Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Akijulikana kama askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye kwasasa ndio Mbunge wa Kawe si mara ya kwanza kuingia kwenye mitifuano na serikali.

Ana kesi nyingi pia ambazo mwisho wake una utata

Ana kashfa nyingi pia

Ni aina ya mtu ambaye sidhani kama ana mshipa wa soni. Ni kinyonga na hachelei kugeuza maneno

Ni kwanini baada ya yote hayo anapeta tu?

Jibu ni moja tu. Walimuamini wakamtumia katika shida zao mbalimbali za kijamii, mahusiano, siasa, kiroho na hata kifedha..anawajua nje ndani.

Amebeba siri zao nyingi sana, anawajua na kuwafahamu kwa mengi mema na mabaya. Kamwe hawawezi kumgusa.

Atafanya atakavyo, atasema atakavyo lakini watafunika kombe tu mwanaharamu apite. Amewafanya kama mateka wake. Anawatumia atakavyo, Dr. Slaa anamjua vema huyu.

Kama ukweli ni tofauti na huu. Basi naamini atachukuliwa hatua walau za kupewa karipio la wazi. Hebu msikize hapo



Kuna mtu mmoja tu ndio alikuwa na uthubutu wa kumsema waziwazi. Naye si mwingine bali ni Mzee Makamba
 
Gwajiboy,mtu mwenye ushawishi sana.Kwa Chadema Kabla hajasepa na KWA CCM.
In short ana PHD ya ushawishi na si Zaid.
Lakini pia Huyu nafikiri ni group letu lileeee la TIES-ES
Ninakukumbuka baada ya ile kesi ya kuwa kwenye orodha ya ng’anda na kuwekwa ndani. Wanakwaya wake walikwenda kuimba nje ya Central Police Station. Mwendazake went mad.
 
Haya yote yanaibuka kwa sababu anaeleza anachokiamini, na ambacho dunia nzima inakijua juu ya hiki mnachokiita chanjo? Hivi ni kweli ninyi mnataka kuniambia hamjasoma utata uliopo kwenye hizi chanjo za mwendokasi?...
Kama hujui tafsiri ya kitu si vema kukitumia utaonekana kituko mbele za watu

LOW MINDSETS DISCUSS PEOPLE, MIDIUM MINDSETS DISCUSS EVENTS BUT HIGH MINDSETS DISCUSSE ISSUES
 
Kama hujui tafsiri ya kitu si vema kukitumia utaonekana kituko mbele za watu

LOW MINDSETS DISCUSS PEOPLE, MIDIUM MINDSETS DISCUSS EVENTS BUT HIGH MINDSETS DISCUSS ISSUES
Leo wanaume wazima tuanze kuimbishwa taarabu za kumwongelea mtu kijinga kijinga wakti hatuna hata misingi ya kitaalam ya kumpinga hoja zake. Etu tunaanze kumtukana, kumpa majina badala ya kuongelea hoja. Ni zaidi ya kituko!.
 
Hili linaaply kwako pia. Wewe unajua ulozi. Habari zingine ukiziingilia, unaonekana kituko.
IMG-20210729-WA0040.jpg
 
Gwajima alieleza uelewa au hisia zake na nampongeza Sana kwa Hilo,

Serikali au watu wanaotofautiana nae walitakiwa kuja na hoja ili kupangua wasiwasi wake na kwa wengine. Shida inaanzia pale tunapoangalia Nani kasema badala ya kuangalia Nini kasema.

Wizara na viongozi wake walitakiwa si kuanzisha marumbano naye ambayo muda mwingine wao ndo wanajidhalilisha. Dk Mollel Nani hajui kiki iliyompa Unaibu kipindi Cha Mwendazake, Nani hajui Dk Gwajima alivyokuwa anatetea kujifukiza kuliko miongozo ya WHO.....!

Gwajima amebaki kule ambako watanzania wengi walipelekwa kipindi kile hivyo naye anahitaji elimu na ufafanuzi mzuri ili naye abadili mawazo kama walivyofanya Dk. Gwajima na Mollel.

Mtu sahihi ambaye anaweza kusimama akaueleza Umma bila unafiki kwa wanasiasa ni Dk Ndungulile, huyu hakukubali kuaminishwa ambacho hakiamini na kilicho tofauti na taaluma yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom