Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 139
- 147
Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewakabidhi TANAPA Malori matano na mitambo mitano yenye thamani ya Dola milioni 2.4 sawa na shilingi Bilioni 6.4 za Kitanzania, tukio hilo limefanyika leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Mpingo House) jijini Dar es salaam.
Vifaa hivyo viliyonunuliwa kupitia mradi wa Dharura kwa Uhifadhi na Utalii Tanzania (Emergency Recovery Support for Biodiversity in Tanzania) kupitia benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW).
Akizungumza katika makabidhiano haya Balozi Dkt. Chana alieleza kuwa vifaa hivyo vitaboresha shughuli za Uhifadhi pamoja na miundombinu katika Hifadhi za Taifa Serengeti na Nyerere kwa malengo ya kupunguza athari zilizosababishwa na janga la UVIKO-19 kwenye Utalii na Uhifadhi.
Dkt. Chana alisema “Nawaagiza Bodi na Wakuu wa Mashirika ya TANAPA na TAWA kuhakikisha kuwa vitendea kazi hivi vinatumika kufanya kazi zilizokusudiwa za Uhifadhi wa Maliasili na Utalii na vinatunzwa ipasavyo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za matumizi ya vifaa vya Serikali.”
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhanini TANAPA Jenerali mstaafu George Waitara alishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kusaidia uhifadhi nchini Tanzania hasa katika miradi ya dharura.
“Msaada huu wa dharura umetuwezesha kuvuka kipindi cha dharura ya uviko 19 katika Uhifadhi na kuendelea kuimarisha miundombinu yetu bila kuyumba. Kwa kufanya hivyo, mifumo ya Ikolojia iliendelea kushamiri ndani ya Hifadhi za Taifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) Tanzania, Dkt. Ezekiel Dembe alieleza mafanikio ya miradi mbalimbali inayotekelezwa Tanzania kwa kusema “Frankfurt Zoological Society imekuwa Tanzania kwa zaidi ya miaka 65 kwamba tunajivunia kufanya kazi na Wizara ya Maliasili na Utalii, TANAPA, TAWA na wadau wengine wote tunaofanya nao kazi kwa sababu wamekuwa wakitekeleza makubaliano ya mikataba ipasavyo”.
Mradi wa Usaidizi wa dharura kwa Uhifadhi na Utalii nchini Tanzania umesaidia juhudi za kutoa msaada wa haraka na mipango ya muda mrefu ya kurejesha na kulinda mifumo ikolojia mbalimbali ya Tanzania, hasa pale ambapo vitisho vikubwa kama mabadiliko ya tabianchi, ujangili, au majanga ya asili yanayosababisha uharibifu kwa wanyamapori na makazi yao, juhudi za mradi zinahusisha ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Ujerumani, Shirika la Frunkfurt Zoological Society pamoja na jamii za wenyeji ili kudhibiti na kuimarisha ustahimilivu wa bioanuwai nchini.