Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Gwajima ni mtu mmoja care xana then anafuata nyanyo za magufuri na akigombea uraisi lazima nimpitishe next time
Mbowe chanjo iwe ya lazima

Uvccm Huyu Mbowe asitupangie akachanje yy na familia yake huko,hatuchanji.

Gwajima Hii chanjo ina mapungufu,si salama.

Uvccm Huyu Gwajima anapotosha watu,tunalaani.

[emoji42][emoji2][emoji2214][emoji2214][emoji2214]
 
Na pia ukweli ni kwamba mataifa yote ambayo yametoa chanjo vifo vinapungua.
Corona inakwenda kuwa gonjwa la Africa kwa ujinga wetu kama ambavyo ukimwi unatuhenyesha.
Kuna mdudu kwenye bongo zetu si bure.
Ni kweli ukichanjwa unaugua corona lakini ukali wake ni sawa na ambaye hajachanjwa? Chanjo inasaidia kupunguza ukali wa corona kufikia level ya mafua ya kawaida.
Kweli kabisa mkuu. Mfano mzuri marekani. Tokea Joe Biden aingie na kuharakisha kushughulikia covid 19 vifo vimepungua sana baada ya kuwapa wananchi wao chanjo. Ila hapa kwetu watu wengi sana mpaka wasomi wanaamini mabeberu wanataka kutuua!!! Yaani mzungu akitaka kutuwipe out hahitaji kutengeneza chanjo. Anatuua kupitia vitu vyao tunavyovitumia. kila kitu chetu tunachotumia ni cha mzungu!!!! Ndiyo maana Mungu anasikitika sana anasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa". Mtu mweusi hana maarifa kabisa. Eti chapa ya 666!!! Kuogopesha watu tu!!!!
 
Hili linaaply kwako pia. Wewe unajua ulozi. Habari zingine ukiziingilia, unaonekana kituko.
Mshana jr yuko sahihi. We humjui Gwajiboy.
Mi namjua wakati anaanza tu mambo ya kanisa, alikuwa anakuja kutumia internet kwenye cafe yetu mara kwa mara pale ubungo juu pale ukianza kupanda kilima yeye alikuwa na kanisa dogo tu pale ilipokuwa hunters club/ bar pale ubungo alikuwa hajaanza kabisa mambo ya kufufua watu.

Aliwai kuwa na kesi kubwa iliyomsumbua sana ya kuuza magari kwa kutumia kipengere cha kufutiwa kodi taasisi za kanisa. Aliifuta ki aina.

Wakati anafufua watu yuko maarufu sana alifanya kitu cha kushangaza kilichosababisha rafiki yangu ahame kanisa lake.
Kuna jamaa alikuwa anataka kuoa , yeye akamweka sawa yule jamaa asioe mchumba wake, badala yake Gwajiboy akamuunganisha na dada yake yeye Gwajiboy.

Ana vijimambo vingi ambavyo havitoki nje.
Sasa nyie mnamwita mtumishi wa Mungu.

Ni mtu pumbafu sana kwa ujumla. Hana cha TISS wala nini, anajua kuna watu wanamsikiliza.
 
Mshana jr yuko sahihi. We humjui Gwajiboy.
Mi namjua wakati anaanza tu mambo ya kanisa, alikuwa anakuja kutumia internet kwenye cafe yetu mara kwa mara pale ubungo juu pale ukianza kupanda kilima yeye alikuwa na kanisa dogo tu pale ilipokuwa hunters club/ bar pale ubungo alikuwa hajaanza kabisa mambo ya kufufua watu.

Aliwai kuwa na kesi kubwa iliyomsumbua sana ya kuuza magari kwa kutumia kipengere cha kufutiwa kodi taasisi za kanisa. Aliifuta ki aina.

Wakati anafufua watu yuko maarufu sana alifanya kitu cha kushangaza kilichosababisha rafiki yangu ahame kanisa lake.
Kuna jamaa alikuwa anataka kuoa , yeye akamweka sawa yule jamaa asioe mchumba wake, badala yake Gwajiboy akamuunganisha na dada yake yeye Gwajiboy.

Ana vijimambo vingi ambavyo havitoki nje.
Sasa sie mnamwita mtumishi wa Mungu.

