Arusha: Mtifuano wa machinga soko la Kilombero

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
955
Mji wa arusha umechafuka ghafla baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo mjini hapa kuvamia eneo lililouzwa na aliyekuwa meya miaka ya nyuma. Eneo hilo liko karibu na soko la Kilombero.

Hali hiyo imekuja baada wa manispaa ya arusha kukamata bidhaa za wafanyabiashara hao ambapo eneo walilokuwa wamepangiwa kuwa dogo kuliko wafanyabiashara hao.


IMG-20120927-WA0006.jpg

Umati wa watu wakiwa wanaandamana kuvunja uzio na kuweka soko mikononi mwao
IMG-20120927-WA0018.jpg

Hali ilipo zidi kuwa tete yakaongezeka Mawili
 
Wamachinga wamevamia uwanja wa Kilombero na kung'oa uzio wa mabati na kuchoma vitu vyote na kujigawia maeneo ya kufanyia biashara. Hali si shwari na risasi zinarindima mjini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwa wale walio karibu na soko la kilombero hapa Arusha tunaomba mtujuze kwa kina kinachoendelea hapo maana rafiki yangu kaniambia kuna mtifuano mkubwa sana wa wamachinga wamevamia na kubomoa uzio uliojengwa wakipinga kuhamishiwa nmc
 
Hakuna aliyepigwa na kitu chenye Ncha kali? Mpaka sasa hivi hawajafika kutuliza/kuwatawanya wafuasi wa chama cha upinzani (ccm)?
 
Kwa hiyo hawataki kuhamishiwa NMC...??

Mkuu issue ni kwamba NMC hapatoshi... Wengi wa waliokuwa maeneo ya sokoni wao hawajapata nafasi NMC, na sasa wanafukuzwa wanaambiwa huko....
Kosa kubwa lililofanyika hapa, ni huu mpango walikurupuka nao.. Wangetulia, wakaona NMC inaweza kubaba wamachinga wangapi, wangewaandikisha majina, na kuwagawia accordingly.... Haya ni matokeo ya kuingiza siasa chafu kila kona.
 
Kulikuwa na issue gani hapo??
Nasikia Kamanda Lema majuzi alikuwa na mkutano. Aliwalaumu Machinga kwa usaliti, kwamba walikubaliana na aliyekuwa Mbunge-Lema kutohama hadi watengewe eneo na kuwa eneo walopewa ni dogo, halina huduma muhimu na ni tindiga, mvua ikinyesha maji yanapanda juu.
Mgambo wa Jiji nao wameanzaoperesheni tangu juzi kuwaondoa machinga mitaani.
Eneo lililovamiwa lilikuwa wapewe wamachinga kabla hata ya 2010 lkn Jiji wakaliuza wakati wamachinga hawana eneo
 
Kwa wale walio karibu na soko la kilombero hapa Arusha tunaomba mtujuze kwa kina kinachoendelea hapo maana rafiki yangu kaniambia kuna mtifuano mkubwa sana wa wamachinga wamevamia na kubomoa uzio uliojengwa wakipinga kuhamishiwa nmc

Kuna mtu kanidokeza kwamba shule ya Arusha Sec, wameandika barua ya kupinga hilo soko karibu na shule yao,kwani wanashindwa kusoma kwa ajili ya kelele.
 
Huu ni upumbavu wa serikali ya jiji la Arusha! Kuna mkutano mkubwa unaendelea hapa kwahiyo limepita zoezi la kuwahamisha Wamachinga lakini ninavyoona hili zoezi baada ya mkutano huu kuisha serikali hii litawarudisha tena katikakati ya jiji!
 
Kuna mtu kanidokeza kwamba shule ya Arusha Sec, wameandika barua ya kupinga hilo soko karibu na shule yao,kwani wanashindwa kusoma kwa ajili ya kelele.

Safi sana, shule na soko wapi na wapi?
Nna uhakika hili soko linatolewa pale NMC mda sio mrefu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom