Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,403
2,000
Kwa heshima naomba nkuvulie kofia niliyovaa wakati huu naandika huu uzi.

Wakati historia inaandikwa juu ya upatikanaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maxence Melo tutamtambua kama prominent figure wa kwanza kabisa kutoka hadharani na kumuomba Mheshimiwa Rais Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan kutupatia katiba mpya.

Mkurugenzi huyu mtendaji wa Jamii Forums alilitoa ombi hili maalumu kwa Mheshimiwa raisi alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 hivi karibuni juu ya masuala mbali mbali.

Najua wapo wengi ambao wanatamani kupatikana kwa katiba mpya na wamekuwa wakilipigia kelele suala hili kwa muda mrefu sana, kwa mfano viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za kibinaadamu kadhaa. Lakini Maxence Melo yeye sio kiongozi wa chama cha upinzani wala sio mwanaharakati wa haki za binaadam, yeye ni mdau mkubwa wa sekta ya TEHAMA na hili ndilo lililonifanya kuandika uzi huu wa kumbukumbu maana kwa wadau wengi wa habari katika zama hizi wamekumbwa na uoga wa hali ya juu kiasi kwamba wanashindwa kutoka front na kutoa/ kuongelea mambo ya msingi kama haya.

Mheshimiwa Rais wa Awamu ya sita Mama yetu Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mtu msikivu, mwelewa, mkarimu, Muogopa Mungu haswa, mkweli, mpole, mwenye huruma, mwenye upendo wa kweli na sio wa maigizo, mnyenyekevu na mzalendo.

Hili linanifanya mimi binafsi kuamini kwamba Mama hatotoka madarakani In Shaa Allah mpaka ahakikishe ametuachia katiba mpya.

Mtu yoyote mwenye mapenzi ya dhati na ya kweli kwa nchi hii ataelewa kwamba katiba tuliyonayo sasa ina dosari kubwa sana na za msingi ambazo hata jitihada gani zichukuliwe basi ni vigumu sana kupiga hatua. Hivyo basi, jambo la kwanza kabisa kulifanya ili nchi yetu hii ipige hatua za dhati za maendeleo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa.

Kwako mheshimiwa rais, mimi binafsi naomba kutilia nguvu hoja ya Maxence Melo kwamba huu ndio wakati sahihi wa kuliendea jambo hili. Usisubiri muda uende zaidi Mama. Hii ndio legacy yako Mama na hakika nchi hii itakukumbuka for hundred and thousand years to come.

Wasiolitakia mema taifa letu wasikutishe wala kukurudisha nyuma katika adhma hii. Tunatambua ulituambia tusubiri kidogo, lakini mama hakuna ajuae kesho yake.

Waswahili walisema ngoja ngoja huumiza matumbo, na chelewa chelewa ukute mwana si wako. Muda ni sasa Mama yetu kipenzi. Nenda ukaandike historia, nenda ukawakomboe kiukweli wanyonge wa nchii hii.

Kwa wananchi: Tunaendelea kusisitiza kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

Viva Mama Samia! Muda ni sasa!
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,403
2,000
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Sawa ila kwa sasa wacheni ujuaji.

Tume ya warioba ilipopita kukusanya maoni hukutoka, ukatuona sisi tuliokwenda kutoa maoni ni wajinga. Leo unajifanya una kimbelembele cha kutoa maoni.

Tulia kwanza mama aliweke sawa hili halafu maoni yako yataanza kupokelewa. Wewe unadhani uchaguzi wa rais unafanyika tu kiholela holela???
 
Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
12,403
2,000
Katiba mpya ndio kaburi la chama chakavu
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.

Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???

Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,462

Usipofuata biblia, utaishia tu kutengwa na kanisa... USIPOFUATA KATIBA.. GEREZA LINAWEZA LIKAKUHUSU
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
5,001
2,000
Nrudia tena katiba mpya ndio kabur la chama chakavu,kama vp muulize mzee wa msoga nn kilimfanya ageuke mwishon ktk mchakato wa kutafuta katiba mpya????
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.

Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???

Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Kwa heshima naomba nkuvulie kofia niliyovaa wakati huu naandika huu uzi.

Wakati historia inaandikwa juu ya upatikanaji wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maxence Melo tutamtambua kama prominent figure wa kwanza kabisa kutoka hadharani na kumuomba Mheshimiwa Rais Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan kutupatia katiba mpya. Mkurugenzi huyu mtendaji wa Jamii Forums alilitoa ombi hili maalumu kwa Mheshimiwa raisi alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 hivi karibuni juu ya masuala mbali mbali.

View attachment 1809190

Najua wapo wengi ambao wanatamani kupatikana kwa katiba mpya na wamekuwa wakilipigia kelele suala hili kwa muda mrefu sana, kwa mfano viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za kibinaadamu kadhaa. Lakini Maxence Melo yeye sio kiongozi wa chama cha upinzani wala sio mwanaharakati wa haki za binaadam, yeye ni mdau mkubwa wa sekta ya TEHAMA na hili ndilo lililonifanya kuandika uzi huu wa kumbukumbu maana kwa wadau wengi wa habari katika zama hizi wamekumbwa na uoga wa hali ya juu kiasi kwamba wanashindwa kutoka front na kutoa/ kuongelea mambo ya msingi kama haya.

Mheshimiwa Rais wa Awamu ya sita Mama yetu Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mtu msikivu, mwelewa, mkarimu, Muogopa Mungu haswa, mkweli, mpole, mwenye huruma, mwenye upendo wa kweli na sio wa maigizo, mnyenyekevu na mzalendo. Hili linanifanya mimi binafsi kuamini kwamba Mama hatotoka madarakani In Shaa Allah mpaka ahakikishe ametuachia katiba mpya.

Mtu yoyote mwenye mapenzi ya dhati na ya kweli kwa nchi hii ataelewa kwamba katiba tuliyonayo sasa ina dosari kubwa sana na za msingi ambazo hata jitihada gani zichukuliwe basi ni vigumu sana kupiga hatua. Hivyo basi, jambo la kwanza kabisa kulifanya ili nchi yetu hii ipige hatua za dhati za maendeleo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa.

Kwako mheshimiwa rais, mimi binafsi naomba kutilia nguvu hoja ya Maxence Melo kwamba huu ndio wakati sahihi wa kuliendea jambo hili. Usisubiri muda uende zaidi Mama. Hii ndio legacy yako Mama na hakika nchi hii itakukumbuka for hundred and thousand years to come. Wasiolitakia mema taifa letu wasikutishe wala kukurudisha nyuma katika adhma hii. Tunatambua ulituambia tusubiri kidogo, lakini mama hakuna ajuae kesho yake.

Waswahili walisema ngoja ngoja huumiza matumbo, na chelewa chelewa ukute mwana si wako. Muda ni sasa Mama yetu kipenzi. Nenda ukaandike historia, nenda ukawakomboe kiukweli wanyonge wa nchii hii.

Kwa wananchi: Tunaendelea kusisitiza kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

Viva Mama Samia! Muda ni sasa!
Katiba mpya inaweza kuandikwa lakini ikawa mbovuuuu kuliko hata iliyopo sasa hivi.

Katiba nzuri ya wananchi haiwezi kuandikwa na wanasiasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom