Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Dr kavuna alichopanda,cha msingi aje akanushe ili Gwajima aendelee kutueleza kilicho mpeleka Dr kwa Madiba nawatu aliokwenda nao.hayo mengine tunamwachia Bi jose na familia yake.

Inasikitisha kwani Watanzania tumekuwa watu wa visasi na wa kupenda maovu na fitna. Sasa huyu Askofu asiyefyatilia maagizo ya kiroho na anavunja sheria zote za uchungaji, hivyo kweli wewe unamuona anafanya jambo zuri.

Slaa ni mwana Siasa, anastahili kujibiwa na wanasiasa, mchungaji anastahili kuvumilia. Mbona Gwajima alipomtukana ASKOFU MKUU WA KANISA KATOLOKI, yeye hakujibiwa kwa mbwembwe au kebehi, ila Cardinal Pengo alimsamehe na kumuombea kheri.

Lets be realistic, we can allow politicians to play their games, but we should never allow Religious leaders kuanika chupi zetu chafu uwanjani. HAIKUBALIKI KATIKA MADHEHETU YOTE YA KIDINI ULIMWENGUNI, GWAJIMA HAS TO REPENT PERIOD>
 
Viongozi wako wa dini ni malaika!? Mimi sio muumini wa Gwajima ila nilifurahi kitendo chake cha kumkemea Pengo

Kwa hiyo kama viongozi wengine siyo malaika ndio excuse ya Gwajima kutoa matusi kwa Kadinali Pengo? Kama ulifurahi Gwajima kumtukana Pengo, kwa nini tena leo unafurahi Gwajima huyohuyo anaposema Dr. Slaa amewatukana maaskofu na yeye atawatetea? Hii inamaanisha wewe na Gwajima wote wanafiki?!!! Utawateteaje maaskofu ambao hata wewe uliwatukana?
 
Kwani lini alikwambia anawachukia kumsema pengo ilikua sawa na hata hili sakata la slaa yupo pia hata maaskofu wenzake wa kikatoliki wanamlazia damu tu
 
Hili ndio tatizo la watanzania wengi, tunapenda kukurupuka bila kufanya utafiti. Kama ulisikiliza hotuba ya Dr. Slaa alimnukuu huyo Gwajima kuwaa ndiye aliyesema na kuwa Maaskofu 30 wakatoliki wamehongwa maana wale wa Kilutheri walishakubali kumuunga Lowasa mkono. Dr. Slaa alisema kama ni kweli maaskofu wamehongwa?!!!!

Hata mimi namshangaa Gwajima kama kiongozi wa dini kutoa siri za waumini wake na kuendelea kusema kuwa Dr. Slaa amewatukana maaskofu akisahau jinsi alivyomtukana Kadinali Pengo. Kweli manabii wa uwongo hawataisha!

Kwa mfano umedanganywa nini!?
 
Dr alijisahau akamtaja Gwajima kwa jina la Mshenga lililolenga kumdhalilisha.
Sasa kwa nini Gwajima kumchana.Dr.iwe nongwa?

dawa ya moto ni moto dr. ajue watu wana hasira sana na ccm mtu yoyote uwe maarufu kiasi gani juhud za kuitetea ccm utapata shida sana kama dr. mihogo
 
No lini wewe unae hoji umekuwa askofu au shekhe au umetumwa? Nani kakwambia gwajima kuwatetea maaskofu wenzake na mashehe ni kosa?. Mbona slaa alidhihalki mpango was lowasa wa kuwatoa mashehe akipata urais? Hivi unajuwa kama Dr.slaa amewahi kumwomba advocate kibatara peter awatetee hao mashehe mnao waita magaidi? Au mnaropoka tu kwasababu mnalipwa?. Angekuwa baba yako shehe yuko mahabusu anabakwa ungeaandika huo upuuzi wako?.
umeanza vizuri ila hiyo baba yako hapo chini imeonyosha una upungufu kwenye ubongo siuo mzima wewe
 
Dr alijisahau akamtaja Gwajima kwa jina la Mshenga lililolenga kumdhalilisha.
Sasa kwa nini Gwajima kumchana.Dr.iwe nongwa?
Alimtaka katika hali ya kumdhihaki na kumdhalilisha.
Akamuita mshenga na kusema wakati gwajima anamwambia alidhani ni sifa kumbe ni ujinga, sasa kama mtu anaweza kukudhalilisha nammna hiyo kwa nini na wewe usimlipue.
Dr mihogo aliyataka mwenyewe.
 
