Maneno haya ya Mh. Rais nimaneno ambayo yamelenga kuvunja mioyo ya wengi na kuwafurahisha wachache, wenye kufaidika na mfumo huwo wa dhuluma. Najua Rafiki yangu Godbless Lema amesikia kauli hiyo, huenda akaijibu mapema sana leo ama kesho ama sasa ama akaipuuza kauli hizo za kejeli.
Mimi kama mimi HENRY J KILEWO Mwananchi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Naifananisha kauli hii kama kauli ya mtu 'aliyeshindwa kuwatumikia Wananchi wake na kuanza kutafuta mchawi wake' Wananchi wa ARUSHA wanampenda mbunge wao na huenda wakampata mapema sana leo ama kesho ama saa watakayoamua, Cheo hakiwezi kupora haki ya mtu ama utu bali huchelewesha tu. Tazama viganja vyako vya mikono. Je, Vinamistari ? Na kama ipo, je! kuna mtu anayeweza kuifuta? Kama hakuna, Basi hakuna mtu anayeweza kuzuia, haki,utu na usawa wa mwanadamu.
Tuendeleeni kumuomba mungu tutayaona mengi zaidi ya haya naamini mungu anakusudio lake na atatenda Makubwa mapema leo ama kesho... Watashindana na sisi lakini hawatashinda. WATATUUA KWA RISASI ZA MOTO, WATAKUFA KWA PRESHA YA DHAMBI, MSIOGOPE MUNGU YUPO UPANDE WETU.