Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Gwajima alieleza uelewa au hisia zake na nampongeza Sana kwa Hilo,

Serikali au watu wanaotofautiana nae walitakiwa kuja na hoja ili kupangua wasiwasi wake na kwa wengine. Shida inaanzia pale tunapoangalia Nani kasema badala ya kuangalia Nini kasema.

Wizara na viongozi wake walitakiwa si kuanzisha marumbano naye ambayo muda mwingine wao ndo wanajidhalilisha. Dk Mollel Nani hajui kiki iliyompa Unaibu kipindi Cha Mwendazake, Nani hajui Dk Gwajima alivyokuwa anatetea kujifukiza kuliko miongozo ya WHO.....!

Gwajima amebaki kule ambako watanzania wengi walipelekwa kipindi kile hivyo naye anahitaji elimu na ufafanuzi mzuri ili naye abadili mawazo kama walivyofanya Dk. Gwajima na Mollel.

Mtu sahihi ambaye anaweza kusimama akaueleza Umma bila unafiki kwa wanasiasa ni Dk Ndungulile, huyu hakukubali kuaminishwa ambacho hakiamini na kilicho tofauti na taaluma yake.
Heko
 
Hoja hapa chanjo inazuia nisipate korona? Jibu ni HAPANA unapata! Je chanjo hii inazuia nikiwa na korona nisimuambukize mwingine? Jibu ni HAPANA unawezakumwambukiza! Je nikichanjwa nikapata korona siwezi kufa! Jibu ni HAPANA unawezakufa! Je hayo MACHANJO ni ya nn? JIBU yanazuia maambukizi ya KORONA. Mbona waliochanjwa Ulaya wanazidi kupukutika kwa kasi?🤔 Tuwe na ngozi nyeusi na AKILI iwe nyeusi huo ni upimbi.
 
Kawazid ufaaham vingoz wengi sana na atawasumbua sana sipati picha na tundulisu angekuwepo bungeni 😅😂😂 Vilazaa wangee Aga wenyewe
 
Akijulikana kama askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye kwasasa ndio Mbunge wa Kawe si mara ya kwanza kuingia kwenye mitifuano na serikali.

Ana kesi nyingi pia ambazo mwisho wake una utata

Ana kashfa nyingi pia

Ni aina ya mtu ambaye sidhani kama ana mshipa wa soni. Ni kinyonga na hachelei kugeuza maneno

Ni kwanini baada ya yote hayo anapeta tuu?

Jibu ni moja tu. Walimuamini wakamtumia katika shida zao mbalimbali za kijamii, mahusiano, siasa, kiroho na hata kifedha..anawajua nje ndani.

Amebeba siri zao nyingi sana, anawajua na kuwafahamu kwa mengi mema na mabaya. Kamwe hawawezi kumgusa.

Atafanya atakavyo, atasema atakavyo lakini watafunika kombe tu mwanaharamu apite. Amewafanya kama mateka wake. Anawatumia atakavyo, Dr. Slaa anamjua vema huyu.

Kama ukweli ni tofauti na huu. Basi naamini atachukuliwa hatua walau za kupewa karipio la wazi. Hebu msikize hapo[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

View attachment 1872360

Kuna mtu mmoja tu ndio alikuwa na uthubutu wa kumsema waziwazi. Naye si mwingine bali ni Mzee Makamba[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Kile ni kichwa Cha kisukuma mtapata shida Sana kumkamata labda mtumie mabavu kwa sababu yeye anachozungumza ni fact with evidence

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Gwajima anamlilia baba yake, anaona legacy inapotezwa. Hataacha kulia akikumbuka aliunda genge la kupoteza wanaomkosoa baba yake hata akapewa ubunge anaona hana namna yaa kumshukuru zaidi ya kuenzi mawazo yake. Hakuna namna ,, mwache aendelee kulialia. Kwanza chanjo hazitutoshi wote, watakaoshawishika na gwajima watasaidia kufanya zitoshe.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nilitamani hoja za Gwaji zijibiwe kwa hoja kinzani kuliko kumshambulia Gwaji mwenyewe,

Ukifuatilia hoja za Gwaji utagundua amezieleza kitaalamu sana japo nina uhakika Gwaji si mtaalamu wa afya

Wataalamu wetu wangetufafanulia kitaalamu ili tupate nguvu za kuondoa hoja za Gwaji kichwani

Ukiangalia waliomjibu Gwaji, wengi ni wanasiasa, hawana utaalamu wowote na wamejibu kifupi na kisiasa sana

Mfano Makamba Jr. Amesema Gwaji apuuzwe, lakini hajafafanua ni kwanini tumpuuze

Kigwangala yeye anamtaka Shekh Rashid aende akajisomee makala za kisayansi(yuko sawa lakini hajajibu swali la Shekh)

So Shekh Rashid anaweza kuwa hana hoja nzito, lakini anapojibiwa kwa hoja zisizo za msingi hoja zake zinabaki valid,

Naamini nchi hii ina wataalamu wa kutosha, watusaidie kujibu hoja za Shekh ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.
 
Kwani wanochanjwa hawana akili? Si wamejiridhisha? Huwezi kumtukana hivi raisi wako halafu unaangaliwa tu!!! Eti achanjwe zote milioni moja!!! Who is Gwajima to us? Kwani yeye kuwa ni msemaji wetu watanzania? Is he a scientist? a pharmasist? Ni mtaalam wa nini hasa? Who is he? is he a preacher? He claimed to resurrect, why did he not resurrect our president? Was he there when the vaccine was being manufactured? Huyu ni mjanja fulani tu anayejua kuongea na kupotosha watu!!! Hii theory kwamba wazungu wanataka kutumaliza, hivi mzungu akitaka kutumaliza lazima atumie chanjo itakayompoint moja kwa moja? Tunatumia kila kitu cha wazungu kwanini hawatumalizi kupitia vitu vyao tunavyovitumia? Why all the trouble kutengeneza chanjo when they can finish us in an instant with no hussle!!!!
Who is Gwajima to us? Kwani yeye kuwa ni msemaji wetu watanzania? Is he a scientist? a pharmasist? Ni mtaalam wa nini hasa? Who is he? is he a preacher? He claimed to resurrect, why did he not resurrect our president? Was he there when the vaccine was being manufactured? Huyu ni mjanja fulani tu anayejua kuongea na kupotosha watu!!![emoji736][emoji1545][emoji817]
 
Back
Top Bottom