Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa







Leo Jumanne Septemba 08, 2015 Askofu Gwajima anaongea na waandishi wa habari akitoa maelezo juu ya alichokisema Dk. Slaa wakati anaongea na waandishi wa habari pia kutoa maelezo ya uhusikaji wake kwenye tukio husika.
===========

Gwajima: Mshenga ndio huwa anatumwa na mposaji, kwa hio siri zote za mposaji anazo mshenga lakini alikosea tu kwamba, mimi kusaidia kumleta mzee Lowassa CHADEMA ni kazi ya Mungu kwa sababu Biblia inasema heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Kwa hio, kwa desturi wanasiasa huwa hawaelewani mpaka wapate mtu wa kuwaleta pamoja kwa sababu wanasiasa wanageukana muda wowote.

Kwa sababu hio mimi nilisimama pale sio kwa sababu ni bora kuliko wengine lakini kwa sababu nilikuwa mtu sahihi kwa wakati ule kuwaleta pamoja hawa wanasiasa wawili na wengin
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana GWAJIMA, umemuonesha Profesa Mihogo na yule Mke wa Mahimbo kuwa Usaliti haulipi!
 
hata wasipo onyesha ujumbe ushafika kwa wahusika na kama uyo slaa na ccm yao wanaubavu embu mamjibu mh.gwjima gwajima oyeeee mabadilikooo lowasa
 
Kiukweli nimesoma hii habari kwa utulivu na kuirudia mara mbili, lakini sijaona hoja yoyote ya msingi zaidi ya mipasho na uongo mkubwa uliotumika kumjibu Dr. Slaa! Kinachonifurahisha ni kwamba wote wanaojaribu kumjibu na kumchafua Dr. Slaa hawana hoja za msingi na wachungaji hao kama kina Gwajima ambao wanasema wanafufua watu na kuchunga kondoo wa bwana kwanini wanakuwa waongo?
 
hata wasipo onyesha ujumbe ushafika kwa wahusika na kama uyo slaa na ccm yao wanaubavu embu mamjibu mh.gwjima gwajima oyeeee mabadilikooo lowasa
Lowasaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Mabadilikooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!
 
Gwajima tunaomba usifiche kitu,weka wazi!

Nani alikutuma kufanya upatanisho huo?

Ulitumwa na
El au Dr Slaa?
Au mwingine?
 
Tanzania tuna mabishop wa kila aina
Bishop ambae hakatai kazi ya ushenga wa chama cha siasa bali anafafanua majukumu yake ya ziada
Bishop ambaye anashutumu idara ya usalama wa nchi kimzahamzaha
Bishop anajihusisha na kazi za kisiasa kindakindaki
UKAWA ndio huelewa mambo ya aina hii
 
Nimesikitika sana kuwa walinzi wa nyumbani kwa Slaa waliwekwa na Gwajima,wafanyakazi wa ndani walitoka kwa Gwajima.Gwajima anajua sehemu kubwa ya maishaya Slaa.Yaani Dr akiwa home lazima Gwajima anajua as walinzi wake ni vibaraka wa Gwajima.Kweli Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu

I never knew slaa is this much empty.. Mimi ni mpinzani wa Gwajima sikuwahi kudhani kama maisha ya mtu kama Slaa yako mikononi mwa Gwajima badala ya Mungu
 
kwani escrow, twiga kupandishwa ndege, richmond, ubadhirifu wizara ya maghufuri, epa, deep green, kagoda, tangold, vivuko vibovu, mabehewa feki, kiwira, etc, etc sio maslahi ya taifa yaliyofisadiwa. Mbona mko kimya???????? Ni wakati gani yanakuwa maslahi ya taifa?

escrow wanaendelea kushughulikiwa, suala la tembo na twiga lilishughulikiwa na bado linashughulikiwa, kuhusu richmond watu walijiuzuru na kwakuwa ni jinai watashughulikiwa, kumbuka jinai haina kikomo (no limit of time)
 
sio wote tunafanya siasa mkuu, tujali maslahi ya nchi kwanza, mtu akifikiria tofauti na chadema/ukawa mshamjudge kama ni ccm. mbona hamheshimu uhuru wa mtu? yaani ni chadema/ukawa ambao wakiona mtu amevaa jezi ya ccm wanazomea! mbona ninyi ccm hawawazomei mkiwa mmevaa jezi zenu?!, kama mnakuwa ivi hamjashika dola, mkishika dola itakuaje!

Naona sasa maji ya shingo mpaka unafikia kujikana hilooooooo
 
Gwajima nae! Sasa hii ndio nini kuvuana nguo hadharani?....mpaka underwear! Hii mbaya sana.
 
Pengine labda ni kutokana na kwamba hakuna cha maana alichokiongea Gwajima, zaidi ya kushambulia maisha binafsi ya Dk. Mihogo, ndio maana kituo bora kabisa nchini cha ITV hakijaonesha taarifa yake!

Wamekosea sana kwakuwa taarifa ni chochote ...kumbuka even a fool has a story to tell
 
Nimesikitika sana kuwa walinzi wa nyumbani kwa Slaa waliwekwa na Gwajima,wafanyakazi wa ndani walitoka kwa Gwajima.Gwajima anajua sehemu kubwa ya maishaya Slaa.Yaani Dr akiwa home lazima Gwajima anajua as walinzi wake ni vibaraka wa Gwajima.Kweli Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu
Hivi ilikuwaje, Red Brigade ikaruhusu kiongozi wa chama akalindwa na 'taasisi' nyingine wakati kwa katiba ya Chadema kazi ya usalama wa viongozi na mali za chama zinalindwa na red brigade?
Hivi ulinzi wa taasisi hii uliwekwa baada ya sakata la yule aliyetaka 'kumudhuru' Dr. Slaa?
 
Back
Top Bottom