Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Hajaingilia dirishani kumbuka wote wawili walizunguka nchi nzima wakiomba kura.
Hata kule US ikitokea Biden mwenye miaka 79 akafariki yule mama anachukua nchi.

Acheni dharau kijana.
 
Katiba mpya au iliyoboreshwa ni nzuri Sana

Lakini je hao waandishi wa katiba mpya ni wakina Nani?

Tusije kukuta tunaleta vitu vya ajabu
Tunataka katiba mpya.

Uboreshwaji unafanyika kila Leo lakini ngoma ni ile ile. Uboreshwaji unawahusisha wabunge tu, katiba mpya inahusisha kuchkua maoni kutoka kwa Wananchi.

Mama atateua watu reliable. Na ndio maana tunasema Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
Ni wazo zuri lakini sio wakati sahihi.Panahitajika political willingness ya hali ya juu sana kufanikisha wazo hili.Nazungumzia utayari wa watu Ku sacrifice masilahi yao ya sasa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,siuoni utayari huo katika taifa hili kwa sasa.
 
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.

Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???

Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
Lakini kuna amani na utulivu kwa sababu ya hivyo vitabu.
 
Unazijua gharama za uchaguzi!!?
ama unaongea ilimradi
Bilioni 157 hzo ndo gharama za uchaguzi kwa mujibu wa tume ya uchaguzi pia unapozungumzia kutekeleza katiba au jambo la emergency gharama hazingaliwi pia hv unadhani wameweka terms za miaka 5 ndo ufanyike uchaguzi kwa kukwepa gharama?
 
Kweli kabisa hii itasaidia kutokuwa na uwezekano wa makamu kumuwekea sumu Raisi na kujipitisha akijichekesha kwamba Raisi katestiwa kidogo ila anaendelea vizuri huku anajichekesha🤣🤣🤣
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
 
Ila katoa mapendekezo mazuri sana,Raisi ikitokea kafariki uitishwe uchaguzi baada ya miezi miwili,mitatu mingi sana anaweza nogewa
Kwa maoni haya ni wazi kuwa umevurugwa kama wale wasiotaka kuamini awamu ya tano imekwisha na sasa tuko awamu ya sita.

Pole eeh.
 
Back
Top Bottom