Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Nilitamani hoja za Gwaji zijibiwe kwa hoja kinzani kuliko kumshambulia Gwaji mwenyewe,

Ukifuatilia hoja za Gwaji utagundua amezieleza kitaalamu sana japo nina uhakika Gwaji si mtaalamu wa afya

Wataalamu wetu wangetufafanulia kitaalamu ili tupate nguvu za kuondoa hoja za Gwaji kichwani

Ukiangalia waliomjibu Gwaji, wengi ni wanasiasa, hawana utaalamu wowote na wamejibu kifupi na kisiasa sana

Mfano Makamba Jr. Amesema Gwaji apuuzwe, lakini hajafafanua ni kwanini tumpuuze

Kigwangala yeye anamtaka Shekh Rashid aende akajisomee makala za kisayansi(yuko sawa lakini hajajibu swali la Shekh)

So Shekh Rashid anaweza kuwa hana hoja nzito, lakini anapojibiwa kwa hoja zisizo za msingi hoja zake zinabaki valid,

Naamini nchi hii ina wataalamu wa kutosha, watusaidie kujibu hoja za Shekh ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.
Hakika Mkuu
 
Kwani wanochanjwa hawana akili? Si wamejiridhisha? Huwezi kumtukana hivi raisi wako halafu unaangaliwa tu!!! Eti achanjwe zote milioni moja!!! Who is Gwajima to us? Kwani yeye kuwa ni msemaji wetu watanzania? Is he a scientist? a pharmasist? Ni mtaalam wa nini hasa? Who is he? is he a preacher? He claimed to resurrect, why did he not resurrect our president? Was he there when the vaccine was being manufactured? Huyu ni mjanja fulani tu anayejua kuongea na kupotosha watu!!! Hii theory kwamba wazungu wanataka kutumaliza, hivi mzungu akitaka kutumaliza lazima atumie chanjo itakayompoint moja kwa moja? Tunatumia kila kitu cha wazungu kwanini hawatumalizi kupitia vitu vyao tunavyovitumia? Why all the trouble kutengeneza chanjo when they can finish us in an instant with no hussle!!!!
Mkuu elewa kuwa zana ya kumalizwa Haufi leoleo ... Ila kuna vitu MUHIMU vya utu wako vinaondoka taratibu MIAKA Hadi MIAKA. . na vizazi vyote vinavyofuata vitakuwa vinapata CHANJO hii kama ilivyo Ndui na nyinginezo ambayo hupigwa mtoto mara anapozaliwa
 
Mkuu hawa watu wanatia hasira mno. Gwajima ni mhuni mmoja anayecheza na mindset finyu za baadhi ya watu tu. Hana lolote. Unamsikia anasema etu mtu akitaka kumuua yeye huyo mtu anaangamia kabla yake. Yaani kile kitendo cha kufikiria tu kumfanyia jambo baya, basi wewe unakuwa umeshajimaliza mwenyewe. Anajifanya yeye ni masiha mpakwa mafuta. Sidhani kama Mungu anaweza kuwa na ukaribu na mtu wa aina hii!
Tujibu HOJA zake za msingi
 
Ameandika Pastor Dr.Zakayo Nzogere (PhD), Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la MICC Mwanza.

Pamekuwa na matamko mengi yanayokinzana kutoka kwa watumishi wa Mungu kuhusu UVIKO19.

Wapo wanaosema ni maandalizi ya “Mpinga Kristo” na alama ya Mnyama 666; na wengine wakisema ni mlipuko wa kawaida usio na uhusiano wowote wa kiimani.

USHAURI WANGU KWA WATUMISHI WENZANGU;

1. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi tuna majibu ya kila jambo kila wakati.

2. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi kila unachokiamini, unachokisema, au kukifiria basi kimetoka kwa Mungu. Mambo mengine ni utashi binafsi unaotokana na taarifa ulizonazo.

3. Kuwa Mtumishi wa Mungu haikupi mamlaka ya kuwafanyia wafuasi wako maamuzi binafsi. Hata Mungu mwenyewe anatutaka tuchague kati ya uzima na mauti; hatulazimishi (Kumbukumbu 30:19).