No lini wewe unae hoji umekuwa askofu au shekhe au umetumwa? Nani kakwambia gwajima kuwatetea maaskofu wenzake na mashehe ni kosa?. Mbona slaa alidhihalki mpango was lowasa wa kuwatoa mashehe akipata urais? Hivi unajuwa kama Dr.slaa amewahi kumwomba advocate kibatara peter awatetee hao mashehe mnao waita magaidi? Au mnaropoka tu kwasababu mnalipwa?. Angekuwa baba yako shehe yuko mahabusu anabakwa ungeaandika huo upuuzi wako?.

inasikitisha kuto kuelewa
 
Alimtaka katika hali ya kumdhihaki na kumdhalilisha.
Akamuita mshenga na kusema wakati gwajima anamwambia alidhani ni sifa kumbe ni ujinga, sasa kama mtu anaweza kukudhalilisha nammna hiyo kwa nini na wewe usimlipue.
Dr mihogo aliyataka mwenyewe.

Wanaodai Gwajima kakosea kumdhalilisha.Slaa walitaka.Gwajima afanye nini baada ya Slaa kumidhihaki namna ile?Alichokifanya Gwajima ni kutoa ufafanuzi wa uhusiano wake na Slaa na kuweka wazi ushiriki wake kumleta.Lowasa UKAWa.
 
Niliskiliza hotuba ya Dr. Slaa vzuri, sikuskia hilo tusi kwa maaskofu.
Kuhusu kuhongwa kwa maaskofu nilimsikia akisema Gwajima ndiye aliyemwambia Dr. Na akasema Kuwa kama alichoambiwa na Gwajima ni kweli, basi maaskofu wajitafakari then wapige magoti watubu.
 
CCM mna teseka ya nini kuanzisha mi post kibao!? Modi hongera kwa kuziunganisha zoote.👏👏👏👏
 
Mimi kama mwana jamvi wa muda mrefu ninasikitika sana kuona maana halisi ya jamiiforum ikibadilika toka jamvi la watu wenye fikra pevu, watu wanaojadili mambo kwa upana wakiangalia maslahi mapana ya nchi yetu, watu wanaojua kujenga hoja, kuzifafanua na kuzitetea kwa hoja na lugha yenye hekima, busara na upeo wa kiwango cha juu, leo imebadilika kuwa uwanja wa wahuni, walevi na watu wasiokuwa na hekima.
Lugha za matusi, uchochezi na ushabiki wa kijinga zimetawala jamvi mpaka kufikia wakati watu wanashindwa kuweka mambo sensitive ili yajadiliwe kwani watu smart na wanaojua kuchambua na kujadili mambo kwa upana na uelewa wa kiwango kilichokuwepo awali hawapo tena.
Inakera na kuuma sana kuona sehemu pekee ambayo watu wenye akiri timamu na wazalendo wa kweli walikua wakikutana kujadili na kubadilishana mawazo imekuwa namna hii.

"TUJISAHIHISHE"
Kama akili yako haijakomaa kwa kiwango cha kutosha kujadili mambo nyeti na yanayoamua mwelekeo wa Nchi yetu, bora mara trillion Ukae kimya na kusoma tu wanachochangia wenye akili timamu.

Huu ujinga mnaofanya humu kama wahuni wa vijiweni wanaochangia wakiwa wamebwia drugs na pombe nawaombeni sana muuweke pembeni.

INASHANGAZA SANA KUONA WATU WAKICHANGIA THREADS ZA AINA HII KWA USHABIKI WA AJABU AJABU KANA KWAMBA KILICHOFANYIKA NI KIZURI SANA.
UJINGA MKUBWA.
JAMBO ALILOFANYA GWAJIMA NI JAMBO LA KUKEMEWA KWA NGUVU ZOTE.
SASA WATU HUMU ETI SABABU TU GWAJIMA YUPO UPANDE WA UKAWA WANATAKA KUHALALISHA UPUUZI ALIOONGEA.
KUWENI NA AKIRI ENYI KIZAZI KILICHOPOTEA
vip lile alilofanya slaa je? ni la kupongezwa? au ndo kunya anye kuku akinya bata kaharisha??!!

akuanzae mmalizie, tumeshageuza shavu la kushoto vya kutosha sasa.
 
