KERO Askari wa Hifadhi ya Taifa, Nyerere tuna UGUMU WA MAISHA na tunadai posho

KERO Askari wa Hifadhi ya Taifa, Nyerere tuna UGUMU WA MAISHA na tunadai posho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari;

Mimi ni askari wa hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ninayefanya kazi katika hifadhi ya Taifa Nyerere. Kwa kipindi kilefu askari wa hifadhi tumekuwa tukipitia ugumu wa maisha kutokana na kadhaa kama ifuatavyo

I) kutokulipwa staiki zetu Kwa Wakati, lakin pia Malipo ya staiki mbali mbali yamekuwa ni kidogo kiasi kwamba hayawezi kutusaidia kujikimu na ugumu wa maisha mfano Askari Analipwa pesa ya nyumba TSH elfu 60000 Kwa mwezi kiasi ambacho hakiwezi kutosha hata kulipia pango la chumba kimoja.

II) OC ambayo imekuwa ikiletwa hifadhini Maofisa wahifadhi"Viongozi "wamekuwa wakigawana wao tu na kuwaacha Askari bila malipo yeyote ama kuwalipa kiasi kidogo kama kuwaridhisha tofauti na kiasi wanacho dai, mfano saiv tuna miezi 4 hatujalipwa posho Hali inayopelekea kushuka Kwa morali ya kazi,

III) Mishahara tunalipwa tar 30, wakati taasisi nyingine mishahara hulipwa tar 23-25

Tunaomba mtusaidie kutusemea kwa Viongozi ili wajue magumu tunayopitia mpaka tunaelekea kukata tamaa ya kutunza hizi maliasili zetu
 
Back
Top Bottom