4. Kuchukua tahadhari siyo kukosa Imani. Kuna wakati Yesu alichukua tahadhari ya kutoingia Yerusalemu waziwazi kwa sababu kuna watu walitaka kumuua; hivyo akaingia kwa siri (Yohana 7:1-10). Si kwamba aliogopa kufa; bali hakutaka kufa kabla ya kutimiza kazi iliyomleta.

Wayahudi walipotaka kumuua Mtume Paulo alitoroshwa mjini kwa kushushwa na KAPU (Matendo 9:25); hebu fikiria Mtumishi wa Mungu kujificha kwenye kapu.

5. Ni sahihi Mtumishi wa Mungu kuwa na msimamo binafsi kuhusu mambo tofauti, lakini si sahihi KUMUINGIZA MUNGU kwenye misimamo binafsi.

Mtume Paulo anatusaidia kwenye kutoa matamko ambayo sio maagizo ya Mungu moja kwa moja, kwa kuweka wazi mara zote anapotoa mtazamo binafsi juu ya jambo fulani:

1Korintho 7:6 (NEN) “Nasema haya kama ushauri na si amri”

1Korintho 7:12 (NEN) “Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila mimi)..”

MIMI NAAMINI YAFUATAYO:

1. Covid19 ni janga la kawaida na litapita.

2. Chanjo ya Covid haina athari zozote za kiroho kwa Mkristo.

3. Hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu wala kugeuza imani yetu.

4. Ni sahihi Wakristo kuchukua tahadhari zote za kiafya kama tunavyoelekezwa na wataalamu.

NB: Mtu akisema tahadhari dhidi ya UVIKO ni kukosa Imani; muulize kwanini anafunga mkanda kwenye gari? Kwanini anavaa kofia ngumu kwenye pikipiki? Au kwanini ameweka chandarua chumbani? Zote hizo ni tahadhari, sio ukosefu wa imani.!
Mtumishi ... Taahadhari ZOTE zinazingatiwa lakini sio kila taadhari ni rafiki . Ndio maana Mungu amesisitiza tuishike sana elimu ili tusije tukaangamia kwa kukosa maarifa.
Kwahiyo sio kila mahala Mungu atajitokeza kukuokoa, la hasha kuna sehemu atataka utumie elimu uliyonayo kujinasua wewe mwenyewe.
Rejea kitabu Cha UFUNUO WA YOHANA .. soma mwanzo mwisho... Halafu oanisha na hali inayoendelea sasa.
 
Ameandika Malisa GJ.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu chanjo ya Corona katika nchi nyingi za Afrika. Baadhi ya viongozi wa dini wamedai chanjo hiyo inalenga kupunguza idadi ya watu weusi kwa kuwazuia kuzaliana, na wengine wameihusisha na chapa ya 666 inayodaiwa kuwa ya Mpinga Kristo.

Kufuatia madai hayo mwanaharakati Tracy Zille wa Afrika Kusini ameandika maoni yafuatayo (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);
_________
Waafrika wanapaswa kuwa watu wa mwisho kulalamika kuhusu chanjo ya Corona. Kama kweli wazungu wangetaka kuwaua wangeshafanya hivyo miaka mingi iliyopita. Vinywaji vingi vinatoka Ulaya, hadi maziwa ya watoto. Wangetaka kuwaua wasingekua na haja ya kusubiri chanjo ya Corona.

Kitu kikubwa waafrika wanachoweza kutengeneza ni watoto wasio na mpangilio baada ya kufanya ngono kienyeji. Tulieni, hakuna mtu mwenye mpango wa kuwaua. Nyie sio muhimu sana wala sio tishio kwa dunia kiasi cha kutaka kuwaua.

Kama hamtaki chanjo yetu basi tengenezeni yenu. Lakini kama hamuwezi kutengeneza kondomu wala miswaki, mtaweza kweli kutengeneza chanjo ya corona? Hadi vichokoa meno (toothpick) mnaagiza China halafu mko busy kutukana wazungu eti wanataka kuwaua?