Mimi kama mwana jamvi wa muda mrefu ninasikitika sana kuona maana halisi ya jamiiforum ikibadilika toka jamvi la watu wenye fikra pevu, watu wanaojadili mambo kwa upana wakiangalia maslahi mapana ya nchi yetu, watu wanaojua kujenga hoja, kuzifafanua na kuzitetea kwa hoja na lugha yenye hekima, busara na upeo wa kiwango cha juu, leo imebadilika kuwa uwanja wa wahuni, walevi na watu wasiokuwa na hekima.
Lugha za matusi, uchochezi na ushabiki wa kijinga zimetawala jamvi mpaka kufikia wakati watu wanashindwa kuweka mambo sensitive ili yajadiliwe kwani watu smart na wanaojua kuchambua na kujadili mambo kwa upana na uelewa wa kiwango kilichokuwepo awali hawapo tena.
Inakera na kuuma sana kuona sehemu pekee ambayo watu wenye akiri timamu na wazalendo wa kweli walikua wakikutana kujadili na kubadilishana mawazo imekuwa namna hii.

"TUJISAHIHISHE"
Kama akili yako haijakomaa kwa kiwango cha kutosha kujadili mambo nyeti na yanayoamua mwelekeo wa Nchi yetu, bora mara trillion Ukae kimya na kusoma tu wanachochangia wenye akili timamu.

Huu ujinga mnaofanya humu kama wahuni wa vijiweni wanaochangia wakiwa wamebwia drugs na pombe nawaombeni sana muuweke pembeni.

INASHANGAZA SANA KUONA WATU WAKICHANGIA THREADS ZA AINA HII KWA USHABIKI WA AJABU AJABU KANA KWAMBA KILICHOFANYIKA NI KIZURI SANA.
UJINGA MKUBWA.
JAMBO ALILOFANYA GWAJIMA NI JAMBO LA KUKEMEWA KWA NGUVU ZOTE.
SASA WATU HUMU ETI SABABU TU GWAJIMA YUPO UPANDE WA UKAWA WANATAKA KUHALALISHA UPUUZI ALIOONGEA.
KUWENI NA AKIRI ENYI KIZAZI KILICHOPOTEA
Mr nawewe jitafakali pia ulichoandika hapo juu ni ushabiki huwezi kusema gwajima akemewe kwa kosa gani alilolifanya kwani Dk, slaa alichokizungumza kny mkutano wake kina masilahi gani na nchi kama una akili timamu tafuta chanzo cha haya yote yanayojitokeza sasa
 
Nimemsikiliza kwa makini jana Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima akitoa utetezi wake juu ya kile kilichoelezwa na Dr Slaa kuwa ni Ushenga baina ya ndoa ya Lowasa na CHADEMA. Kimsingi amekubaliana na yale yaliyoelezwa na Dr Slaa na kujitetea eti alikuwa anafanya hivyo kama wajibu wake wa msingi kwa wanasiasa. Eti kwamba wanasiasa wengi wanapotaka kugombea wanaenda kwa waganga wa kienyeji hivyo yeye alitaka kumuandaa Lowasa kiroho.

Jambo lililonishtua zaidi ni pale aliposema kuwa kama Dr Slaa ataendelea kuwatukana Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Anglikana, Lutherani, TAG, Masheikh na Maimamu nk, hatakaa kimya bali atajitokeza kuwatetea. Kwamba Masheikh na Maaskofu wasijisumbue kumjibu Dr Slaa bali yeye ataifanya kazi hiyo.

Binafsi nimetafakari sana juu ya msimamo huu wa Gwajima. Nimejiuliza, ni wapi Dr Slaa kawatukana Masheikh na Maaskofu? Au kuwaambia kuwa baadhi yao wamepokea hongo toka kwa Lowasa jambo ambalo ni kweli ni matusi? Ni lini Gwajima amekuwa na urafiki na Maaskofu wa Kanisa Katoliki? Ni lini Gwajima amekuwa na Urafiki na Masheikh na Maimamu?

1. Gwajima aliwahi kumtukana Askofu Pengo wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam

2. Gwajima huyo huyo aliwahi kumtukana Askofu Balina wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga ambaye kwa sasa ni marehemu.

3. Gwajima pia aliwahi kumtukana Askofu Norbert Mtega wa Kanisa Katoliki, Jimbo kuu la Songea.

4. Gwajima pia aliwahi kuwatukana Masheikh na Maimamu wakati wanadai haki ya Waislam ya kuwa na Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba Mpya.

