Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Wamekosea sana kwakuwa taarifa ni chochote ...kumbuka even a fool has a story to tell

Yah Datx Tru Even A Fool Has A Story Lakin Anasikilizwa Na Mafool Wenzake..Af Acha Dharau Mzee Taarifa Sio Chochote Mbna Ukikata Gogo Taarifa Yako Haitangazwi?
 
Yah Datx Tru Even A Fool Has A Story Lakin Anasikilizwa Na Mafool Wenzake..Af Acha Dharau Mzee Taarifa Sio Chochote Mbna Ukikata Gogo Taarifa Yako Haitangazwi?

Hii nayo ni taarifa...Kumbuka even a fool has a story to tell
 
navipongeza vituo vyote vilivyoamua kupotezea mipasho ya huu ushetani usio na tija kwa wananchi. nina uhakika ukawa wamehuzunika kweli maana walivyosikia kuwa anaongea na vyombo vya habari leo basi walijiweka tayari kweli wakifikiri kuwa kuna la maana litaongelewa...matokeo yake ndiyo hayo tuliyoyaona na kuyasikia-disappointment tupu kwa ukawa.

kuna sehemu kama nilisikia amesema, ''.....kuanzia saa sita asubuhi hadi saa nane mchana!''.

hivi lile swali la yule mzee lilijibiwa kweli?!!!!! badala yake nikaona wanaukawa waliowekwa mahsusi wakimpigia makelele yule muuliza swali.

nilishangaa pale aliposema kuwa yule mama (mrs slaa) hawezekani tena hivyo hawezi kwenda kuongea naye tena, nilishangaa kweli. maana nilijiuliza, 'vp askofu amekata tamaa/ameshindwa?'

amesema lowassa alikuwa rafiki yake wakati alipokuwa ccm. kwa wenye akili hii tafsiri yake ni kwmb 1.ss c rafiki tena (kwa ushahidi tuuonao, je ni kweli?).2 anaipenda ccm.


huyu mtu ni wa kuogopwa km ukoma!!
 
ITV wanarudiaga SAA tano hizo habari pia siku hizi mitandao INA play part kubwa sana kuliko taarifa ya habari
 
Dr silaa sio mgombea kwa hivyo itv wana habari za kutosha kutuonesha,poleni ccm labda tbc wataonesha.ukawa dr silaa sio size yetu gwajima ana mtosha
 
Angalia Full video ya Mkutano wa Askofu Gwajima na Waandishi wa Habari
"Askofu Gwajima akijibu tuhuma za Dr Slaa 08/09/2015" on YouTube -
 
Last edited by a moderator:
Haya sasa CCM wamrudishe Dr. Slaa kujibu hizi hoja za Gwajima.
....hakika Gwajima kammaliza dr vibaya sana...tulishema humu kuwa dr Slaa ingekuwa vema akajinyamzia kama Lipumba baada ya kuasi chama kwa matakwa ya mke....Huku kuja kwenye media na kuropokaropoka hovyo tulisema kutawafanya watu wafunguke dhidi yake....na sasa ona wanaomjua vema wanamvua nguo hadharani babu....hii ni aibu kuu na sidhani kama dr atarudia kuropoka hadharani.....yeye akae marekani aliko na mkewe wafungiane ndani huko huko marekani kama watakavyo.....

...ahaaa ...sipati picha babu alifungiwa hata serena hotel!!....ahaaa....sasa ya nini yote hiyo???...kisa urais tu!!...yani hata uanaume unakutoka mtu!!!!!...unamshindwa mchumba tu utauweza urais na mauzauza yake????.....alafu bado dr.Slaa alimsema JK kuwa dhaifu?????....noooo....hakika huyu babu kweli naamini hata JK angekuwa bora...

......yaani mtu unahama chama na kuacha kazi zako na wafuasi wako kwa ajili ya matakwa ya mchumba????alafu unataka uwe rais wetu????...hivi huyu ana tofauti gani na usemi wa Nyerere kuhusu maamuzi ya rais yasimtegemee mkewe????


....Hivi kweli kumbe watanzania na chadema mwanzoni wangeweza kutuingizia majanga ikulu!!!....hivi hili jambo ccm wanalionaje???...wale waliompigia chapuo slaa kuwa rais (e.g Mzee Mwanakijiji)....wamemsoma Gwajima leo???.....Napata kuamini sasa kuwa hakika kweli haya yanayotokea yametokea kwa mpango wa Mungu...huyu mama mshumbusi ni shetani mbaya....na hakika nawashukuru kina Mbowe kuliona hili na kumtosa Slaa urais....duh duh!!!..ahaaaa....
 
Kiukweli, kwa sisi tunaompenda dr Slaa kiukweli kweli, tunaumia na tunamsikitia sana huyu mzee wetu.

Baada ya miaka mingi ya utumishi huku na kule, baada ya mambo mengi ya kishujaa na kujitolea, sasa hivi ndivyo maisha ya huyu mzee yanavyoishia....Total disgrace and failure of the highest order.