Jifunzeni angalau kutengeneza condom kwanza kabla hamjapiga kelele zisizo na msingi kuhusu chanjo ya Corona. Dawa nyingi mnazotumia katika hospitali zenu ni kutoka Ulaya, lakini leo mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua kupitia chanjo ya Corona.

Hata chupi mnazovaa zimetoka nje ya Afrika. Kama sio kutoka China basi ni mitumba kutoka Ulaya na Marekani. Hamuwezi kutengeneza hata chupi za kusitiri maungo yenu lakini mko "busy" kutukana wazungu wanaoumiza vichwa vyao kutengeneza chanjo ya corona.

Hamuwezi hata kutengeneza dawa rahisi ya kutuliza maumivu ya kichwa kama Panadol, lakini mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua. Sasa uamuzi ni wenu. Kuikubali chanjo ya corona mpone, au muikatae mfe kwa ujinga wenu.

Kama sio wazungu midomo yenu ingekua inanuka kama maiti ya panya kwa sababu hamuwezi kutengeneza hata dawa ya meno. Colgate inatengenezwa Marekani, Aquafresh Uingereza, Mentadent Canada, Sensodyne Japan. Tungetaka kuwaua si tungeshawamaliza siku nyingi? Kwanini tusubiri kuja kuwaua kupitia chanjo ya corona?

Tunatengeneza wanasayansi wa kuisaidia dunia, nyie mko busy kutengeneza Mitume na Manabii matajiri. Tunatengeneza chanjo ya corona nyie mnatengeneza mafuta ya upako. Halafu mnasema tunataka kuwaua. Wajinga nyie.

Hata dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKWIMWI (ARVs) zinatoka Ulaya na Marekani. Sasa kama kweli wazungu wanataka kuwaua waafrika si wangeshawamaliza kupitia ARVs? Unakuta mwafrika amekondeana kwa UKIMWI lakini akishameza ARVs za wazungu akapata afya anasema eti wazungu wamebuni chanjo ya Corona ili kuua waafrika. Upumbavu gani huu?

Msinitukane kwa kuwaeleza ukweli. Tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vikuu (Chuo kikuu UDSM kilijengwa mwaka 1961 na JF Kennedy, Chuo kikuu cha Zambia kilijengwa na Harold Wilson mwaka 1996, Chuo kikuu Nairobi kilijengwa na Anthony Eden mwaka 1956 kikiitwa Royal Technical College).

Hiyo ni mifano tu lakini tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vingi na vituo vingi vya utafiti. Nyie mnatumia pesa zenu kujenga makanisa makubwa na kuwanunulia Mitume na Manabii magari ya kifahari.

Vituo vyetu vya utafiti vimebuni chanjo za magonjwa makubwa kama surua, polio, tetekuwanga, ndui, homa ya ini etc. Vituo vyenu vya mitume na manabii vimebuni mafuta ya upako. Mnanunua mafuta ya upako kwa gharama kubwa bila kupiga kelele, lakini chanjo ya corona mnayopewa bure mnapanua midomo kuitukana. Mna mdudu kichwani, si bure.

Halafu hii sio chanjo ya kwanza kuwaletea huko Afrika. Tumeleta chanjo nyingi na mmezitumia bila kelele. Chanjo za polio, surua, homa ya ini, tetekuwanga etc. Tungetaka kuwaua si tungetumia chanjo hizo? Kwanini tusubirie ya corona?

Baadhi ya nchi za Afrika mmeanza kuharibu miundombinu ya teknolojia ya 5G kwa kuihusisha na Corona. Hili si jambo la kushangaza kwa sababu mnaua hadi mama zenu wa kuwazaa kwa kuwahusisha na uchawi. Kwa sababu tu ya ngozi zao kusinyaa kwa uzee na macho yao kuwa mekundu kwa kutumia nishati ya kuni, kwenu huo ni ushahidi wa uchawi. Mnawaua bila huruma.

Muda si mrefu mtaanza kuwaua wagonjwa wa Corona kwa kuhisi wamelogwa au wametupiwa mkosi. Haya ndio mawazo ya watu wapumbavu, wasioelimika na washamba kama nyie. Watu ambao mnaamini eti kila nyumba ya tajiri ina chumba maalumu cha kufuga majoka yanayomletea hela.

