Rais Samia: Serikali Yangu Sio ya Maneno ni ya Vitendo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo ataongoza maadhimisho siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya itakayofanyika kitaifa mkoani humo tarehe Juni 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda.

Rais Samia amezungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema..."

Rais Samia aliwajibu akisema
"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi (huku akiweka mkono wake masikioni) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya”

Wanajamvi, Rais wa Nchi kasema sisi tuseme tu yeye anapiga kazi tu
---

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati aliposimama kuwasalimia wakazi wa Tengeru mkoani Arusha amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda. Rais Samia amesema:

"...Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya...”
---

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Credit: Clouds Media
 
B3C4DFFA-0E07-4DAD-BD2C-458FFF73B16D.jpeg


Kama ana hata chembe ya aibu , basi ajiuzulu haraka.., na hatuachi hadi ajiuzulu au wajitoe kwa lazima kwenye huo mkataba usio na kikomo, hata tukipelekwa mahakamani, potelea mbali.
 
Mini sijaelewa aliposema yeye ni vitendo tu.Ni vitendo vip sasa anavyofanya?toka ashike madaraka hamna vitendo vyenye tija kwa wananchi zaidi ya maumivu kwa watu.tumeona ameongeza tozo lukuki,umeme bei juu,mafuta bei juu na sasa ameamua kuuza bandari za tanganyika na kuziacha za zanzibar
 
Sijawahi kwenye maisha yangu kuwa na mashaka na rais yeyote, ila huyu mama hapana!

Tangu aliposema ukiscratch my back i will scratch yours,mmmhh wanawake tunajuana tu udhaifu wetu japo sio wote, ila kwa mama huyu alopata urais kwa kudra, hapana kabisa imani naye!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom