DOKEZO Askari Polisi atuhumiwa kumuua raia Arusha kwa kumpiga risasi 3, Wananchi wamtuhumu kwa mauaji ya mara kwa mara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Israel Daudi, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi 3 na askari Polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuachia ng'ombe kuingia shambani.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Olaresho, Kata ya Olasiti katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia tukio hilo Diwani wa Kata ya Olasiti, Alex Martin amesema hilo ni tukio la pili kwa askari huyo kufanya mauaji katika Kata hiyo ya Olasiti kwani huko nyuma alishafanya mauaji na Wananchi walitaka kumuua askari huyo lakini diwani aliingilia kati kwa kumuepusha askari huyo kuuliwa na Wananchi.

Lakini cha kushangaza askari huyo amerudia tena kufanya mauaji katika kata hiyohiyo.

Diwani Alex ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutotumia nguvu na mabavu kwa raia wake pasipo sababu.

Wananchi waomba sheria ichukue mkondo wake.

===

JamiiForums imefanyia kazi suala hili, soma: Askari Polisi amuua raia Arusha kwa kumpiga risasi 3. Wananchi wamtuhumu kwa mauaji ya mara kwa mara
 
Hii habari haijabalance kuna mtu huko olasit alisema huyo kijana alikaidi amri ya kuingiza mifugo shamba lilokuwa likilindwa na walinzi wa kampuni binafsi.

Askari hao walipoona wanazidiwa nguvu na watu wakaomba msaada polis, polis walipofika wakataka ajisalimishe lakin aliendelea kuwafuata akiwa na silaha za jadi risasi kadhaa zikapigwa hewani lakin hakutii ndipo wakafyatua kiuno..
 
Hii habari haijabalance kuna mtu huko olasit alisema huyo kijana alikaidi amri ya kuingiza mifugo shamba lilokuwa likilindwa na walinzi wa kampuni binafsi, Askari hao walipoona wanazidiwa nguvu na watu wakaomba msaada polis, polis walipofika wakataka ajisalimishe lakin aliendelea kuwafuata akiwa na silaha za jadi risasi kadhaa zikapigwa hewani lakin hakutii ndipo wakafyatua kiuno..
Wachungaji huwa ni hatari sana kwa kutumia silaha zao hasa fimbo na manati. Wanajua sana kumrushia mtu ikawa ni silaha hatari kuliko hata bunduki. Pia kuchapa hupewa mafunzo maalum.

Ng'ombe huingia shambani bahati mbaya hasa kwa kusinzia. Akishtuka anakuta wameingia, sasa kwa uoga huenda kureport kuwa amepigwa na ng'ombe kuzuiwa, so team ya wenye Ng'ombe wanakuja kulianzisha.
Hapo ni ngumu kujua kipi ni kipi. Ila wachungaji ni tatizo.
 
Back
Top Bottom