Askofu Benson Bagonza: Penye jina CHADEMA weka CCM

Askofu Benson Bagonza: Penye jina CHADEMA weka CCM

Hawa ndio maaskofu sio walamba makalio na wacheza sinema za utupu na kondoo wa bwana , sasa huyu utamlinganisha na hii Pimbi hapa chiniView attachment 1568230
Hujui......Wakitaka tuwapende lazima wafanye kama zamani, ndipo tutakapowakubali kuwa nao ni ma Askofu kama hao wengine wanaotupigia chapuo!.....Sijui.....Kuanzia sasa ujue, tunatangazia dunia hivi; Askofu yeyote akiwa upande wetu, huyo siyo adui yetu maslani!
Screenshot_20200724-175445.jpg

ONA SASA PENDEZAAA EEHEEE!
 
Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____

1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!
Huyu mzee ni akili kubwa sana.
 
Hivi Watu Wa Huko Wanakula virutubisho gani Maana ukiacha hao wawili kuna Yule Padri Privatus Karugendo na Yule Karugendo Mwingine Alikuwa Anaandika Makala ndani ya gazeti la Rai?!!
Haya maandishi yanaonyesha kuwa unawakubali hawa watu. Kongole.
Ukweli utakuweka huru.
 
Huyu ndy askofu anaitendea vyema elimu yake ya dini,huyu ndy anaijua uaskofu nini mana yake (education,religion and politics) ..hivi haviachani ndy mana advanced level haijalishi wewe ni mpagani lakn kwny GS lazma usome hivi....kule Rwanda kipindi fulani waliweka vigezo vya uchungaji...Asante askofu kwa kuitendea vyema elimu yako!!endelea kuweka nuru penye giza na haki penye dhuruma!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Maskofu mjinga sana.unajifanya unajua falsafa kuliko wengine.kama unataka kuwa mwanasiasa si uvue hilo likofia kichwani ukaingie Kwenye siasa.matendo yenu Mabofu ya sili mbona yanajulikana lakini hakuna anayewasema.shame on you
 
Jiwe ana mke wa pili humu JF Mtatambua tu kwa comment zake kama umemtambua embu mtaje bila hata mficho
 
Back
Top Bottom