo atajua kwa nini mkia wa beberu ni mfupi
 
Dr Slaa alisema mambo makubwa mawili kuhusu Gwajma:

1) Kuwa ndiye alikuwa mshenga wa Lowasa kuichumbia CHADEMA. Wote tulikuwa tumeaminishwa na Mwewenyekiti wa CHADEMA kuwa UKAWA ndio walimfuata Lowasa kumuomba agombee urais kupitia CHADEMA. Baada ya Slaa kusema Gwajima alikuwa kuwadi wa kuiomba CHADEMA imruhusu Lowasa apitie huko kugombea urais watu wulihitaji ufafanuzi na kutaka kujua Gwajima kama kiongozi wa dini anabakije salama akishiriki siasa kwa undani huo

2) La pili tulilotarajia Gwajima ajibu ni kama kweli alimwambia Slaa kuwa makanisa yanamuunga Mkono Lowasa-Walutheri kwa kuwa yeye ni mLuteri na Wakatoliki kwa kuwaonga maaskofu 30 kati ya 34.
Majibu ya Gwajima tena baada ya kuwasubirisha watanzania yameishia kueleza kuwa Slaa hakuacha siasa kwa sababu ya Lowasa bali kalazimishwa na mkewe.

Kusingekuwa na agenda ya uchaguzi; Gwajima akasema haya, hii ingekuwa habari ya maana. Sasa watanzania tunahangaika kushawishiana namna ya kumpata rais bora. Mgombea mmoja ana historia ya kashfa za kupenda mali toka enzi za mwalimu Nyerere.

Slaa amekuja na ‘kuchafua hali ya hewa' kwa kuwaeleza watanzania ukweli wa mgombea huyu. Gwajima akatarajiwa kusema lolote la maana. Anaishia kueleza habari za raia wa kawaida (Slaa) kuwa alizuiwa na mkewe kuendelea na Siasa. Hii inamsaidiaje mtu anayetaka kuamua kati ya Magufuli na lowasa?

Mimi ninafikiri gwajima ana matatizo tena yameshika kichwani. Jumla ya mwenendo wa Gwajima unaashiria hayo. Josephina kumzuia Slaa kuendelea na siasa haimaanishi kuwa Gwajima hakumwambia Slaa kuwa maaskofu walihongwa. Kwa kutosemea hilo anaendelea kuwaweka pagumu viongozi hawa. Nimesikia maelezo ya mmoja wao kuwa kanisa linadumu kuchangisha. Mimi sijui sana lakini kama kanisa linadumu kuchangisha ni lazima lijielekeze kuchangisha watu waadilifu vinginevyo litapoteza maana halisi ya kanisa. Wako maskini wengi waadilifu wanatosha kuyachangia makanisa. Haiwezekani maaskofu 30 kumchangisha mtu mmoja wote bila kujua na bila kujua kuwA SI MUADILIFU.
 
gwajima.jpg
 
Kama unalengo la kumtetea Gwajima sikuungi mkono. Tatizo watu kama Gwajima wanajaribu ku- brainwash watu.
Tafakari; Leo anakuja kusema kuwa kanisa Katoliki na viongozi wake ni "very credible" wakati juzi juzi tu kamdhalilisha vibaya kiongozi wao mkuu (Card. Pengo). Sasa anajikomba kwao, au anajua jamaa wamesahau!! Hiyo credibility ya kanisa hilo ameigundua lini, leo? Huyu si anadhani wote sie ni wajinga na brainwashed?

Kanisa siyo Pengo. Pengo alisaliti maaskofu wenzake. Gwajima hakulisema kanisa wala maaskofu katoliki alimzungumza mmoja aliyesaliti maaskofu wa TCF.
 
YOTE JUU YA YOTE UKOMBOZI NA MABADILIKO NI LAZIMA 2015, aliyepo out aliye nje ndani
 
Kama maelezo ya gwajima ni sahihi basi salaa ni mtu dhaifu sana kwa wanawake. Si ajabu kuwa na wanawake 2 au zaidi tangu aache upadre. Hainiingii akilini mwanamke amwamrishe na kumdhalisha kiasi hicho. Mie ningeingia na mlango. Inawezekana tatizojkawa mkewe ndio mwenye nyumba. Hapo lazima aipate. Mwanaume gani anadhishwa ovyo mpaka kuzuiwa kwenda kazini! Haiingii akilini. Yaani nashindwa hatabkuandika. Mwanamke uliyemuoa. Au slaa ndie aliolewa. Kwangu mimi mgemkuta mhimbili asubuhi.
 
Nachukia sana na huwa simalizi hata kusoma uzi unaochonganisha mambo ya dini na ukabila. CCM mmeishiwa hoja baada ya watu wenu kuchukua pesa nyingi pasipo impact yoyote UKAWA. Tukutane October mapakashume nyie.
 
Back
Top Bottom