Askofu Benson Bagonza: Penye jina CHADEMA weka CCM

Viva Magu
Heil JPM

Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____

1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!
 
Hivi Watu Wa Huko Wanakula virutubisho gani Maana ukiacha hao wawili kuna Yule Padri Privatus Karugendo na Yule Karugendo Mwingine Alikuwa Anaandika Makala ndani ya gazeti la Rai?!!
 
Ndio unaleta kura kwa Chadema [emoji3][emoji3][emoji3]
Nyinyi mmebakia kukubalika na watu wa aina hii, na wenyewe wamesha anza kuwatema
tapatalk_1574537881507.jpg
 
Bagonza agombee hata udiwani kupitia Chadema aone atakavyogaragazwa
Mzee kakosa pumzi, kuna vitu wanantamani lakini wanaogopa,
Kwa nini asijitoe mhanaga kama Gwajima?
Bagonza anatuaminisha kuwa chadema hawakosei?
Na kama anahisi wanaonewa kwa nini asiwe wazi kama mshauri wao kwenye mambo ya kisheria na awasimamie wasikosee?
Je bagonza anataka kusema endapo mtu atakosea na kwenda kinyume na kanuni za jamii na kanisa pale kwake hawezi kumsimamisha au kumfukuza kwenye kanisa?
Au kumsimamisha kushiriki kitu inaitwa ekaristi takatifu, au Meza ya bwana?
Mwisho nimuombe askofu aachane na vimafumbo vya kwenye kanga au mke mwenza,
Kama anapenda chadema basi ahamie huko ambako ni CHAMA cha maraika.
 
Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____

1. Kama Tume ya Uchaguzi (NEC) ikifanya makosa, ukaikosoa lakini ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini kwamba makosa ya NEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

2. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue vyombo vya dola vinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa CHADEMA wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa CHADEMA ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (NEC). Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CHADEMA wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa CHADEMA hawana Imani na sanduku la kura. Penye jina CHADEMA waweza kuweka CCM.

5. CHADEMA wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku CHADEMA wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye jina CHADEMA waweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.!
BABA ASKOFU HUJAWAHI KUSEMA UPUMBAVU
 
Nilikwenda Ngara Nikaonyeshwa
Ambako Huduma Za Bishop Zinatolewa. Kule Ngara Wapo Hawa Wawili
Bishop Bagonza
Bishop Niwemugizi
Rulenge Ngara Kagera Tanzania
Huduma safi na mazingira mazuri,mimi nasali kwa Bagonza
 
Back
Top Bottom