Kimsingi Mchungaji Gwajima katika hili hana moral authority ya kumnyooshea kidole Dr Slaa ambaye hajatukana. Yeye ndiye alipaswa kujikanya mwenyewe kwa matusi ambayo amekuwa akiporomosha kila siku kwa mahasimu wake kiroho na kisiasa.

Sehemu yoyote palipo na mazungumzo yenye lengo la kuleta AMANI basi tofauti binafsi huwekwa pembeni.

Iko wazi kuwa waislam hawaiamini dini ya kikristo.Na pia wakristo nao hawamtambui Mtume Mohamed.

Lakini hilo haliwafanyi waikristo na waislam kutozungumza.

Gwajima angeonekana wa ajabu kwenda pale mbele alafu akazungumzia dhehebu lake tu,maana huo ungetafsiriwa kama Udini.

Alafu kitu kingine mkuu,kutukanwa kwa mtu sio mpaka akutukanie Mama au matusi tuliyozoea.

Tambua kwa watu wenye heshima kubwa kama viongozi wa dini,tena katika daraja la UASKOFU kuhusishwa na tuhuma za rushwa ambazo sio za kweli NI ZAIDI YA TUSI.

Kwahiyo kama ni kweli Dr.Slaa amezusha hizi tuhuma,basi alichofanya ni zaidi ya kuwatukana.

Pia Gwajima ana haki ya kuwatetea maana ni yeye ndio kahusishwa nao.

Kwahiyo mkuu sioni cha ajabu katika hili swala.
 
Inasikitisha kwani Watanzania tumekuwa watu wa visasi na wa kupenda maovu na fitna. Sasa huyu Askofu asiyefyatilia maagizo ya kiroho na anavunja sheria zote za uchungaji, hivyo kweli wewe unamuona anafanya jambo zuri.

Slaa ni mwana Siasa, anastahili kujibiwa na wanasiasa, mchungaji anastahili kuvumilia. Mbona Gwajima alipomtukana ASKOFU MKUU WA KANISA KATOLOKI, yeye hakujibiwa kwa mbwembwe au kebehi, ila Cardinal Pengo alimsamehe na kumuombea kheri.

Lets be realistic, we can allow politicians to play their games, but we should never allow Religious leaders kuanika chupi zetu chafu uwanjani. HAIKUBALIKI KATIKA MADHEHETU YOTE YA KIDINI ULIMWENGUNI, GWAJIMA HAS TO REPENT PERIOD>
ssm ndo mlivopanga na huyo slaa lakini ukawa nao ni vichwa mjue? kiwalacho ki nguon mwenu ssm, ukawa wanapata taarifa ya mikakati yenu kabla hamjaifanyia kazi. bomu mlilowarushia ukawa wamelidaka na kulirudisha kwenu kwa kasi ya kombora la b52, limewalipukia. mwaka huu ssm inapigwa kutokea ndani na kutokea nje.
 
Sehemu yoyote palipo na mazungumzo yenye lengo la kuleta AMANI basi tofauti binafsi huwekwa pembeni.

Iko wazi kuwa waislam hawaimini dini ya kikriato.Na pia wakristo nao hamtambui Mtume Mohamed.

Lakini hilo haliwafanyi waikristo na waislam kutozungumza.

Gwajima angeonekana wa ajabu kwenda pale mbele alaf akazungumzia dhehebu lake tu,maana huo ungetafsiriwa kama Udini.

Alafu kitu kingine mkuu,kutukanwa kwa mtu sio mpaka akutukanie Mama au matusi tuliyozoea.

Tambua kwa watu wenye heshima kubwa kama viongozi wa dini,tena katika daraja la UASKOFU kuhusishwa na tuhuma za rushwa ambazo sio za kweli NI ZAIDI YA TUSI.

Kwahiyo kama ni kweli Dr.Slaa amezusha hizi tuhuma,basi alichofanya ni zaidi ya kuwatukana.

Pia Gwajima ana haki ya kuwatetea maana ni yeye ndio kahusishwa nao.

Kwahiyo mkuu sioni cha ajabu katika hili swala.
muu umetoa darsa murua sana, Tatizo ni hawa wanafunzi wako, uwezekano wa kuelewa hoja ni mdogo ndo maana sisi wengine huamua kuwa blast tu.
 
Back
Top Bottom