Arusha sasa ni Salama - Kikwete

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Rais Jakaya Kikwete amewapongeza wakazi wote wa Arusha kwa kurudisha amani iliyokuwa imepotea.

Rais amesema kamwe serikali yake isingeruhusu mkutano wa kimataifa kufanyika Arusha katika hali ya sintofahamu iliyokuwepo kabla.

Rais ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosambazwa kwa vyombo vya habari muda mchache uliopita.

Rais amesema mkutano wa kimataifa uliofanyika Arusha ni kutokana na juhudi za wakazi wa Arusha kurejesha amani iliyokuwa imepotea.

Amewasihi wakazi wote wa Arusha kuendeleza amani iliyopo ili jiji hilo liendelee kutambulika kama Geneva ya Afrika.

Rais amemalizia kwa kusema Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 
Amani iliyokuwa imepotea? Naomba kuelimishwa jamani, juu ya kauli hii.
 
Mkuu nadhani anakumbushia polisi walivyovamia maandamano ya amani ya CDM na kufanikiwa kuua wanachama watatu.Pia vurugu walizokuwa wanamfanyia mbunge aliyeporwa ubunge Godbless Lema
 
Hatimaye kauli ya Lema aliyosema kuwa kuvuliwa kwake ubunge ilikuwa ni planned process imedhihirika rasmi. Walk on the words of the so called president Kiwete you will realize it!. Kwa hiyo kiwete anataka tuamini kuwa Kamanda Lema alikuwa kikwazo cha amani na kuvuliwa kwake ubunge ndio kumeleta amani!!??
 
Uzuri mmoja hotuba zake zote anaandikiwa, akili yake haihusiki na hayo aliyoyasema. Kauli yake ikiwa tata, sii utata kwake bali kwa wasaidizi wake. Ni kweli amani imeanza kurejea baada ya wauaji wa mwenyekiti wa Chadema kukamatwa. Ni matumaini yetu kuwa hata wale polisi walioa raia wasiokuwa na silaha watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
.
 
Huu ni mwisho wa ubaya! Ni aibu la laana! Kikwete nenda hijja labda mungu atakusamehe na kukurudishia akili na haiba yako! at this point umekwisha baba! Kwa kauli yako hii aah! Mh. Lema alisema kweli.
 
waitishe uchaguzi wa ubunge Arusha Mjini ndio watajua maana ya ukimya wao wa sasa.
 
ni kweli maana mr maandamano now hana power amejitaid kukishawishi chama kifanye ziara ili apate posho kwa maana ana hali mbaya
 
Hatimaye kauli ya Lema aliyosema kuwa kuvuliwa kwake ubunge ilikuwa ni planned process imedhihirika rasmi. Walk on the words of the so called president Kiwete you will realize it!. Kwa hiyo kiwete anataka tuamini kuwa Kamanda Lema alikuwa kikwazo cha amani na kuvuliwa kwake ubunge ndio kumeleta amani!!??
Nimeipenda the so called president
 
Arusha tumekuwa na amani maisha. Kumekuwa na siku ambazo polisi wamewavamia wananchi ambazo ni chache sana! Huyo analipuka tu!
 
Mkuu nadhani anakumbushia polisi walivyovamia maandamano ya amani ya CDM na kufanikiwa kuua wanachama watatu.Pia vurugu walizokuwa wanamfanyia mbunge aliyeporwa ubunge Godbless Lema

tabu kiongozi wetu ni mtoto wa kiswahili kwani wamezoea mipasho mda wote,alitakiwa kusema ni amani ipi mbona watu tunakula good time 24 oclock
 
Uzuri mmoja hotuba zake zote anaandikiwa, akili yake haihusiki na hayo aliyoyasema. Kauli yake ikiwa tata, sii utata kwake bali kwa wasaidizi wake. Ni kweli amani imeanza kurejea baada ya wauaji wa mwenyekiti wa Chadema kukamatwa. Ni matumaini yetu kuwa hata wale polisi walioa raia wasiokuwa na silaha watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
.

hapo kwenye green ni upuuzi mtupu! Hizi propaganda za "tatizo ni wasaidizi wake" mkazipeleke huko msoga! Huku tuna akili zetu!
 
Arusha ina amani ni siasa tu za kutokukubaliana na kushindwa ndizo zinazoaribu jiji hili.
 
Back
Top Bottom