Sikikizeni nyie wapumbavu. Kama chanjo ya Corona ingegunduliwa Afrika, viongozi wenu wasingeitumia. Wangesafiri kwenda India au nchi za Ulaya kutafuta chanjo nyingine.

Viongozi wa Afrika hawaamini katika huduma za afya za nchi zao. Hawaamini hospitali zao, hawaamini madaktari wao, hawaamini hata dawa zao. Ndio maana wakiugua hata malaria tu wanapanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwahiyo wakati mkiwaza eti wazungu wanataka kuwaua kwa chanjo ya corona, viongozi wenu nao wanawaza mnataka kuwaua kwa huduma mbovu za afya. Ndio maana wanajenga hospitali lakini hawatibiwi humo, wanasomesha madaktari lakini hawawaamini. Wanakimbilia kutibiwa nje. Wanajenga shule lakini watoto wao hawasomi humo.

Chanjo ya Corona ni kengele ya kuwakumbusha waafrika kuchagua viongozi wenye maono na uwezo wa kupambana na matatizo yao. Afrika ingekuwa na uongozi thabiti ingekua bara tajiri zaidi duniani. Lakini kwa sababu ya ujinga wenu wa kuchagua viongozi wasio na maono, wameuza rasilimali zenu kwa wazungu na Wachina, kwa faida yao na familia zao, huku wananchi mkiteseka kwa umaskini.

Utajiri mwingi wa Ulaya, Marekani na China umetoka Afrika kwa sababu ya upumbavu wa viongozi wenu. Badilikeni. Kabla hamjalaumu wazungu, jilaumuni kwanza wenyewe kwa kuchagua viongozi goigoi.!

Nini maoni yako?
AS RECIEVED
ni Upumbavu mtupu, kabla ya wazungu kuja Africa kwani waafrica walikua hawana maisha?
 
ni Upumbavu mtupu, kabla ya wazungu kuja Africa kwani waafrica walikua hawana maisha?
Unapata na jeuri, kwa kutumia vifaa vya wazungu.achaneni na vitu vyao sasa mrudi yale maisha ya porini.

Watu ambao hata vyao vya shule, kukata magovi huko usukumani bado mnapata msaada wa wazungu.halafu mnaanza kutunisha vifua[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Haimaanishi hatuwezi kuishi bila hivyo, Kama itafika wakati tuuze utu wetu ili tutumie hivyo vitu vyao, nitakuwa wa kwanza kuachana navyo
 
Akijulikana kama askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye kwasasa ndio Mbunge wa Kawe si mara ya kwanza kuingia kwenye mitifuano na serikali.

Ana kesi nyingi pia ambazo mwisho wake una utata

Ana kashfa nyingi pia

Ni aina ya mtu ambaye sidhani kama ana mshipa wa soni. Ni kinyonga na hachelei kugeuza maneno

Ni kwanini baada ya yote hayo anapeta tu?

Jibu ni moja tu. Walimuamini wakamtumia katika shida zao mbalimbali za kijamii, mahusiano, siasa, kiroho na hata kifedha..anawajua nje ndani.

Amebeba siri zao nyingi sana, anawajua na kuwafahamu kwa mengi mema na mabaya. Kamwe hawawezi kumgusa.

Atafanya atakavyo, atasema atakavyo lakini watafunika kombe tu mwanaharamu apite. Amewafanya kama mateka wake. Anawatumia atakavyo, Dr. Slaa anamjua vema huyu.

