Kiukweli, kwa sisi tunaompenda dr Slaa kiukweli kweli, tunaumia na tunamsikitia sana huyu mzee wetu.
Baada ya miaka mingi ya utumishi huku na kule, baada ya mambo mengi ya kishujaa na kujitolea, sasa hivi ndivyo maisha ya huyu mzee yanavyoishia....Total disgrace and failure of the highest order.
Hata kama, kwa move zake za sasa, kuna maslah flan hivi ya kifedha kayapata dr slaa, hata kama ni makubwa kias gan, kiukwel hayawezi kulingana na gharama na kiwango cha heshima na nafasi aliyokuwa amejijengea slaa hapa Tanzania, kwa Watanzania na dunia kwa ujumla. Dakta kadanganyika sana aisee!! kiukwel ukisikia binadam kutumika exactly kama kondomu ndo huku. kondomu huwa inatupwa kwenye shimo la choo au kumwagiwa mafuta ya taa/petrol na kuchomwa moto baada ya kumaliza ile kazi yetu.
Kosa alilofanya dakta Ni kama vile Mandela alivotoka gerezani baada ya miaka 27 eti ageuke na kusema anaungana na makaburu kuendeleza utawala wao makaburu. Hata kama angekuwa amepewa magunia ya pesa sidhani kama yangekuwa na maana yoyote kwake ukilinganisha na nafasi yake kwa nchi yake, watu wake na dunia kwa ujumla.
Kweli kina mama na kina dada ni kina mama na dada zetu na ni kweli kila penye mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke nyuma. Hata hivyo, kupitia hili, na mengine ya aina hii, ni vema pia wanaume tuwe macho kuwa baadhi ya wanawake ni viumbe khatari sana, kwa maisha na harakati za mwanaume, hasa kama tukikosea namna ya kuwa handle.
Ama kwa hakika, Kwa wale wasomaji wa biblia, hii ni stori ya kusikitisha sana ya Samsoni mwenye nguvu na mamlaka kulaghaiwa kizembe na kizezeta sana na kiumbe mwanamke.
dah, eeeh Mungu eeeeeh...well, anyway, kwaheri dakta, tumeshakupoteza!! umeachwa uchi wa mnyama.
Naandika hapa kwa uchungu sana, tunakusikitikia na kukuhurumia sana mzee wetu, lakini safari ya ukombozi lazima iendelee.
Kwa wale wasomaji na waumini wa biblia, Bwana Yesu Kristu ilibidi adhalilishwe kwa kutukanwa, kutemewa mate na makohozi, taji la miiba kichwani na mwisho kutundikwa msalabani uchi na kwa aibu kuu hadi kifo lakini mwishoni alikishinda kifo, akafufuka kutoka kaburini na kuwaletea ukombozi wa milele mamilion kwa mamilioni ya watu wamwaminio. Kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristu, Mzee wangu dakta slaa pengine usiwaze sana mzee kwa uchafu huu uliojipaka mwenyewe kwani, kama ilikuwa ni lazima ujivue nguo, na ubaki uchi hivyo, ili Taifa nzima la Tanzania likombolewe, basi na iwe hivyo mzee.
Inawezekana udhalili na aibu uliyoamua kujivika ni sehemu muhimu ya malipo ya gharama za kulikomboa taifa letu.
pole mzee, maji yalishamwagika...sasa angalia usiendelee kuwakimbiza waliobeba nguo zako.....chutama baba yetu tafadhali utufichie aibu sisi wajukuuzo. Tafadhali ubaki na kaheshima japo kidogo babu yetu.
Hhaaa! Haya maneno yamenichoma moyo wangu ni machungu lakini basi tena Dr tutakusahau soon. Pamoja na heshima uliojijengea.kweli Samso alidanganywa na Delila.akasema siri zote.