Hata kama, kwa move zake za sasa, kuna maslah flan hivi ya kifedha kayapata dr slaa, hata kama ni makubwa kias gan, kiukwel hayawezi kulingana na gharama na kiwango cha heshima na nafasi aliyokuwa amejijengea slaa hapa Tanzania, kwa Watanzania na dunia kwa ujumla. Dakta kadanganyika sana aisee!! kiukwel ukisikia binadam kutumika exactly kama kondomu ndo huku. kondomu huwa inatupwa kwenye shimo la choo au kumwagiwa mafuta ya taa/petrol na kuchomwa moto baada ya kumaliza ile kazi yetu.

Kosa alilofanya dakta Ni kama vile Mandela alivotoka gerezani baada ya miaka 27 eti ageuke na kusema anaungana na makaburu kuendeleza utawala wao makaburu. Hata kama angekuwa amepewa magunia ya pesa sidhani kama yangekuwa na maana yoyote kwake ukilinganisha na nafasi yake kwa nchi yake, watu wake na dunia kwa ujumla.

Kweli kina mama na kina dada ni kina mama na dada zetu na ni kweli kila penye mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke nyuma. Hata hivyo, kupitia hili, na mengine ya aina hii, ni vema pia wanaume tuwe macho kuwa baadhi ya wanawake ni viumbe khatari sana, kwa maisha na harakati za mwanaume, hasa kama tukikosea namna ya kuwa handle.

Ama kwa hakika, Kwa wale wasomaji wa biblia, hii ni stori ya kusikitisha sana ya Samsoni mwenye nguvu na mamlaka kulaghaiwa kizembe na kizezeta sana na kiumbe mwanamke.

dah, eeeh Mungu eeeeeh...well, anyway, kwaheri dakta, tumeshakupoteza!! umeachwa uchi wa mnyama.

Naandika hapa kwa uchungu sana, tunakusikitikia na kukuhurumia sana mzee wetu, lakini safari ya ukombozi lazima iendelee.

Kwa wale wasomaji na waumini wa biblia, Bwana Yesu Kristu ilibidi adhalilishwe kwa kutukanwa, kutemewa mate na makohozi, taji la miiba kichwani na mwisho kutundikwa msalabani uchi na kwa aibu kuu hadi kifo lakini mwishoni alikishinda kifo, akafufuka kutoka kaburini na kuwaletea ukombozi wa milele mamilion kwa mamilioni ya watu wamwaminio. Kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristu, Mzee wangu dakta slaa pengine usiwaze sana mzee kwa uchafu huu uliojipaka mwenyewe kwani, kama ilikuwa ni lazima ujivue nguo, na ubaki uchi hivyo, ili Taifa nzima la Tanzania likombolewe, basi na iwe hivyo mzee.

Inawezekana udhalili na aibu uliyoamua kujivika ni sehemu muhimu ya malipo ya gharama za kulikomboa taifa letu.

pole mzee, maji yalishamwagika...sasa angalia usiendelee kuwakimbiza waliobeba nguo zako.....chutama baba yetu tafadhali utufichie aibu sisi wajukuuzo. Tafadhali ubaki na kaheshima japo kidogo babu yetu.
 
Hongera Bishop kwa kuuweka upande wa pili wa shilingi na sasa nimeelewa kilicho nyuma ya pazia. Naamini umeutumia uchungaji wako pasi na kuficha neno. Mwenye kuelewa ameelewa na uamuzi u juu yake.
Rai yangu kwa ccm ni kuacha kuvuruga na kuingilia uhuru wa wapiga kura kwa kuwafundisha kutukana na kukashifiana. Athari za jambo hili ni kuleta mgawanyiko na kuuvuga umoja wetu wa kitaifa ambao ukienda kuurudisha ni gharama kubwa.
Lililopo ccm elezeni ilani yenu na acheni masuala ya ufisadi mliouanzisha na kuulea kwani hakuna mwanaukawa asilia aliyekuwapo nanyi kwa kipindi mnafisidi nchi. Ccm mnajivua nguo wenyewe na aibu yake ni ya kutisha.
Na kwa Slaa acha kutumika vibaya kwani mwisho wa ubaya ni aibu!
Barikiwa sana bishop kwa ujasiri uliouonyesha na wengine tujifunze kwako kwa kutokuwa wanafiki na waongo.
 
nasikia lowasa aliwaahidi hawa maaskofu matrion ya hela iwapo atabahatisha kuwa rais....ndo maana maaskofu wanahaha kumwingiza lowasa ikulu....
siku si nyingi mtaona press ya kakobe nae akimwaga kampeni....


Kama kila mtu akiandika na kuhutubia anachokisikia kuwa ni ukweli unafikiri tutakuwa wapi? Lazima watu wenye akili timamu wazungumze vitu wanavyovifahamu fika na sio kuzungumza kama watoto.

Huyo Lowassa ana pesa kiasi gani za kumuonga kila mtanzania katika nchi hii?

ACHENI UPUMBAVU WENU
 
Back
Top Bottom