Kama ukweli ni tofauti na huu. Basi naamini atachukuliwa hatua walau za kupewa karipio la wazi. Hebu msikize hapo[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

View attachment 1872360

Kuna mtu mmoja tu ndio alikuwa na uthubutu wa kumsema waziwazi. Naye si mwingine bali ni Mzee Makamba[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Huyo ni kibwetere tu kama vibwetere wengine😂😂😂
 
Tusitishane kama covid nmeugua mimea tiba yaani vitamin C zimeniponya na nipo fit! We kachomwe usichokijua ambacho wenzako wanachomwa na bado wanakufa kama kuku.
Arafu hii johnson inapigwa vita, marekani imeleta shida. Tuagarie mbadala wa another vaccine
 
Basi tuna serikali ya ajabu kuwahi kutokea
Basi tuna serikali ya ajabu kuwahi kutokea
Nasikia pale Zenji mwaka jana uchaguzi serikali ilikodi wajeda wa kirundi ili kuua wana harakati watakao pinga matokeo ya uchaguzi!!TUNADAIWA NDIO MAANA NAMBA MOJA HADI TATU WALIFANYA ZIARA KWA WARUNDI WASIJE CHOMOA WAYA WA BETRI DUNIA IKAJUA!!!moja ya maajabu pia au sio???!!!
 
Akijulikana kama askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye kwasasa ndio Mbunge wa Kawe si mara ya kwanza kuingia kwenye mitifuano na serikali.

Ana kesi nyingi pia ambazo mwisho wake una utata

Ana kashfa nyingi pia

Ni aina ya mtu ambaye sidhani kama ana mshipa wa soni. Ni kinyonga na hachelei kugeuza maneno

Ni kwanini baada ya yote hayo anapeta tu?

Jibu ni moja tu. Walimuamini wakamtumia katika shida zao mbalimbali za kijamii, mahusiano, siasa, kiroho na hata kifedha..anawajua nje ndani.

Amebeba siri zao nyingi sana, anawajua na kuwafahamu kwa mengi mema na mabaya. Kamwe hawawezi kumgusa.

Atafanya atakavyo, atasema atakavyo lakini watafunika kombe tu mwanaharamu apite. Amewafanya kama mateka wake. Anawatumia atakavyo, Dr. Slaa anamjua vema huyu.

Kama ukweli ni tofauti na huu. Basi naamini atachukuliwa hatua walau za kupewa karipio la wazi. Hebu msikize hapo[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

View attachment 1872360

Kuna mtu mmoja tu ndio alikuwa na uthubutu wa kumsema waziwazi. Naye si mwingine bali ni Mzee Makamba[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Hapo ndipo penye hekima kila mtu kwa imani yake kumuomba Mungu maamuzi sahihi,maana nae Gwajima ni binadamu kama binadamu yoyote.Ni maoni yake tuu!
 
Nasikia pale Zenji mwaka jana uchaguzi serikali ilikodi wajeda wa kirundi ili kuua wana harakati watakao pinga matokeo ya uchaguzi!!TUNADAIWA NDIO MAANA NAMBA MOJA HADI TATU WALIFANYA ZIARA KWA WARUNDI WASIJE CHOMOA WAYA WA BETRI DUNIA IKAJUA!!!moja ya maajabu pia au sio???!!!
Mungu wangu[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Nilitamani hoja za Gwaji zijibiwe kwa hoja kinzani kuliko kumshambulia Gwaji mwenyewe,

Ukifuatilia hoja za Gwaji utagundua amezieleza kitaalamu sana japo nina uhakika Gwaji si mtaalamu wa afya

Wataalamu wetu wangetufafanulia kitaalamu ili tupate nguvu za kuondoa hoja za Gwaji kichwani

Ukiangalia waliomjibu Gwaji, wengi ni wanasiasa, hawana utaalamu wowote na wamejibu kifupi na kisiasa sana

Mfano Makamba Jr. Amesema Gwaji apuuzwe, lakini hajafafanua ni kwanini tumpuuze

Kigwangala yeye anamtaka Shekh Rashid aende akajisomee makala za kisayansi(yuko sawa lakini hajajibu swali la Shekh)

So Shekh Rashid anaweza kuwa hana hoja nzito, lakini anapojibiwa kwa hoja zisizo za msingi hoja zake zinabaki valid,

Naamini nchi hii ina wataalamu wa kutosha, watusaidie kujibu hoja za Shekh ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.
Umeambiwa ukitaka kachanje kama hutaki acha, bado wawashwa wapi?
 
Back
Top Bottom