Ni mtu pumbafu sana kwa ujumla. Hana cha TISS wala nini, anajua kuna watu wanamsikiliza.
Ni mtu pumbafu sana kwa ujumla. Hana cha TISS wala nini, anajua kuna watu wanamsikiliza.[emoji736][emoji817][emoji1545]
 
Ameandika Malisa GJ.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu chanjo ya Corona katika nchi nyingi za Afrika. Baadhi ya viongozi wa dini wamedai chanjo hiyo inalenga kupunguza idadi ya watu weusi kwa kuwazuia kuzaliana, na wengine wameihusisha na chapa ya 666 inayodaiwa kuwa ya Mpinga Kristo.

Kufuatia madai hayo mwanaharakati Tracy Zille wa Afrika Kusini ameandika maoni yafuatayo (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);
_________
Waafrika wanapaswa kuwa watu wa mwisho kulalamika kuhusu chanjo ya Corona. Kama kweli wazungu wangetaka kuwaua wangeshafanya hivyo miaka mingi iliyopita. Vinywaji vingi vinatoka Ulaya, hadi maziwa ya watoto. Wangetaka kuwaua wasingekua na haja ya kusubiri chanjo ya Corona.

Kitu kikubwa waafrika wanachoweza kutengeneza ni watoto wasio na mpangilio baada ya kufanya ngono kienyeji. Tulieni, hakuna mtu mwenye mpango wa kuwaua. Nyie sio muhimu sana wala sio tishio kwa dunia kiasi cha kutaka kuwaua.

Kama hamtaki chanjo yetu basi tengenezeni yenu. Lakini kama hamuwezi kutengeneza kondomu wala miswaki, mtaweza kweli kutengeneza chanjo ya corona? Hadi vichokoa meno (toothpick) mnaagiza China halafu mko busy kutukana wazungu eti wanataka kuwaua?

Jifunzeni angalau kutengeneza condom kwanza kabla hamjapiga kelele zisizo na msingi kuhusu chanjo ya Corona. Dawa nyingi mnazotumia katika hospitali zenu ni kutoka Ulaya, lakini leo mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua kupitia chanjo ya Corona.

Hata chupi mnazovaa zimetoka nje ya Afrika. Kama sio kutoka China basi ni mitumba kutoka Ulaya na Marekani. Hamuwezi kutengeneza hata chupi za kusitiri maungo yenu lakini mko "busy" kutukana wazungu wanaoumiza vichwa vyao kutengeneza chanjo ya corona.

Hamuwezi hata kutengeneza dawa rahisi ya kutuliza maumivu ya kichwa kama Panadol, lakini mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua. Sasa uamuzi ni wenu. Kuikubali chanjo ya corona mpone, au muikatae mfe kwa ujinga wenu.

Kama sio wazungu midomo yenu ingekua inanuka kama maiti ya panya kwa sababu hamuwezi kutengeneza hata dawa ya meno. Colgate inatengenezwa Marekani, Aquafresh Uingereza, Mentadent Canada, Sensodyne Japan. Tungetaka kuwaua si tungeshawamaliza siku nyingi? Kwanini tusubiri kuja kuwaua kupitia chanjo ya corona?

Tunatengeneza wanasayansi wa kuisaidia dunia, nyie mko busy kutengeneza Mitume na Manabii matajiri. Tunatengeneza chanjo ya corona nyie mnatengeneza mafuta ya upako. Halafu mnasema tunataka kuwaua. Wajinga nyie.

Hata dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKWIMWI (ARVs) zinatoka Ulaya na Marekani. Sasa kama kweli wazungu wanataka kuwaua waafrika si wangeshawamaliza kupitia ARVs? Unakuta mwafrika amekondeana kwa UKIMWI lakini akishameza ARVs za wazungu akapata afya anasema eti wazungu wamebuni chanjo ya Corona ili kuua waafrika. Upumbavu gani huu?

Msinitukane kwa kuwaeleza ukweli. Tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vikuu (Chuo kikuu UDSM kilijengwa mwaka 1961 na JF Kennedy, Chuo kikuu cha Zambia kilijengwa na Harold Wilson mwaka 1996, Chuo kikuu Nairobi kilijengwa na Anthony Eden mwaka 1956 kikiitwa Royal Technical College).

Hiyo ni mifano tu lakini tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vingi na vituo vingi vya utafiti. Nyie mnatumia pesa zenu kujenga makanisa makubwa na kuwanunulia Mitume na Manabii magari ya kifahari.

Vituo vyetu vya utafiti vimebuni chanjo za magonjwa makubwa kama surua, polio, tetekuwanga, ndui, homa ya ini etc. Vituo vyenu vya mitume na manabii vimebuni mafuta ya upako. Mnanunua mafuta ya upako kwa gharama kubwa bila kupiga kelele, lakini chanjo ya corona mnayopewa bure mnapanua midomo kuitukana. Mna mdudu kichwani, si bure.

