Arusha: Mtifuano wa machinga soko la Kilombero

Si walisema baada ya Lema kuvuliwa ubunge Arusha imekuwa shwari? vipi tena tunasikia machafuko?
Ni heri vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kukandamiza haki ya wanyonge.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Si walisema baada ya Lema kuvuliwa ubunge Arusha imekuwa shwari? vipi tena tunasikia machafuko?

Juzi Lema kawaambia watu wa Arusha huhitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu kutetea/kudai haki yako na akawaasa kutokuwa wabinafsi..
 
interejensia ya polisi ilishindwa kufanya kazi. hii ni mipango ya mda mrefu mbona??
58710_10151081305996811_1441004937_n.jpg

384456_10151081332876811_2052928567_n.jpg

mia

Jitafutieni Chakula cha watoto wenu! Wapuuzeni manispaa na meya wao wa kichina!
 
Viongozi wa artilali ya ccmq arishaq wanafikiria kwa jurymiaq malalio yao badala ya vichwa. Imagine pale nmc pana shule jirani sana. Wao wanapeleka happy soko kutakuwa na kusoma hapo? Au kwa vile watoto wao hawasomi hapo?
 
Huyo ndiyo kamanda LEMA moja wapo ya hazina za CDM

Unajua kilichotokea wamachinga waliitwa na mkuu wa wilaya akaongea mbovu sana juu ya Chadema na Lema kumbe Lema ana msikiliza maana alikuwa ameingiza vijana wake...
 
Kwenye facebook Julius Mtatiro ameandika kuwa waliopigwa katika eneo hilo ni viongozi wa CUF waliokuwa wanatangaza mkutano wao wa Jumapili. Anawalaumu Chadema kwa kupanga kundi la vijana kuwashambulia viongozi wake kwa lengo la kuwaua. Hii ina uhusiano na hiyo ya mpambano wa machinga katika eneo hilohilo?
 
Wamachinga wamevamia uwanja wa Kilombero na kung'oa uzio wa mabati na kuchoma vitu vyote na kujigawia maeneo ya kufanyia biashara. Hali si shwari na risasi zinarindima mjini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Polisi hawakutumia risasi, bali walikuwa kwenye jitihada za kuzima moto baada ya wamachinga kuchoma matairi.
OCD na Operations wa polisi Daudi walifika eneo la tukio, ilibidi wabaki wanaangalia na kusimamia ugawaji wa wamachinga.
Nadhani polisi wameogopa kutumia nguvu kutokana na ugeni mzito uliopo hapa Arusha.
 
Kwa wale walio karibu na soko la kilombero hapa Arusha tunaomba mtujuze kwa kina kinachoendelea hapo maana rafiki yangu kaniambia kuna mtifuano mkubwa sana wa wamachinga wamevamia na kubomoa uzio uliojengwa wakipinga kuhamishiwa nmc

Sasa kama rafikio kakuambia kama kuna mtifuano kwa nini usingemuuliza nini tatizo mapaka ikatokea hiyi mitifuano au unataka kusumbua watu tu hapa
 
Kwenye facebook Julius Mtatiro ameandika kuwa waliopigwa katika eneo hilo ni viongozi wa CUF waliokuwa wanatangaza mkutano wao wa Jumapili. Anawalaumu Chadema kwa kupanga kundi la vijana kuwashambulia viongozi wake kwa lengo la kuwaua. Hii ina uhusiano na hiyo ya mpambano wa machinga katika eneo hilohilo?
Mbona wanatangaza mkutano ni leo wakafika maeneo ambayo wamachinga wanajenga jenga vibanda baada ya kugawiana maeneo ndipo wamachinga hao wakaanza kuwazomea sasa walijuaje kama wale ni chadema na siyo CCM au machinga wote ni chadema na kama ni chadema walienda kufanya nini kwa wanachadema....
 
nipo arusha Polisi wamemwagwa wakutosha kutoka babati, karatu na moshi. nimepigiwa sim na rafiki yangu ambaye ni polisi anasema wamepewa amri ya kuja arusha kutona babati. wamebeba mabomu ya kutosha. na mkuu wa mkoa ameapa kukiua chama CA chadema kwa madai kuwa wao ndio wamesababisha wamachinga kuwa wakali

Mji wa arusha umechafuka ghafla baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo mjini hapa kuvamia eneo lililouzwa na aliyekuwa meya miaka ya nyuma. Eneo hilo liko karibu na soko la kilombero. Hali hiyo imekuja baada wa manispaa ya arusha kukamata bidhaa za wafanyabiashara hao ambapo eneo walilokuwa wamepangiwa kuwa dogo kuliko wafanyabiashara hao
 
Polisi hawakutumia risasi, bali walikuwa kwenye jitihada za kuzima moto baada ya wamachinga kuchoma matairi.
OCD na Operations wa polisi Daudi walifika eneo la tukio, ilibidi wabaki wanaangalia na kusimamia ugawaji wa wamachinga.
Nadhani polisi wameogopa kutumia nguvu kutokana na ugeni mzito uliopo hapa Arusha.
Hata mimi naona ni hivyo kwahiyo basi machinga wajipange...
 
Back
Top Bottom