Halafu hii sio chanjo ya kwanza kuwaletea huko Afrika. Tumeleta chanjo nyingi na mmezitumia bila kelele. Chanjo za polio, surua, homa ya ini, tetekuwanga etc. Tungetaka kuwaua si tungetumia chanjo hizo? Kwanini tusubirie ya corona?

Baadhi ya nchi za Afrika mmeanza kuharibu miundombinu ya teknolojia ya 5G kwa kuihusisha na Corona. Hili si jambo la kushangaza kwa sababu mnaua hadi mama zenu wa kuwazaa kwa kuwahusisha na uchawi. Kwa sababu tu ya ngozi zao kusinyaa kwa uzee na macho yao kuwa mekundu kwa kutumia nishati ya kuni, kwenu huo ni ushahidi wa uchawi. Mnawaua bila huruma.

Muda si mrefu mtaanza kuwaua wagonjwa wa Corona kwa kuhisi wamelogwa au wametupiwa mkosi. Haya ndio mawazo ya watu wapumbavu, wasioelimika na washamba kama nyie. Watu ambao mnaamini eti kila nyumba ya tajiri ina chumba maalumu cha kufuga majoka yanayomletea hela.

Sikikizeni nyie wapumbavu. Kama chanjo ya Corona ingegunduliwa Afrika, viongozi wenu wasingeitumia. Wangesafiri kwenda India au nchi za Ulaya kutafuta chanjo nyingine.

Viongozi wa Afrika hawaamini katika huduma za afya za nchi zao. Hawaamini hospitali zao, hawaamini madaktari wao, hawaamini hata dawa zao. Ndio maana wakiugua hata malaria tu wanapanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwahiyo wakati mkiwaza eti wazungu wanataka kuwaua kwa chanjo ya corona, viongozi wenu nao wanawaza mnataka kuwaua kwa huduma mbovu za afya. Ndio maana wanajenga hospitali lakini hawatibiwi humo, wanasomesha madaktari lakini hawawaamini. Wanakimbilia kutibiwa nje. Wanajenga shule lakini watoto wao hawasomi humo.

Chanjo ya Corona ni kengele ya kuwakumbusha waafrika kuchagua viongozi wenye maono na uwezo wa kupambana na matatizo yao. Afrika ingekuwa na uongozi thabiti ingekua bara tajiri zaidi duniani. Lakini kwa sababu ya ujinga wenu wa kuchagua viongozi wasio na maono, wameuza rasilimali zenu kwa wazungu na Wachina, kwa faida yao na familia zao, huku wananchi mkiteseka kwa umaskini.

Utajiri mwingi wa Ulaya, Marekani na China umetoka Afrika kwa sababu ya upumbavu wa viongozi wenu. Badilikeni. Kabla hamjalaumu wazungu, jilaumuni kwanza wenyewe kwa kuchagua viongozi goigoi.!

Nini maoni yako?
AS RECIEVED
 
Kweli kabisa mkuu. Mfano mzuri marekani. Tokea Joe Biden aingie na kuharakisha kushughulikia covid 19 vifo vimepungua sana baada ya kuwapa wananchi wao chanjo. Ila hapa kwetu watu wengi sana mpaka wasomi wanaamini mabeberu wanataka kutuua!!! Yaani mzungu akitaka kutuwipe out hahitaji kutengeneza chanjo. Anatuua kupitia vitu vyao tunavyovitumia. kila kitu chetu tunachotumia ni cha mzungu!!!! Ndiyo maana Mungu anasikitika sana anasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa". Mtu mweusi hana maarifa kabisa. Eti chapa ya 666!!! Kuogopesha watu tu!!!!
Hii inadhihirisha maana halisi ya kuwa ulimwengu wa tatu yaani Kila kitu ikiwemo uwezo wa kupambana na magonjwa kuwa chini Sana.
Wazungu hawakukosea kutuweka hilo kundi sababu watu hawana mbele Wala nyuma mnaletewa msaada tena mnaanza kuhoji wakati hata mpewe miaka elfu hakuwezi kutengeneza hiyo chanjo.
 
Mimi naona gwajima hoja zake zina msingi na anataka kupatiwa majibu sio kumsimanga na watu wengi upeo wao wa kufikilia ni mdogo kujibu hoja za Gwajima watakalia kumsimanga
 
Back
Top Bottom